Bunge letu linapoteza hadhi!

Bunge letu linapoteza hadhi!

Tatizo lililopo ni mfumo !
Inapaswa kutenganisha mihimili ya dola yaani Bunge, Mahakama na
Serikali. Vinginevyo mipasho na siasa za ki CCM hazitaisha bungeni na
bunge litazidi kupoteza maana ya kuwepo kwake ! Mpaka sasa ukiniuliza
umuhimu wa Bunge nitapata shida kujibu ! Ni kheri bunge lisiwepo
waendelee kuihoji serikali kwenye vikao vyao vya chama ! Maana bunge
sasa limekuwa kama kikao cha chama !!!!!!!!!!

ndg yangu hata party supremacy inaafect bunge kutokana na wingi wa wabunge kutoka chama tawala.
 
ndg yangu hata party supremacy inaafect bunge kutokana na wingi wa wabunge kutoka chama tawala.
Mihimili ikitenganishwa vyama vya siasa vitakuwa havina influence bungeni. Wabunge hawatakuwa na ndoto za uwaziri, na spika na viongozi wengine wa bunge hawatawekwa na chama
 
Wana JF taswira ya bunge letu imebadilika kiasi cha kutosha. Matumizi ya kiti cha spika kimekuwa kandamizi katika hoja zenye msingi na zenye maslahi kwa nchi hii. Pamoja na ukandamizaji huo "TIME WILL TELL". "THE UNKNOWNS WILL BE KNOWN VERY SOON". Mikataba ya kimataifa iliyotakiwa kuridhiwa leo haina maslahi kwa taifa hili. Inawajengea mabepari mazingira mazuri ya kuchota rasilimali za nchi hii. Mfano ni Kyoto Protocal, wenzetu hawaingii kichwakichwa, tumebaki kuwa carbon sinker viwanda vya wenzetu.
 
Leo napata kutoa jibu langu kwenu wazalendo juu ya CCM iliyojaa mi...bunge iliyojaa woga,hofu na mashaka.WAZALENDO WENZANGU,MUNGU huchukia sana mwanadamu mwenye tabia hizo tatu.BADALA YAKE huwapenda wanadamu waliojawa na Upendo,Ujasiri na Matumaini.Wazalendo wenzangu,kundi hili la pili daima hudumu katika uzalendo.Hivi tukitoa Quiz pale Bungeni kwa wawakikilishi wetu individually kwa swali"TOA MAANA MBILI ZA NENO MZALENDO",je tusingepata majibu ya vioja? Tukumbuke mwaka 1995 mzee John Malecela alipata kutoa salaam kwa spika kwa niaba ya ccm,alisema"Mheshimiwa spika kwa niaba yangu na chama cha mapinduzi,napenda nikuhahakishie kwamba hoja yoyote itakayoletwa humu bunge na serikali hii ccm,TUTAIPITISHA TU".Ndugu WAZALENDO,maneno hayo ya Mzee John ni dhahiri wazi kwamba wabunge wa ccm wamejawa na 'anti-citizenry elements',nini maana yake? Maana yake ni kwamba wabunge hawa wana mioyo miwili[uchama 52% na uzalendo 48%],kwa maana hiyo,wabunge wa ccm ni waumini wa sera za woga,hofu na mashaka ambazo huanzia kwenye 'party caucos' ambapo watoa mada hutumia lugha za vitisho kuwazuia wabunge walioaminika kuwa ni wazalendo.Tujiulize wako wapi wabunge hawa?DEO FILIKUNJOMBE,ANNA KILANGO,SAMWEL SITTA na wengine kwa muktadha?Itachukua muda mfupi ujao Mwenyeenzi Mungu asikie kilio cha Wazalendo kwamba atupe wabunge wenye upendo na nchi yao,wenye ujasiri wa kutetea rasilimali za nchi yao na wenye matumaini ya kubadiliisha hali ya nchi kiuchumi,kisiasa,kijamii,kiutamaduni na kiulinzi.Ndugu wazalendo kila mmoja anayetaka kugombea nafasi ya ubunge kupitia ccm afahamu kabisa atageuka roboti wa kulinda maslahi ya chama kwanza kabla ya uzalendo.MWAKA 2015 hakika tutashuhudia katika maeneo mengi Wazalendo[nje ya ccm] wakiibuka washindi kwa kuwa mgombea mzuri na makini lazima atoke ccm.NACHUKIA WOGA,HOFU NA MASHAKA.
 
Wabunge wa chadema wastaarabu sana, mimi sina muda wa kuvumulia upumbavu wa wazi huki nikiomba muongozo, hivyo siwezi kukaa kwenye bunge la kishoga kama hili kuendekeza upuuzi huku wana nchi wana shida wza kutupa
unadhani hapo kwenye bold nyekundu kulikuwa na ulazma wa kutukana?
 
Umakini wa bunge.
Ndugu wana nchi,nalishukuru bunge kwa kuendelea kuwa makini na matatizo ya wana nchi hasa kwa wale wachache wanao tanguliza maslahi ya wananchi wote.nasema ni kwa wachache kwa sababu kuu moja tu.nayo ni pale ambapo zinaibuliwa hoja na zinafukiwa na wanene kama ambavyo muheshimiwa mbatia na lowasa,tundu na wengine kuhusu carriculum ya elimu.

Tuache hilo:wizi wa makampuni ya simu kama alivyo liibua mbunge mmja likihusu ezypesa na zantel. Leo nawapa jingine nikiamini wabunge mahili na wanasheria makini kama tundu,taslima,mwakyembe na wengineo watalivalia njuga.

Kuna kitu katika sheria kinaitwa standard form contract ambayo katika mkataba upande mmoja unaunda taratubu na upande mwingine una amua kuingia mkataba au kuacha kwa kingereza tuna sema:terms are made by one part and the other part decides to be bound by them or not.

Leo hii ukituma uujumbe katika mtandao wa airtel unakatwa shilingi 125 eti ukituma badae ukatwe shs moja. Pia ukipiga mtandao mwingine mpokeaji akawa hapatikani,au akachelewa kupokea ela huanza kukatwa eti utume ujumbe wa sauti. Hii haima makubaliano wowote na mwenye simu.

Kwa maana hiyo ama tunazuiliwa uhuru wetu wa kutuma ujumbe kwa viwango vya kiserikali kisheria au tuma ibiwa.tafadhari fatilien. Na kama vipi viongozi wanao husika wawajibike
 
Habari ndio hiyo sio woga bali kukosa uzalendo kwa taifa lao MACCM ni zaidi ya ujuavyo
 
Leo ndugu zangu wana JF napenda tubadilishane mawazo juu yamajukumu ya Bunge letu kulingana na kinachoendelea katika kipindi hiki cha bunge. Mimi huwa najiuliza kuhusu majukumu ya Bunge, ambayo huwa tunajua kuwa moja wapo ya majukumu yake ni kutunga sheria.

Kwa muda mwingi Bunge letu kazi yake kubwa huwa kuletewa miswaada ya sheria, kuipitia, kuikubali, kuirekebisha na wakati mwingine kuikataa (kwa kifupi kuipisha).

Mara chache wabunge wamekuwa wakileta hoja binafsi, ni mara chache kama siyo hakuna kabisa, mbunge kuleta mswaada binafsi na ukapitishwa na kuwa sheria (ambayo mimi ningeona ndiyo ingekuwa wanatimaiza wajibu wao wa kutunga sheria. La kunisikitisha ni pale ambapo Bunge la mama Makinda linataka kuzuia wabunge kuleta hoja binafsi.

Hii ni sawa na kuwanyima haki yao ya kutungwa sheria. Kama serikali haijaona haja ya kuleta mswaada wa sheria, hata kama kuna haja na wabunge wameona basi jambo hilo halitungiwa sheria.

Tutafakari.
 
Mkuu kuna video clip ya Dr. Slaa akiongea na waandishi wa Habari akielezea utendaji wa bunge

Bunge la June linatakiwa lianze lini na kazi zake kuu ni zipi

Bunge la October na la February. Kujibu sehemu ya hoja yako anasema Bunge la February kazi yake kuu
ni kutunga sheria ama kurekebisha sheria na huwa linatakia kuanza Jumanne ya mwisho wa mwezi Feb. ila Makinda Et al
wamechakachua.
 
Hata Makinda haelewi kazi ya Bunge yeye anajua kazi yake ni kuwakandamiza wapinzani wasiongee na uchama zaidi!anasahau kilichowapeleka pale!akimaliza Bunge anaanza kuzurula anakusanya cha juu astaafu vizuri!atajuta maana kipindi chake kifupi amevuruma demokrasia ya Bunge na hana uwezo wa kuendesha Bunge!akili ndogo sana kuongoza akili nzito!
 
Eti kinaitwa chombo cha kutunga sheria wakati muda mwingi wanatamani wao ndio wawe serikalini... Bunge la tanzania halifanyi kazi mama. Yaani kutunga sheria.
 
Hata Makinda haelewi kazi ya Bunge yeye anajua kazi yake ni kuwakandamiza wapinzani wasiongee na uchama zaidi!anasahau kilichowapeleka pale!akimaliza Bunge anaanza kuzurula anakusanya cha juu astaafu vizuri!atajuta maana kipindi chake kifupi amevuruma demokrasia ya Bunge na hana uwezo wa kuendesha Bunge!akili ndogo sana kuongoza akili nzito!
Wabunge pia hawajui.... mimi nilifurahiwa na kuona hoja binafsi nikaanza kuamini kwamba sasa Bunge linafanya kazi mama... kwa mfano tume ya kurekebisha sheria ilistahili kuwa chini ya Bunge sio serikalini.
 
waelewa pale ni wabunge wa chadema tuu,wengine wanasubiri fadhila za kuchaguliwa na chama waendelee kuwa wabunge
 
Bado ninasikitika kusema kuwa Bunge letu lina mtizamo wa chama kimoja. Ndiyo maana kazi kubwa ya Bunge letu imebaki kupitia hoja za Serkali na kuzipitisha!

Ni kweli kazi kubwa ya Bunge ni kutunga sheria na tulitarajia kuona wabunge wakipeleka siyo hoja binafsi tu Bali hata miswada ya sheria binafsi katika maeneo wanayoona yana upungufu au yanahitaji sheria. Tunachokiona katika Bunge letu ni 'kuiomba' Serkali kuleta mswada!

Mwisho ningependa kuona rekodi za wabunge wetu na hasa jinsi wanavyopiga kura zitunzwe. Niliona Mh Spika alipoanza alijaribu kufanya hivi lakini sijui iliishia wapi? Amerudi kulekule kwa kuhoji kwa sauti. Ni vizuri tukafahamu misimamo ya wabunge wetu katika mambo yanayojadiliwa bungeni, lakini pia itatuonyesha utendaji wa kazi wa wateule wetu.
 
Bunge letu tukufu la jahmuri ya muungano wa tanzania,labadili mwenendo na kuoneka kama kijiwe kilichopo vichochoroni.
Watanzania wengi tunashangazwa na mambo mengi wanayoyafanya hawa wabunge tulowachagua kutotetea haki yetu.

Madhaifu mengi yamejitokeza yakiwemo yale ya kielimu,kiuchumi na n.k.
Miongozo inayotolewa ni kwa lengo la kujaribu kutetea maovu.tumechoka kuburuzwa.

Tanzania tunahitaji kubadilika,ifikapo mwaka 2015,tunataka changes na kuwa na wanasiasa wenye umakini wa kututea.
Hatuitaji wabunge na mawazili wababaishaji,wasiojua kuwajibika bali kula mali ya umma.
By now we need to gather and embarck our mind choosing quarified contestants and loos their capabilities with gained experiences.
 
Kila siku tunasikia na kuona mambo yasiyo ya kawaida bungeni,meza kuu ikiulizwa inasema ni upinzani kila kitu upinzani, mpaka imefikia kumuita mnajimu mkuu wa upinzani ungeni ndiyo kinara wa fujo bungeni. Mwaka jana miswada kingi tuu ilihairishwa kwa sababu ya uchache/utoro wa wabunge.

Tukasikia meza kuu ikilalamika wabunge wanaingia bungeni wakiwa wamelewa na wanatumia sigara kubwa mwaka huu tunasikia tena la utoro likilala mikiwa..je yote haya yanatokea kwa sababu ya CDM?

Maana kila linaalotokea tunaambiwa CDM ina shawishi ili kupata umaarufu au yanatokea kwa sababu ya mapungufu ya meza kuu? Unapo kuwa na Bunge lenye wa bunge wa vyama mbali mbali na wasome na nivijana inahijajika zaidi busara hekima na utashi zaidi kuliongoza kuliko jazba.

Bungeni ni sehemu ya uwakilishia wananchi na taifa na si chama tawala wala upinzani kwa yanayo endelea kama yasipo angaliwa mapema sidhani kama bunge la safari hii litaisha pasipo kubigana.
Mungu ibariki Tanzania na watuwake
















bungeni
 
Back
Top Bottom