Bunge letu linapoteza hadhi!

Bunge letu linapoteza hadhi!

Spika na naibu wake hawajui wajibu wao, Aibu ya kumuondoa Sita kwa hila. Hila haina fikra. Hili ni janga la taifa. Muhimili huu sasa unageuzwa kuwa chini ya serikali. Inauma sana, tuhakikishe Spika ajae hawajibiki katika chama cha siasa, tumeshajifunza.

... Mkuu umenena' pokea Likes..!
 
Bunge ndicho chombo kikuu cha jamhuri ya muungano ambacho kitakuwa na madaraka,kwa niaba ya wananchi,kuisimamia na kuishauri serikali ya jamhuri ya muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake..... hayo ni maneno ya katiba ya JMT siyo yangu.

Wabunge wote ni wawakilishi wa wananchi wapo pale kwa niaba yetu kwa sababu haiwezekani Watanzania wote kuingia bungeni ndio maana tumechagua wachache wetu kutoka miongoni mwetu kwenda bungeni kwa niaba yetu kutuwakilisha.

Kilichopo sasa ni serikali inajisimamia yenyewe na inajishauri yenyewe kibaya zaidi inalisimamia pia bunge,bunge limekuwa kama kifaranga cha kuku na serikali imekuwa mwewe,serikali imekuwa juu ya bunge linapanga hoja ya kujadili na pia linafuta hoja ambayo hawaipendi.

Wabunge wengi wa CCM wanajiona kama nao ni sehemu ya serikali niliwahi kumsikia mbunge mmoja wa CCM(ambaye si waziri wala mkuu wa mkoa) akisema na yeye ni kiongozi wa serikali.

Kwahiyo kwa sababu bunge hili chini ya spika Makinda linasimamiwa na linashauriwa na serikali na si la wananchi basi hakuna haja ya kuwa nalo kwa sababu kuwa nalo ni kujiongezea gharama tu.tuiache serikali ijishauri na ijisimamie yenyewe kuliko kuwa na bunge la serikali.
huu uzi walipswa wauone mkuu hapa umejenga hoja na imekamilika sasa tufanyeje waione hawa watu ???
 
Bunge linaonekana kuwa Bunge la vurugu nikwa sababu ya ukiritimba wa uongozi wa Bunge hasa pale Speaker's kutokuwa na ulinganifu, na kuwa na ubabe hasa kutaka wabunge wa upinzani wasionekane kama wana hoja za msingi lakini kimsingi tatizo lilopo ni jinsi ya uendeshaji wa taratibu za bunge!kwani hii yote ni mikakati ya serikali ambayo inatekelezwa na uongozi wa bunge! Na kinacholifanya sasa kila mtu alaumu Mh,Tundu Lissu anaufahamu wa sheria hivyo wanapopindisha hataki kuongopewa!Na lazima aonekane ni mwiba wa Maspeaker's Lakini kitendo cha Hamiss Kigwangala kusema CUF awanashida bungeni halina tja kwani CUF=CCMB sasa anategemea watasema nini??au Kulinganisha TLP na CDM nikama kulinganisha mtumbwi na Meli kubwa za Messina linea!!
 
Bunge linaonekana kuwa Bunge la vurugu nikwa sababu ya ukiritimba wa uongozi wa Bunge hasa pale Speaker's kutokuwa na ulinganifu, na kuwa na ubabe hasa kutaka wabunge wa upinzani wasionekane kama wana hoja za msingi lakini kimsingi tatizo lilopo ni jinsi ya uendeshaji wa taratibu za bunge!kwani hii yote ni mikakati ya serikali ambayo inatekelezwa na uongozi wa bunge! Na kinacholifanya sasa kila mtu alaumu Mh,Tundu Lissu anaufahamu wa sheria hivyo wanapopindisha hataki kuongopewa!Na lazima aonekane ni mwiba wa Maspeaker's Lakini kitendo cha Hamiss Kigwangala kusema CUF awanashida bungeni halina tja kwani CUF=CCMB sasa anategemea watasema nini??au Kulinganisha TLP na CDM nikama kulinganisha mtumbwi na Meli kubwa za Messina linea!!

CCM ilitengeneza mazingira haya siku nyingi pale walipotishia kumfukuza kazi samweli sitta pale alipokuwa speaker na hawa walioko sasa wasingependa yaliyomkuta sitta yawakute nao.
 
CCM ilitengeneza mazingira haya siku nyingi pale walipotishia kumfukuza kazi samweli sitta pale alipokuwa speaker na hawa walioko sasa wasingependa yaliyomkuta sitta yawakute nao.
Nikweli kabisa maana ndiyo maana walitengeneza mazingira mapema kwani walijua kambi ya upinzani imepanuka na CDM ni mwiba kwa serikali hivyo lazima watumie mbinu chafu!
 
Kwa ninavyoona bunge letu linavyoenda, naona siku si nyingi tutashuhudia yale yaliyo likumba bunge la Ukraine siku si nyingi sana zilizo pita.Hebu tudurusu kidogo hapa kisha tujifunze jambo.


 
Last edited by a moderator:
Wakati fulani bhandugu tufikirini kwanza kabla ya kushabikia mambo ya ajabu ajabu bungeni kwa sababu kuna wabunge wakisifiwa ndo wanaendelea na kuna siku itakuwa vurugu kubwa.Nilazma wabunge wawe na nidham ndani ya bunge letu.
Huko Katika bunge la Korea tarehe 22 July 2009 ilikuwa hivi;
 
Last edited by a moderator:
Hakuna Ubaya wa Mambo kama haya mahali ambapo hakuna HAKI. "SULUHU haiji ila kwa NCHA ya UPANGA". Bi Kiroboto na Ndugai hawataki suluhu. Dawa ndo hiyo. Kina mama wabunge wa upinzani ingieni bungeni na viatu vya visigino virefu na chanuo za chuma ili vitumike kama silaha. Kina Baba ingieni na mikanda yenye "buckles" kubwa za chuma. Hakuna tena cha kanuni hapa
 
unadhani tukifikia hatua ya kushushiana mangumi ndo tunaweza kuelewana na kutekeleza majukumu kwa usahihi zaidi kuliko kuzungumza kwa hoja na utulivu?
hoja na utulivu ulishafwata sana lakini haukuzingatiwa .
 
Haki bila kutendeka hapo mjengoni, bunge litavurugika. Spika inabidi awe fair kwa wabunge wa vyama vyote. Serikali isilivuruge bunge letu na kuliburuza!
 
Mara nyingi nimekuwa nikifuatilia taratibu mbalimbali (proceedings) na mijadala inayoendelea bungeni... ambapo kwa sasa kutokana na changamoto kubwa zinazoletwa na makamanda (wapinzani) naona sasa nchi yetu inaweza kufika mahala pazuri miaka hamsini ijayo... Swali ambalo mara nyingi najiuliza, uwepo wa bunge au kazi ya Bunge ni kutunga sheria na kuisimamia serikali katika shughuli zake (japo hili ni hadithi tu), lakini je Bunge letu la Tanzania linampa vipi ufahamu mwananchi wa kawaida juu ya linavyotenda kazi zake?? Mbona mara zote limekuwa likichanganywa lugha na pia kuzungumzia utaalamu zaidi badala ya sera na utekeklezaji wa jukumu lake?? mimi mwananchi wa huku Nyasamba ambae elimu yangu ni ya kawaida sana na ambae kiingereza kwangu ni lugha ya tatu, ninapataje habari za kibunge kwa ufasaha uliokusudiwa??

Kwanini hoja za kitaalamu (tukiachana na vifungu vya sheria) na lugha ya kiingereza visitumike kwenye kamati na idara husika, ila uwasilishwaji wake Bungeni uwe katika lugha ya kawaida sana ambayo mimi na jirani yangu hapa Nyasamba Shinyanga tunaweza kuelewa kiurahisi??

Mfano mzuri ni wasilisho la leo (kujibu hoja) kulikofanywa na Waziri wa fedha kutoa takwimu za kimahesabu za kitaalamu kuhusu deni la taifa tena anataja tarakimu kwa lugha ya kizungu na kwenye mfumo wa dola za kimarekani...

Je sisi wananchi wa kawaida hapo tunaelewa nini?? au hatujalengwa sisi?? au Waziri hajui lugha rahisi kwa ndugu zake wasio na elimu kubwa...

Naomba kuwasilisha!!

Mbumbumbu Intellegent...
Avatar ant nothing but identity!
 
hoja na utulivu ulishafwata sana lakini haukuzingatiwa .
sasa dada yangu; huoni zikiibuka vurugu hatimae wanaweza wakaumia wale ambao wanadhaniwa kwamba ndio wanaotetea haki?huoni itakuwa ni hasara juu ya hasara!
 
Kama BUNGE linashindwa kuisimamia SERIKALI ni la nini???HAKI HAIOMBWI,HAKI HUPIGANIWA.
 
Bunge la TZ linamilikiwa na CCM in nature,kwa hiyo hata utekelezaji wa shughuli za bunge unalenga kukidhi mahitaji ya wanachama wake ambao ni men of gold na sio wale wanaoishia kupewa kofia na chumvi ambao ni men of iron,so lugha inayotumika wanaielewa wamiliki wa bunge.
 
sasa dada yangu; huoni zikiibuka vurugu hatimae wanaweza wakaumia wale ambao wanadhaniwa kwamba ndio wanaotetea haki?huoni itakuwa ni hasara juu ya hasara!
ndo hivyo kwenye msafara wa mamba na kenge wapo...........bora nusu hasara kuliko hasara nzima.
 
magamba ndo mana hoja za msingi za wasio magamba zinazimwa kwa manufaa ya magamba.
 
Spika,Naibu Spika na Wenyeviti wa wabunge wanatakiwa kuwa fair na kutumia vyema sheria na kanuni za bunge kwa manufaa ya Taifa kama Taifa na siyo kwa manufaa ya vyama.Watuonee huruma watanzania kwani tunamatatizo mengi ya kuyafanyia kazi hili la haki za kibunge lisiwe na lenyewe tatizo la kuanza kulifikiria.
 
Bunge ni mali ya wanachi ki uhalisia lakini kwa Tanzania bunge ni mali ya akina mwigulu, nape, makinda,na ndugai
 
Back
Top Bottom