Bunge letu linapoteza hadhi!

Bunge letu linapoteza hadhi!

Siyo siri Bunge katika kikao kilichopita cha 10 lilkuwa Bunge lisilo na viwango wala standards za kuenzi demokrasia.

Tuache unazi wa vyama, pale Bungeni ni mahali pa hoja na si vinginevyo.
Hoja hujadiliwa na muafaka hupatikana kwa ajili ya utekelezaji.

Utungaji sheria, mijadala inayoletwa na wakilishi wa wananchi, kusimamia serikali na taasisi zake ndio misingi mikubwa ya kuwa na Bunge.
Kanuni na taratibu zipo pale kufanya mambo yaendeshwe kistaarabu tu.

Vurugu na kuonyeshana ubabe si dalili njema katika jamii hasa zinapotokea mahali kama Bungeni.
Tumeona kuwa kuna wale wenye damu changa kuliko wengine, hata Mwalimu aliwahi kusema wako left of centre, ni rahisi sana wao kuingia katika mhemko wa hasira, ngumi na kurushiana maneno mabaya.

Lakini yote tisa, kumi ni marefa walioapishwa kuendesha Bunge letu tukufu kwa haki na impartiality kushindwa kazi hiyo.

Kwa matokeo ya Bunge liliopita ni vema wakajifikiria jinsi walivyo udhalilisha mhimili huu muhimu kwa kukosa viwango si vya kimataifa tu, bali hata kitaifa.

Mama Makinda na Job Ndugai tunaomba mjipime wenyewe na kuchukua uamuzi mgumu kwa manufaa ya umma wa Kitanzania!
 
Shida yako huwa una rangi nyingi sana lile la kijani kibichi likiwa limekolea kwa zaidi ya 90% hali ambayo husababisha unafiki pasi na kujitambua au kutaka!
 
Katika hali isiyoyakawaida mpakasasa sipika wabunge na naibu wake wamejikuta wakiongoza bunge kwaititkadi ya chamachao..
 
Shida yako huwa una rangi nyingi sana lile la kijani kibichi likiwa limekolea kwa zaidi ya 90% hali ambayo husababisha unafiki pasi na kujitambua au kutaka!

Utawala bora ni sera ya CCM
 
Nyie mafisadi ndo mliowaweka hawa watu, inashangaza sana kusikia mkipaza sauti za kinafiki kuhusu hawa watu wenu. Labda tu nikusaidie kukumbusha kuwa soma id yangu hapo chini
 
kwa hakika ccm ilikuwa na nguvu kubwa sana kiasi kwamba ingechukua karne kuwaangusha.
Lakini mfumo wa serikari sasa utasaidia kuiua mapema. Anacho fanya spika na naibu wake na kuwapotosha wabunge wa ccm na serikari kiasi kwamba, wanajidhihirisha kuwa maadui wa wananchi na wapinga maendeleo.
Ukweli wa jambo hili uko hivi; ccm wangepinga chochote kinachopendekezwa na kambi ya upinzani, hivyo kupitia wingi wao watazuia hoja zote za upinzani kwa kupiga kura ya hapana hata kama hoja hizo zina maslahi kwao na jamii ya kitanzania. Upande mwingine, wabunge wa ccm wangetetea chochote kinacholetwa na serikari ya ccm, ili kuonyesha ushindi hata kama hoja hizo za serikari zinakosa tija na kulenga kuwakwamua watanzania toka maadui wanaokabiliana nao katika maisha yao ya kila siku.
Matokeo yatakuwa hivi baada ya muda mfupi jamii yote itaelimika na kutambua adui halisi wa maslahi na maendeleo yao ni nani.
Upingaji wa hoja zinazogusa maisha ya watanzania ndicho kigezo kitakachotumiwa na nguvu ya umma kukikataa chama cha mapepo.
Spika kupinga kila hoja ya wapinzani bila kuipima iwapo ina manufaa kwa maslahi ya taifa au la, itasaidia wananchi kuikataa serikari ya walanchi wasiojali hali za walala hoi kwa vile wao wanakula wanashiba, watoto wao wanasoma, wana taraja la kazi na wanatibiwa apollo na hawana shida ya maji majumbani mwao, wanatumia maji ya chupa.
Spika anatusaidia kuona ukweli.
 
Bunge la tisa linaloongozwa na Anne Makinda limekuwa la kipekee katika historia za mabunge ya nchi hii. Bunge hili linafanya kazi ya kuitetea serikali badala ya kuwatetea wananchi wanaowawakilisha ambao kiuhalisia wana matatizo mengi kama vile umaskini wa kipato,elimu duni,njaa,ukosefu wa huduma za afya,maji na mengine kadha wa kadha. Sasa katika hali kama hii nani atasimama na kuwa kipaza sauti cha wananchi wanyonge?
 
sasa unalalmika nini,huo ndiyo utawala bora wa ccm unaouona kwa makida na huyo job mdunguaji wenu
Ni watu wajinga wajinga tu wasiojua kuwa hata kuwepo kwa CDM ni kutokana na CCM kuyakubali mabadiliko ya kisiasa nchini.
Mabadiliko hayahodhiwi na chama chochote katika nchi hii.
 
Ni watu wajinga wajinga tu wasiojua kuwa hata kuwepo kwa CDM ni kutokana na CCM kuyakubali mabadiliko ya kisiasa nchi.
.


mkuu umeposti hoja nzuri sana, wewe ni ccm sote tunafaham lakini kwa hoja hii ukweli umeuweka wazi nami nakuunga mkono tulia kwenye hoja wanaokubeza watajitathimini.

Tatizo unapoteza muelekeo, watani zako wanakutoa nje ya hoja yako nawewe unabebwa na mihemko unatoka na kughafirika.

Kuwa mpole, mtulivu na absorb hizo challenge taratibu kwa hekima watarudi kwenye mstari, na hoja itajadiliwa vizuri.
 
Back
Top Bottom