Bunge letu linapoteza hadhi!

Bunge letu linapoteza hadhi!

Kwakweli aibu! wabunge wa Ccm Wanashindwa kutetea maslahi
ya watz, siasa za wakati huu hazina vyama ni maslahi kwanza ya wananchi kwanza
 
Bunge letu sasa lina laana

Bunge limeingia katika historia ya ovyo kabisa, mkutano mzima wa bunge wa wiki mbili unaisha bila kuwa na muswada wa sheria wala azimio huu ni udhaifu kwa serikali lakini pia tungewalaumu wabunge kwa kutoleta miswada binafsi ila wao wamejitahidi kuja na hoja binafsi ila ch kusikitisha viongozi wa ovyo wakiongozwa na ushabiki wamehujumu hoja binafsi za wabunge, huu ni ujuha wa hali ya juu.

Pamoja na ubwanyenye wa museveni na nguvu yake ndani ya NRM lakini anaogopa sana Bunge hadi anatishia Jeshi kuchukua Nchi, ni hatari watu waliokula kiapo cha kutenda haki kwenye siasa za vyama vingi kuinajisi haki hiyo na kutoishi viapo hivyo.
 
Wabunge wa ccm kwa ajili ya kuitetea serikali dhidi ya wale walio watuma. Wanaiwakilisha serikali bungeni. Isipokuwa mh. Deo Filikunjombe pekee.
 
haya mabo ya jumuiya za kimataifa kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine yamepitwa na wakati,ni wakati wa kuingilia ukandamizaji wa tanzania/ccm
 
  • Kama kila linalosemwa na Wabunge wa CCM ni jema na linapita wakati linalosemwa na Wabunge wa vyama vya upinzani linapingwa na kutupiliwa mbali,Bunge halina maana.


  • Kama Wabunge wa chama tawala wanaachwa kutumia lugha za kuudhi na wale wa upinzani wakitolewa nje ya Bunge na kutakiwa kuwasilisha maelezo,basi Bunge letu linakosa maana.


  • Kama ushahidi unaoletwa mbele ya Spika na Wabunge wanaotakiwa kuuwasilisha unafichwa na kunyamaziwa,Bunge letu linakosa mshiko.


  • Kama maazimio mbalimbali ya Bunge hayatekelezwi na yanapuuzwa,kuna maana gani ya kuwa na Bunge lenye nguvu ya kikatiba kuisimamia Serikali?


  • Ikiwa Wabunge wanakuwa mstari wa mbele kuongoza watu kupiga wenzao na kufanya vurugu(tukio la jana Dodoma),i wapi heshima ya Bunge?

Tujadili...

Usiongelee Bunge kama tatizo bali ongelea tatizo kuwa ni SPIKA na NAIBU wake kuwa ndio tatizo
 
kama spika na naibu spika wange kuwa wazalendo kusinge tokea vurugu bungeni,jamani mwacheni mtu awakilishe anacho taka kuwakilisha ila hoja hujibiwa kwa hoja hata kama hojo hiyo ita rudidiwa mara 100
 
Kwa kifupi kinachoendelea sasa bungeni ni mnyukano kati ya watetea haki kwa upande mmoja na watetea uovu kwa upande mwingine, kati ya watetea maslahi ya wananchi na watetea maslahi ya wateule wachache ndani ya sisiemu (na serikali), kati ya wawakilishi wa wananchi na wawakilishi wa chama tawala (na serikali yake).

Ni mnyukano kati ya wabunge wachache wanaojua shida za wananchi wanaowawakilisha bungeni na wengi ambao wameziba masikio (kwa kujua au kutokujua) na kugeuka kuwa watetezi wa serikali, kati ya 'wachumia tumbo' hata kama wanajiita first class economist na wachumi wa kweli, kati ya wale wanaona rasilimali za nchi na namna zinavyoweza kutumika kama vitega uchumi na 'vibaka uchumi'.

Ni mnyukano kati ya utandawazi na 'mtandaowizi', kati ya uhuru wa kuzungumza na 'uhuni' wa kuzungumza, kati ya wasomi wachache na watu waliowahi kwenda kupasha joto madawati shuleni. Ni mnyukano kati ya nuru na giza, kati ya chumvi na kitu kingine chenye ladha chungu.

Naam, yote haya yapaswa yatokee ili watanzania wajue ya kuwa kile chama walichokiamini (au kuaminishwa) kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi sasa ni chama cha mafisadi, wahamisha twiga na wauza pembe za ndovu. Chama ambacho tuliambiwa kuwa kinaamini kwamba binadamu wote ni sawa sasa kimebadilika na kuwa 'binadamu wote si sawa' maana kuna wanasisiemu na wapinzani, kuna wanamtwara na wanabagamoyo. Chama kilichosema rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala kupokea rushwa, sasa kinasema wagombea wake wote wanatoa rushwa kwenye chaguzi. Ile ahadi ya kuwa nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote, sasa elimu inatumika kwa 'faida' ya chama kwanza.

Hii ni sauti inayopazwa kwa mwito na mshindo mkuu kwa baba, mama, kaka, dada na wadogo zangu kule Namiyonga (Newala), Lumuma (Mpwapwa), Kinalilya (Iramba), Makere (Kasulu), Lubafu (Bukoba), Kabanga (Nzega) au Nkwarungo (Hai) na vijijini kote katika nchi hii, msidanganyike tena kwa pombe, tshirt, kanga au chumvi na kuuza haki zenu za msingi kwa makuwadi wa mafisadi.

Nionapo yote haya, najua kwa hakika mwisho wa mambo yote umekaribia. Naam, hata huo mwisho hauko mbali sana maana naoina Tz mpya yenye tumaini jipya. Naona anguko kuu la sisiemu, naye ajidhaniye amesimama aangalie asije akaanguka. Asomaye na afahamu!!!!!

We nkwarungo hatudanganyiki sisi hivi wewe unawajua wamachame?gud idea bt hapo tu ndio umekosea
 
Ni kulewa tu madaraka na pia ni dharau za viongozi wetu kwa kutuona sisi watanzania hatuna akili na hatuwezi kupambanua mema na mabaya.Na pili usaliti ambao watanzania kama watanzania tunaufanya kwa taifa letu nikupokea rushwa na pesa au zawadi ndogondogo ili kuishabikia CCM na viongozi wake ili ionekane kwamba tunapendezwa na mambo yake.
 
Iko pia shida kwa wenyeviti na wale kina mama wanaoingia kwa viti maalumu wakapige makofi na kuzomea. Nashindwa kuelewa hawa jamaa wanafanya nini hapo dodoma wakati hakuna dawa hosipitali, shule hazina madawati, Spika na naibu wake wanajifanya wababe na kuruhusu wabunge wakanywe bia kwa gharama zetu. Aibu sana hui.
Usiongelee Bunge kama tatizo bali ongelea tatizo kuwa ni SPIKA na NAIBU wake kuwa ndio tatizo[/SIZE][/QUOTE]
 
Bunge ndicho chombo kikuu cha jamhuri ya muungano ambacho kitakuwa na madaraka,kwa niaba ya wananchi,kuisimamia na kuishauri serikali ya jamhuri ya muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake..... hayo ni maneno ya katiba ya JMT siyo yangu.

Wabunge wote ni wawakilishi wa wananchi wapo pale kwa niaba yetu kwa sababu haiwezekani Watanzania wote kuingia bungeni ndio maana tumechagua wachache wetu kutoka miongoni mwetu kwenda bungeni kwa niaba yetu kutuwakilisha.

Kilichopo sasa ni serikali inajisimamia yenyewe na inajishauri yenyewe kibaya zaidi inalisimamia pia bunge,bunge limekuwa kama kifaranga cha kuku na serikali imekuwa mwewe,serikali imekuwa juu ya bunge linapanga hoja ya kujadili na pia linafuta hoja ambayo hawaipendi.

Wabunge wengi wa CCM wanajiona kama nao ni sehemu ya serikali niliwahi kumsikia mbunge mmoja wa CCM(ambaye si waziri wala mkuu wa mkoa) akisema na yeye ni kiongozi wa serikali.

Kwahiyo kwa sababu bunge hili chini ya spika Makinda linasimamiwa na linashauriwa na serikali na si la wananchi basi hakuna haja ya kuwa nalo kwa sababu kuwa nalo ni kujiongezea gharama tu.tuiache serikali ijishauri na ijisimamie yenyewe kuliko kuwa na bunge la serikali.
 
Spika na naibu wake hawajui wajibu wao, Aibu ya kumuondoa Sita kwa hila. Hila haina fikra. Hili ni janga la taifa. Muhimili huu sasa unageuzwa kuwa chini ya serikali. Inauma sana, tuhakikishe Spika ajae hawajibiki katika chama cha siasa, tumeshajifunza.
 
... nikutoka na matumizi mbaya ya kanuni zinazoendesha bunge.
Inaonekana kuna udikteta kutoka kwa spika, kwa jinsi wanavyoendesha bunge.
Labda tuanzishe mchakato wa maoni ya wananchi ili kupata kanuni mpya za kuendesha bunge.
 

Source: m.m. mwanakijiji wa youtube



Source: ITV TANZANIA ya youtube
 
Last edited by a moderator:
sidhani kama ni hekima na busara bungi likiendeshwa kisiasa, mi nadhani bunge ni sehemu muafaka wa kuwasilisha utendaji kazi wa wabunge wetu na maendeleo ya nchi yetu. mhishimiwa spika hebu weka siasa pembeni na mjadili vitu vya msingi bungeni. Mungu bariki Tanzania
 
Serikali imekuwa juu ya bunge, na makinda amekuwa pale kama mwakilishi wa serikali na si mkuu wa mhimili unaojitegemea! Masikini Samwel sitta, sijui aliwafanya nini maccm!
 
Maana harisi na wajibu wa bunge letu umepindishwa, na hili linatokana na wa wakilishi wengi ndani ya bunge kua wabinafsi na kujiangalia wao zaidi kuliko wale wanao wa wakilisha bungeni. Na mmbunge anajiona kama serikali yawezekana ana mkono unao iendesha serikali ndani kwa kutumia pesa yake na hata yeye pia huenda alitumia pesa yake kumuweka Waziri flani au hata Rais flani na hili linasabishwa na bunge kua na ma CCM mengi kama kungekua na idadi sawa au ma ccm yamezidiwa tusinge ona upumbavu unaondelea leo hii mle bungeni. Wananchi tubadilike 2015 uwe mwaka wa mabadiliko kwa kuanzia bungeni.
 
Back
Top Bottom