Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya JMT inaweka wazi kuwa Bunge litakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri serikali ya JMT na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake.
Hii ni dhana ya Separation of Powers which is a must in the running of a sovereign state.
Hali hiyo haipo sasa na ni tofauti kabisa.
Bunge limekuwa kataasisi kadogo kaserikali kwa ajili ya kupitisha maamuzi na mipango ya serikali, hata kama ni haramu au feki.
Katika hali ya kufedhehesha Serikali sasa ndio inalisimamia Bunge !
Waziri sasa ana uwezo wa kuamua kama hoja binafsi iwasilishwe au la, japo ni kinyume na kanuni.
Na kazi kubwa ya spika imekuwa ni kukandamiza upinzani huku akinyenyekea mabosi wake ambao ni mawaziri ie serikali.
Wabunge wa CCM ambao ni wengi zaidi wanaitumia fursa ya uwakilishi wa wananchi kuiwakilisha serikali na kuilinda badala ya kuwakilisha wananchi, ie hawajui wajibu wao na hudhani kuwa wao ni viongozi wa serikali.
Hivyo basi, kwa sasa hatuna chombo cha kuisimamia serikali !