Bunge la Marekani lapitisha Muswada wa Sheria ya kuifungia TikTok

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Bunge la Marekani limepitisha Muswada wa Sheria itakayoruhusu kufungiwa kwa TikTok, mtandao wenye Watumiaji Wamarekani takriban Milioni 170, kama haitatengana umiliki wake na kampuni ya ByteDance yenye asili ya China.

Wakitoa maoni ya kupitisha Muswada huo, Wabunge wamesema TikTok inahatarisha Usalama wa Nchi kwasababu China inaweza kuitumia ByteDance kuingilia Uchaguzi Mkuu wa Marekani na Taarifa Binafsi za Watumiaji.

Utekelezaji wa hatua hiyo utasubiri Kura za Bunge la Seneti ambalo kama litapitisha maamuzi hayo, TikTok itakuwa na miezi 5 tu kujitenga na ByteDance, vinginevyo itaondolewa rasmi kwenye soko la Marekani.

==={=

The House passed legislation that could ban TikTok in the US unless the app parts ways with its Chinese parent company, ByteDance. It's a major challenge to one of the world’s most popular social media platforms, used by 170 million Americans.

Lawmakers supportive of the bill have argued TikTok poses a national security threat because the Chinese government could use its intelligence laws against ByteDance, forcing it to hand over the data of US app users. It’s not yet clear what the fate of the measure will be in the Senate.

If enacted, the bill would give TikTok about five months to separate from ByteDance, or app stores in the US would be banned from hosting it on their platforms.

In a statement, TikTok blasted the House vote and urged the Senate to "consider the facts." China’s foreign ministry responded angrily ahead of the vote, calling it an "act of bullying."
 
Watanzania walifungiwa masaa 72 wakasema kulikuwa hakuna Free speech.

Kwamba mambo ya Wananchi yaamliwe na Wananchi

Nani amewaamulia Wananchi wa Marekani kama sio wanasiasa. Yaani watu karibia milioni mia mbili! Waamuliwe na watu wachache wenye madaraka.

Nadhani wanafanya haya mpaka pale Uchaguzi utakapoisha.? Republicans hatari sana, wanatumia njia zote kuzima sauti za wapinzani wao

Kwa mtazamo mwingine, huu ni Ujambazi. Kwamba ukiwa sio MMAREKANI na ukawa na kampuni au App inayoshindana na matajiri wa Kimarekani, unadondokewa kama mwewe(Eagle hapa) na genge la Serikali. Halafu tukisema tuna vita ya Kiuchumi watu wanatoa mapovu na kushupaza shingo, or Demokrasia, oh Free market. My foot. Kuna Free marke na uamuzi huo?

Aha, hoja yao ni Usalama wa raia na Taifa.

Yale masaa 72 nayo yalikuwa ni kwa Usalama wa Nchi, raia -Taifa..... Itoshe, makampuni au platforms zilizofungiwa(internet) zilikuwa ni za Wageni kama ilivyo tick toku ni ya wageni kwa Wamarekani.

Liwe fundisho kwenu makasuku.
 
Hizi Ban anazoziendekeza USA zitamtokea puani, watu watachoka ban zisizo na msingi kila siku
 
Sio kutojiamini, wapo makini na nchi yao. Hawa jamaa huwa wanaona mbali sana, kuna namna tu hiyo kampuni ina vitu fulani, hawabahatishi hawa.

Kupuuzia puuzia mambo ni kitu hawafanyi hawa.
Hahahaaa,ni wivu tu!Huawei nao walikuwa na shida gani?
 
China inatumia fursa ya kupigwa BAN ngoja uone kama atakaa kimya lazima ije na kitu kipya kwa ajili ya kubust mambo yao
 
chuki tu ya kiuchumi hawa marekani hawajawahi kusupport mafanikio ya yanayohusiana na china zaidi ya kuwaletea vikwazo kwa kila jambo.
 
Hahahaaa,ni wivu tu!Huawei nao walikuwa na shida gani?
Wamarekani waweke wivu kwenye app ya China, kuwa serious basi chief.

Kampuni zinapishana, unaweza kuta mfano Naivas ina shida zake lakini hiyo haimaanishi Uchumi na wao watakuwa na matatizo kama ya Naivas, unanielewa?
 
Unajua hizo app unazozichukulia poa zinaingiza ukwasi kiasi gani?USA ana jambo lake na rival wake China,ni wivu tu wa kibiashara!
 
chuki tu ya kiuchumi hawa marekani hawajawahi kusupport mafanikio ya yanayohusiana na china zaidi ya kuwaletea vikwazo kwa kila jambo.
Kabisa,USA mpaka analazimisha mataifa mengine kutofanya biashara na China!EU nao kama mazombie tu kwa US!
The Netherlands has announced new rules restricting exports of certain semiconductor manufacturing equipment. It follows pressure from the US to curb the sale of computer chip technology to China. The Dutch government did not cite this as a reason though, saying it had taken the step on national security grounds
 
Bunge la Marekani limepitisha Muswada wa Sheria itakayoruhusu kufungiwa kwa TikTok, mtandao wenye Watumiaji Wamarekani takriban Milioni 170, kama haitatengana umiliki wake na kampuni ya ByteDance yenye asili ya China.
Screenshot_20240313_205514_Samsung Internet.jpg
 
Unajua hizo app unazozichukulia poa zinaingiza ukwasi kiasi gani?USA ana jambo lake na rival wake China,ni wivu tu wa kibiashara!
Mkuu, achana nq mambo ya ukwasi hata kama zinaleta kiasi gani. Kikubwa ngoja tuone kama itapita, maana wenzetu wapo free mikono yao haipo in chains.

Kama halina maana bali ni hizo interests wewe umeziita "wivu wa kibiashara wa Marekani kwenda China" basi muswada sina shaka watautupilia mbali, ila sense tu inasema hayaji kwa bahati mbaya haya mambo.
 
USA anaumizwa kichwa na China kiasi kwamba mpaka analazimisha matakwa yake hadi kwa washirika wake dhidi ya China!

The Netherlands has announced new rules restricting exports of certain semiconductor manufacturing equipment. It follows pressure from the US to curb the sale of computer chip technology to China. The Dutch government did not cite this as a reason though, saying it had taken the step on national security
 
Back
Top Bottom