MAKEI inapatikana maeneo gani hapo Mafinga Mkuu wa Kikosi? Nataka nikafanye utafiti kidogo.
Kwa hiyo hivi vipimo havitauzwa kwa kificho tena?View attachment 1261625
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tayari limeipitisha rasmi sheria inayompa mamlaka, mtu kujipima mwenyewe Virusi vya Ukimwi kwa kutumia sampuli zinazotoka kwenye kinywa, pamoja na sheria inayoruhusu kijana kuanzia miaka 15, kupima Ukimwi bila ridhaa ya mzazi.
Sheria hiyo imepitishwa leo Novemba 12, 2019, na kwamba sheria hiyo itasaidia watu kujitambua hali zao mapema, hususani wanaume na kundi la vijana, ambalo kwa sasa ndilo linaloongoza kuwa na waathirika wengi wa ugonjwa huo.
Akizungumza bungeni Dodoma, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile, amesema kuwa tayari Wizara imekwishajipanga juu ya upatikanaji wa vipimo hivyo na tayari imeshaanza kufanya majaribio ya mifumo hiyo ikiwa ni pamoja na kuangalia mapokea kutoka kwa wananchi.
"Vipimo hivi havitakuwa vinatumia damu, vitakuwa vinatumia sampuli ya kinywa na hii watu watapima hata kabla ya kujamiiana na watakapobaini wamepata changamoto hizo wanakuja katika vituo vya kutoa huduma za afya ili kujiridhisha,vijana wengi wameanza kuathirika na kujamiiana wakiwa na umri mdogo, sasa tunatoa fursa kwa vijana kuanzia miaka 15 kupima Ukimwi bila ridhaa ya mzazi wake" amesema Waziri Dkt Ndugulile.
Sijui lengo haswa ya maamuzi haya ni nini, kuna changamoto nyingi sana kwenye utekelezaji wa upimaji na hatimae ufuatiliaji wa matumizi ya dawa, ni miezi zaidi ya miwili sasa upimaji umesimama kwa ukosefu wa Unigold, dawa za kuzuia maambukizi ya Tb ( IPT ) upatikanaji wake ni tatizo, huduma za upimaji ( Liver and Renal function tests, viral load, CD4 na vingine havifanyiki kama miongozo Inavyotaka) kwa nini wizara isitatue kwanza changamoto zilizopo kabla ya kuanzisha hili jipya?
kwanini nipime ukimwiWaungwana, salama!
Kwa mujibu wa hii sheria mpya, unaweza kununua na kuhifadhi vipimio vya ‘HIV’ ndani kwako kwa ajili ya matumizi binafsi na ya kifamilia, wapo wanaopongeza hatua hiyo na wengine kusimama kinyume.
Pamoja na ukweli kwamba suala la maambukizi ya virusi ‘vinavyoweza’ kusababisha UKIMWI (VVU) ni tatizo kubwa, elimu ya kujikinga na kujiepusha na maambukizi mapya bado haipewi uzito unaostahili, hivyo kupelekea kasi ya maambukizi kuendelea kupanda kila kukicha.
Elimu inayotolewa bado haijawafikia walio wengi ukiacha ile kidogo ya awali ambayo wengi tumeipata tungali wadogo sana shule ya msingi, kwa wakati huo tuliamini na kuogopa kweli kweli lakini kumbe ni kwa vile tu tulikuwa hatujaonja asali. Waathirika wakubwa ni ‘watu wazima’ ambao kwa asilimia kubwa hawana tena muda wa kuendelea kupatiwa elimu sahihi hivyo hujikuta katika hatari zaidi ya kuambukizwa na kusambaza.
Kumekuwa na changamoto katika upimaji wa afya kwenye vituo husika, huku ikiripotiwa kuwa wanaume sio wengi wanaojitokeza kwa hiari huku wanawake wakilazimika kufanyiwa vipimo hasa kipindi wanapokuwa wajawazito na hata hao wanaolazimika kupima (ME/KE) inapotokea upenyo wengi wao hukimbia ‘majibu’ au huwa hawapo tayari kujua ukweli.
Sasa kwa sheria hii inaruhusu upatikanaji ‘holela’ wa vifaa vya kupimia VIRUSI, mtu kwa hiari yake ataweza kujipima na kujipa majibu akiwa amejifungia au akiwa na watu ambao mwenyewe karidhia kuwa nao, lakini je elimu inatosha juu ya kupokea matokeo ya vipimo?
Imeshawahi kunitokea mimi enzi za ujana wangu, japo ilikuwa kinyume na sheria ila nilifanikiwa kuwa na vipimio ndani na mara kadhaa nilikuwa naibuka mshindi kwa kutengeneza matokeo CHANYA kabla ya mechi, ila siku moja ikatokea mambo yakasoma ‘kekundu’ kwa huyu ‘mshirika’ ambaye umemshawishi na kumpima. Je, utakuwa katika nafasi gani kumfanya akubaliane?
Tunahitaji elimu, elimu, elimu.
UKIMWI upo, japo umepunguza sifa hivyo umetulia kama vile haupo ila takwimu ziko sahihi.
Pima. Jitambue. Ishi.
kwanini nipime ukimwi
akishajua iweje sasa wakati dawa hamnaIli ujue afya yako.