Halafu "oooh, Tanzania ni nchi yenye uhuru wa habari".
Nyoooo.
Nani ataondoa hoja "zisizo za msingi"? Kwa muongozo gani?
Kama kuna wabunge wenye "hoja zisizo za msingi" kwa nini bunfe lisiache wananchi waone wabunge wao wanavyotoa "hoja zisizo za msingi" live ili kuwaelewa zaidi na kuweza kuamua vizuri zaidi kama wataendelea kuwachagua au watawamwaga uchaguzi ujao?
Kwa nini bunge linaingilia uhuru wa vyombo vya habari?
Kwa nini wanahabari wasilishitaki bunge mahakamani?
Kwa nini wabunge wasitunge sheria ya "freedom of information" itakayohakikisha bunge haliwezi kupitisha maazimio ya kidikteta kama haya?