Budapest Memorandum: Ulaghai wa kihistoria Warusi waliowafanyia Marekani, Uingereza na Ukraine

Kama hujui bado omba uelimishwe lakini Aftican resources are being plundered.

Mfano rahisi fuatilia saga ya Ufaransa na makoloni yake west Africa.
Tanzania hapa una kisingizio gani wakati mna kila kitu. Visingizio hivi vya kijinga vitafanya Afrika ibakie kuwa kichekesho cha dunia milele.
 
Vita siku zote ni uchumi, haya mataifa makubwa huangalia kwanza uchumi! Kama faida hakuna basi hakuna vita!

Ukrainian conflict: The first lithium war?​

  • Russia’s annexing of Ukraine’s massive lithium reserves has ‘benefitted Kremlin’
  • But Putin has succeeded in stopping EU’s plan for Ukrainian lithium

What is the real reason for the war in Ukraine??

The Russian leader ordered the invasion of Ukraine to strike a blow in the battle for control of the means of delivering the global energy transition.

The logic of the argument is this: prior to the Russian invasion, it had been estimated that Ukraine had around 500,000 tonnes of high-quality lithium – a key component of the batteries used in electric vehicles and energy storage systems – and consequently the country was set to become a “key player in the global transition to green technology”.

H
World Bank ilikuwa ikiikopesha Russia mabilioni ya $dola mpaka mwaka 2014. Na kuna wakati ndio ilikuwa mchangiaji mkubwa zaidi katika sekta yake ya utumishi wa umma.

USAID imeipa Russia mamilioni ya dola za misaada mpaka mwaka 2012, imeisaidia kukarabati katiba yake kuongeza uhuru kwa raia, imeisaidia kurekebisha sheria zake kodi za ardhi.
Hizo ni story za kijiweni pia mkuu.
 
Mwaka 1991 wakati USSR inavunjika mataifa kadhaa yaliyokuwa yanaunda umoja huo yalikuwa yanamiliki silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu. Ukraine lilikuwa ni taifa mojawapo lililokuwa likimiliki mzigo mkubwa wa silaha za nyuklia na nyinginezo nzito, ilikuwa taifa la tatu duniani kwa umiliki wa silaha za nyuklia baada ya Urusi na Marekani.

Kuvunjika kwa USSR ilikuwa ni furaha kubwa kwa Marekani na Uingereza na West yote kwa ujumla lakini pia kulikuja na hofu kubwa mno kwao kwamba kusambaratika huko kwa USSR kungeleta sintofahamu kubwa ya masuala ya kiusalama Ulaya kwa sababu mataifa mengi yaliyotoka USSR yalikuwa na silaha nyingi nzito zikiwemo nyuklia. Hapo ndipo Rais wa Marekani wa kipindi hicho George H.W Bush akabuni makubaliano ambayo aliwashirikisha Urusi, Uingereza na Ukraine kutatua sintofahamu hiyo. Baadaye makubaliano hayo yaliendelezwa kwa upana na ukubwa zaidi na Bill Clinton na yakaitwa Budapest Memorundum kwa sababu yalisainiwa rasmi katika mji wa Hungary wa Budapest mwaka 1994.

Makubaliano hayo ni marefu sana lakini katika kina chake hasa ilikuwa ni Ukraine kupeleka Urusi au kuharibu silaha zake zote za nyuklia pamoja na makombora yake masafa marefu kwa ahadi ya kwamba Urusi, Marekani na Uingereza hawataingilia uhuru nchi hiyo na wataheshimu mipaka ya Ukraine kama taifa huru. Pia Urusi kukazia ikaahidi msaada na mkopo wa gesi na mafuta wa zaidi ya $billion 2.5. Ukraine walitaka mkataba kamili kutoka kwa Marekani na Uingereza unao guarantee usalama wa mipaka yake lakini hadi mwisho wa makubaliano waliishia kupata ahadi tu kutoka kwa Wamarekani kwamba watapata ulinzi kamili kutoka kwao endapo taifa lolote litawaingilia au kuwavamia baada ya kukabidhi au kuharibu sila zao. Kulitokea mzozo, ubishani na upinzani mkali sana ndani ya Ukraine hadi kusababisha waziri wa ulinzi kujiuzulu lakini mwisho wa siku Ukraine ikaingia makubaliono hayo na kuyatekeleza yote mpaka kufikia mwaka 2008.

Matokeo yake baada ya muda mfupi baada ya Ukraine kutekeleza makubaliano yote Rais wa Urusi Putin akaanza kutoa kauli za ajabu ajabu kuhusu Ukraine kama "Urusi na Ukraine ni watu wamoja na mwisho wa siku lazima watarudi kuwa watu moja", "Ukraine kwanza ni taifa lisilio halisi la kutengenezwa tu lisilo na historia yake" n.k. Urusi ikaanza kuingilia siasa za ndani ya Ukraine kwa nguvu kubwa kipindi cha Rais Viktor Yanukovych wa Ukraine kuanzia 2010 baada ya kuona Ukraine ilikuwa inaelekea mueleko na kuzidisha ukaribu zaidi na West. Ikaanza kuzalisha vikundi vya uasi na kujitenga mipakani mwa Ukraine, ikavamia Ukraine mwaka 2014 na kuendelea kuivamia nchi nzima mwaka 2022. Urusi ikawa imevunja makubaliano yote ya Budapest memorandum na pia Ukraine ikiwa haina sila zake wala guarantee yoyote ya usalama kutoka Marekani au Uingereza. Wamarekani wengi hawataki kulikumbushia hili suala kwa sababu linaanika kiasi gani walivyo na deni kubwa kwa Ukraine.
Nini kilisababisha Cuban missile crisis? Ni kwanini ilitaka kusababisha WWIII? Ukishapaelewa hapo bila bias hautopata shida kuyaelewa matendo ya Urusi kwa ukraine (Hii sitaki hata kuiandika kwa kuanza na caps).

Urusi baadae walikubali kutoa majeshi yao East Germany kwa makubaliano gani?

Marekani ndo kubwa la mashetani, Marekani ndo kubwa la malaghai hata usipate shida.

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Nakwambia hawa ni watu wa vijiweni tu bwana hawawezi kujua hayo kwani Gorbachev alisema wao waliongelea mambo ya upunguzaji wa silaha za hatari tu na wala hawakuongelea mambo ya Nato.
Ingia YouTube andika "RFK Jr on ukraine war" utaongeza kitu. Havutii kumsikiliza lakini utapata madini.

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Yaani wewe ni mrusi zaid ya Gorbachev kweli kiashi cha kumwita puppet wa west? Usilete utani hapa
Je Boris Yelstin ambaye ndiye aliyesini ile Budapest Memorandum na ndiye aliyemchagua Putin kumrithi kuwa Rais wa Urusi naye alikuwa "Puppet wa west?"

Wewe kuwa na anti-west attitude kama ya Putin haina maana kuwa basi Putin yuko sahii
Gorbachev alikua kibaraka wa west ndio maana hata alipofariki hakupewa mazishi ya kitaifa hata kwa kuzingatia ndio alikua rais wa mwisho wa USSR.

Warusi hawawezi kumsamehe kwa hilo kamwe.

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Moja ya kosa Putin amefanya ni kuivamia Ukraine.

1. Naheshimu wasiwasi wa Usalama wa Russia hasa upande wa Ukraine Ila alitakiwa amalize hofu yake kwenye mazungmzo ya Amani na kuwepo na mkataba wa kuhakikisha Neutrality ya Ukraine.

Matokeo ya uvamivi yamekuwa tofauti sana, Finland na Sweden zimejiunga na NATO na Ukraine inazidi kuwa na nguvu na wakati huo huo Russia anaendelea kutumia rasilimali nyingi vitani, watakuja kushtuka Ukraine Ana Silaha za Nyuklia na military industry kubwa sana
 
Vita siku zote ni uchumi, haya mataifa makubwa huangalia kwanza uchumi! Kama faida hakuna basi hakuna vita!

Ukrainian conflict: The first lithium war?​

  • Russia’s annexing of Ukraine’s massive lithium reserves has ‘benefitted Kremlin’
  • But Putin has succeeded in stopping EU’s plan for Ukrainian lithium

What is the real reason for the war in Ukraine??

The Russian leader ordered the invasion of Ukraine to strike a blow in the battle for control of the means of delivering the global energy transition.

The logic of the argument is this: prior to the Russian invasion, it had been estimated that Ukraine had around 500,000 tonnes of high-quality lithium – a key component of the batteries used in electric vehicles and energy storage systems – and consequently the country was set to become a “key player in the global transition to green technology”.

Vipi kuhusu uvamizi wa Crimea 2014?
 
Moja ya kosa Putin amefanya ni kuivamia Ukraine.

1. Naheshimu wasiwasi wa Usalama wa Russia hasa upande wa Ukraine Ila alitakiwa amalize hofu yake kwenye mazungmzo ya Amani na kuwepo na mkataba wa kuhakikisha Neutrality ya Ukraine.

Matokeo ya uvamivi yamekuwa tofauti sana, Finland na Sweden zimejiunga na NATO na Ukraine inazidi kuwa na nguvu na wakati huo huo Russia anaendelea kutumia rasilimali nyingi vitani, watakuja kushtuka Ukraine Ana Silaha za Nyuklia na military industry kubwa sana
Marekani pamoja na kumchukia sana Urusi hawezi kamwe kuwawezesha ukraine kuwa na nyuklia kwasababu sio mjinga!

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Nini kilisababisha Cuban missile crisis? Ni kwanini ilitaka kusababisha WWIII? Ukishapaelewa hapo bila bias hautopata shida kuyaelewa matendo ya Urusi kwa ukraine (Hii sitaki hata kuiandika kwa kuanza na caps).

Urusi baadae walikubali kutoa majeshi yao East Germany kwa makubaliano gani?
Lini Marekani au NATO walitaka kuweka makombora yao Ukraine? Kuna makombora ya Marekani huko Finland, Uturuki, Romania, Bulgaria, na Estonia?

Urusi walikubali kuondoka East Germany ambayo haikuwa eneo lao kwa kuanzia kwa makubaliano gani?
 
Kuvamia nchi jirani siyo option. NATO ilikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuitawanya Urusi katika kipindi cha kuanzia mwaka `1993 hadi 2004 kwani ilikuwa na control kubwa sana juu yake lakini haikufanya hivyo, badala yake ikajikita katika kuisaidia Urusi ili isimame imare tena, halafu baada ya hapo eti ndipo uadui uanza kama Putbi hakuwa na usongo wa ndani siku hizo zote?

Kitendo cha kuivamia Ukraine hakijasaidia lolote kwenye maslahi ya nchi yake bali ndipo ameikaribisha NATO zaidi mlangoni mwake huku vijana ambao niyo nguvu ya kesho ya taifa wakiwa wanakimbia nchi. Sasa hivi Putin anajivunia wale wazee wa zamani waliokulia ndani ya Soviet Union na watu wa vijijini wanasikiliza habari kwenye TV ya Taifa tu. siyo generation mpya inayoishi kwenye majiji kama Moscow na St Pettersberg.
Lakini bwana Kichuguu,unadhani maeneo kama Finland na Poland kwa kusaidiwa na washirika wake hawawezi kuipiga urusi wakiamua?
 
Back
Top Bottom