Budapest Memorandum: Ulaghai wa kihistoria Warusi waliowafanyia Marekani, Uingereza na Ukraine

Sababu za uvamizi kutoka mdomoni kwa Putin
“Its goal is to protect people who have been subjected to bullying and genocide by the Kyiv regime for eight years. And for this we will strive for the demilitarisation and denazification of Ukraine, as well as bringing to justice those who committed numerous, bloody crimes against civilians, including citizens of the Russian Federation.”
Unaruka ruka tu, umeomba katiba umepewa, unatoka nje ya mada kwa ujanja wa kitoto kabisa.
 
Sababu kubwa ya Putin kufanya anachofanya ni Ukraine kutaka kujiunga NATO. Kama ujuavyo nchi za NATO ni adui wa Russia kuanzia nyanja ya kiuchumi mpaka kijeshi. Na policy yao hao jamaa ni kuweka kambi zao za kijeshi kila kona ya dunia hasa kwa nchi wanazokuwa nazo marafiki au walioko kwenye umoja huo.

Lengo likiwa ni kuendeleza ubabe na kuchuma rasilimali za nchi husika. Yani US na allies wake wanaamini kuweka bases kila pembe ya dunia hata ikitokea all out war wanaweza kumpiga mtu yeyote mahali popote kutokea mahali popote duniani.

Angalia issue ya China na Taiwan. US ndio anasababisha chokochoko.

Sasa kumuingiza Ukraine NATO maana yake US anakuwa na access rahisi na anaweza kuweka kambi za kijeshi karibu kabisa na Urusi ambae ni hasimu wake. Hapo ni sawa na kumshika mrusi kalio. Hakuna nchi inayojitambua inaweza kukubali huu ushenzi, ndio maana hata China huu ujinga wa Taiwan hataki kuusikia.

So kwa maslahi mapana ya nchi yake Putin hakuwa na option zaidi ya kumstopisha Ukraine.
Finland na lithuan wamejiunga NATO na majiran wakaribu wa Urussi kwanini hajawashambulia
 
acha utoto,

umeomba kujua ikiwa katiba ya ukraine inatambua hilo la wao kujiunga nato, nimekupa!

so far inaonekana uwezo wako wa kuelewa mambo ni mdogo,
Haya, chukua point tusipotezeane muda kwenye ignoratio elenchi.
Katiba iliyofanyiwa hayo marekebisho mwaka 2019 inahusiana vipi na uvamizi na uporaji wa Crimea mwaka 2014?
 
Hawana mpaka direct na Russia. Russia amekuwa ally mkubwa wa Bulgaria na Romani miaka nenda rudi na hawana uhasama wa kihivyo.

Hivyo hao jamaa hawana uhasama na Russia kama allies wengine wa NATO.

Na Russia ana presence kubwa sana black sea hata kwenye territories za hizo nchi. Kiujumla black sea ipo controlled na Russia.
Kwani Ukraine ilikuwa ina uhasama gani na Russia ?
Kati ya Russia na Ukraine nani alikuwa na uhasama na mwenzake?
 
We jamaa acha uongo russia haijawahi kukopeshwa mkopo na marekani eti uchumi wa russia umejengwa na marekani yaani adui yako kabisa umsadie kuimarisha uchumi wake leta chanzo cha hiyo habari inayoonyesha kwamba marekani imetoa dollar million kadhaa kuisaidia russia.

Ki historia Ukraine imebadilisha viongozi wengi kuanzia 1991 tena walikuwa wanabadilisha kwa kupokezana term hii akishika Pro-west term inayokuja inashika Pro-Russia hiyo imeenda hivyo mpka mwaka 2014 sasa unavyosema wakifanya uchaguzi, ndo russia huzivamia huo nao ni uongo.

Uvamizi uliofanywa Georgia ilikuwa ni baada ya kutaka kujiunga na NATO, Kama sikosea ni 2008 rejea NATO summit ya mwaka huo waliotaka kujiunga ilikuwa yeye na Ukraine ila baadhi ya member wa NATO walikataa ikiwemo German na Ufaransa ambao nao waliona wakizikubalia itazua vita ila walichowaahidi ni kwamba kwa baadae inaweza kuwafikiria na mwaka huo huo baada ya hiyo summit ndo georgia ilivamiwa na russia.
World Bank ilikuwa ikiikopesha Russia mabilioni ya $dola mpaka mwaka 2014. Na kuna wakati ndio ilikuwa mchangiaji mkubwa zaidi katika sekta yake ya utumishi wa umma.

USAID imeipa Russia mamilioni ya dola za misaada mpaka mwaka 2012, imeisaidia kukarabati katiba yake kuongeza uhuru kwa raia, imeisaidia kurekebisha sheria zake kodi za ardhi.
 
Ki historia Ukraine imebadilisha viongozi wengi kuanzia 1991 tena walikuwa wanabadilisha kwa kupokezana term hii akishika Pro-west term inayokuja inashika Pro-Russia hiyo imeenda hivyo mpka mwaka 2014 sasa unavyosema wakifanya uchaguzi, ndo russia huzivamia huo nao ni uongo.
Huo sio ukweli, Ukraine haijawahi kuwa na utaratibu wa viongozi kubadilishana madaraka kati ya Pro-west na Pro-Russia. Viongozi wote wa nyuma waliotangulia kabla ya Viktor Yanukovych hawakuwa na upande wowote, walikuwa neutral. Viktor Yanukovych aliyechaguliwa mwaka 2010 ndiye aliyeanzisha vurumai za Pro-Russia na Pro-Russia West kutokana na kuwa fisadi aliyepitiliza na maslahi binafsi makubwa ya biashara huko Russia.
 
Nimekuwa nawashangaa sana mafuasi wa Putin kulaumu Uingereza na Marekani kuisaidia Ukraine kiulinzi ilihali ilikuwa ni wajibu wa nchi zote tatu pamoja na Urusi kulinda Ukraine chini ya Makubaliano hayo. Kwa vile Putin aliamua kwa makusudi kuvunja makubaliano hayo haina maana kuwa Uingereza na USA nazo zitayavunja.

Putin ni kichaa wa ajabu alieyekuja kuvuruga amani ya ya dunia kwa nia ya kurudisha ule mfarakano wa zamani wa cold war ambao haukuwa mzuri kwa maisha ya binadamu wa kawaida. Sasa sijui yeye anategema kupata nini kutokana na mfarakano huo.
Putin ni jasusi mzalendo mno kwa nchi yake alijua bila kuwasogeza NATO mbali na moscow hao jamaa ipo siku watamgeuka vibaya , walikubaliana vizuri nchi zilizotoka ussr zisijiunge na NATO lakini nato akazinganisha kama nchi nane hivi tena kwa suprise ndo mbabe akaona akae chonjo
 
Uvamizi uliofanywa Georgia ilikuwa ni baada ya kutaka kujiunga na NATO, Kama sikosea ni 2008 rejea NATO summit ya mwaka huo waliotaka kujiunga ilikuwa yeye na Ukraine ila baadhi ya member wa NATO walikataa ikiwemo German na Ufaransa ambao nao waliona wakizikubalia itazua vita ila walichowaahidi ni kwamba kwa baadae inaweza kuwafikiria na mwaka huo huo baada ya hiyo summit ndo georgia ilivamiwa na russia.
Sababu waliyotoa Russia ya kuivamia Georgia mwaka 2008 ni madai ya kwamba serikali ya Georgia ilikuwa ikifanya mauaji ya kimbari"genocide" dhidi ya South Ossetia ambao walikuwa waasi wanaotaka kujitenga kama kule Donbas.
 
Sababu kubwa ya Putin kufanya anachofanya ni Ukraine kutaka kujiunga NATO. Kama ujuavyo nchi za NATO ni adui wa Russia kuanzia nyanja ya kiuchumi mpaka kijeshi. Na policy yao hao jamaa ni kuweka kambi zao za kijeshi kila kona ya dunia hasa kwa nchi wanazokuwa nazo marafiki au walioko kwenye umoja huo.

Lengo likiwa ni kuendeleza ubabe na kuchuma rasilimali za nchi husika. Yani US na allies wake wanaamini kuweka bases kila pembe ya dunia hata ikitokea all out war wanaweza kumpiga mtu yeyote mahali popote kutokea mahali popote duniani.

Angalia issue ya China na Taiwan. US ndio anasababisha chokochoko.

Sasa kumuingiza Ukraine NATO maana yake US anakuwa na access rahisi na anaweza kuweka kambi za kijeshi karibu kabisa na Urusi ambae ni hasimu wake. Hapo ni sawa na kumshika mrusi kalio. Hakuna nchi inayojitambua inaweza kukubali huu ushenzi, ndio maana hata China huu ujinga wa Taiwan hataki kuusikia.

So kwa maslahi mapana ya nchi yake Putin hakuwa na option zaidi ya kumstopisha Ukraine.
upo sahihi sana
 
Umenza vem article yako lakini umeingiza propaganda plae ulipoanza 2008 Putin aligeuka. Je ulifuatilia mahojioni ya Putin na Mwandishi Culson Tucker? Hebu fuatilia. Na putin aikua anasema kama kasema uongo wakanushe.

Lakini pia hukuweka kiini cha mgogoro huu wa sasa. Vita vya wenyewe 2014 to 2022 Urusi ilihusikaje? NATO je? Eu je na hao wote walikua Sehemu ya Budapest Memorandum?
Putin na Tucker Carlson walikuwa wanapiga story za Russia na Ukraine jinsi walikuwa wamoja enzi hizo za Ivan the Terrible! Ni kihoja na upuuzi mtupu.
Baada ya vita vya pili vya dunia mataifa yote walikubaliana mipaka ya nchi iliyokuwa ikisimama wakati huo ndio itaendelea kuheshimiwa daima, walikubaliana watu wasirudishe historia tena nyuma ya zama hizo za giza kudai maeneo fulani ya nchi nyingine au nchi nyingine kuwa zilikuwa ni sehemu yake.
 
Finland na lithuan wamejiunga NATO na majiran wakaribu wa Urussi kwanini hajawashambulia
Urusi haiwezi kuishambulia Finland kwa sababu tangu uvamizi wa USSR kwa Finland mwaka 1940 uliozua Winter War Finland imekuwa ikijiandaa kikamilifu kivita na Urusi wakati wowote.
 
Kwamba urusi hana uwezo wa kuivamia hiyo nchi dhaifu Zaid ya Ukraine?acha kujiaibisha nafuu unyamaze tu
Urusi haiwezi kuishambulia Finland kwa sababu tangu uvamizi wa USSR kwa Finland mwaka 1940 uliozua Winter War Finland imekuwa ikijiandaa kikamilifu kivita na Urusi wakati wowote.
Ba
 
Putin na Tucker Carlson walikuwa wanapiga story za Russia na Ukraine jinsi walikuwa wamoja enzi hizo za Ivan the Terrible! Ni kihoja na upuuzi mtupu.
Baada ya vita vya pili vya dunia mataifa yote walikubaliana mipaka ya nchi iliyokuwa ikisimama wakati huo ndio itaendelea kuheshimiwa daima, walikubaliana watu wasirudishe historia tena nyuma ya zama hizo za giza kudai maeneo fulani ya nchi nyingine au nchi nyingine kuwa zilikuwa ni sehemu yake.
Hivi wewe unaishi wapi. Unafaham chochote kuhusu Palestina na Israel, unafahamu chochote kuhusu Gholan Height, unahamu chochote kuhu mgogoro wa Tanzania na Malawi na msimamo wa Uingereza....

Yapo mengi ya kujifunza na kuelewa nini kinapelekea migogoro hiyo na kisha linganisha na ulichosema kuhusu makubaliano baadà ya WWII. Na misimamo ya mabeberu.

Congo haina amani sio bahati mbaya
 
Palestina haijawahi kuwa taifa na pia mgogoro wa Malawi na Tanzania ni mwepesi sana na wapiga porojo tu ndio huwa wanaukuza, sheria ya kimataifa kuhusu mpaka wa ziwa au mto ni kwamba mpaka unakuwa katikati ya ziwa au mto.
 
Back
Top Bottom