Bro ulokole mwingi mwisho unaharibu sasa

Bro ulokole mwingi mwisho unaharibu sasa

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,708
Reaction score
35,716
[emoji184]Umeshindwa mpaka sasa kuoa kisa upo kiroho saaaana eti tunamngoja Bwana

[emoji184]Umejifanya upo kiroho mpaka unakera, maana umeitoa kiroho mwingi alafu kutongoza binti huendi kutongoza ili uoe umekaa tuu kusema Bwana atanikumbuka kama Ibrahimu alivyo kumbukwa akapewa mtoto.

[emoji184] Broo muda wako wa kuoa umefika huna cha kusubiri, nenda kamtongoze yule binti ili upate mke.

[emoji184] Hivi huoni kwamba kila siku mabinti wanajiremba ili wewe ukiwaona uwatongoze( uwachumbie) ujipatie mke, sasa umebaki umeuchuna tuu kuongea na binti huongei naye anabaki kufanya maombi tuuu eti Bwana atakutokea kama malaika, kwanini usimwambie unaogopa ukiroho wako utapotea? Hakuna utakacho poteza broo

[emoji184]Hivi huoni kama utu uzima umekuangukia tayari na uzee unakungoja stand muondoke, broo changamkia dili bado sula yako inalipa, mabinti wanakusubiri wewe tuu

[emoji184]Broo unawaweka wakati mgumu sana mabinti yaani hawaelewi kwamba wao ni warembo kweli au sura zao hazilipi? Yaani hawakuelewi kabisa maana wamefanya kila wanalo weza ili ushituke ila wanaona umeuchuna tuu.

[emoji184] Broo hivi huoni unavyo salimiwa kiheshima?
Huoni wanavyo kupokea Biblia kanisani na kukukaribisha kwenye kiti wakisema karibu Mtumishi?

[emoji184]Wamejitahidi wasiwe watoro hapo kanisani na wanapiga kila kazi ilimradi Mzee uone japo maono alafu utongoze, Mzee umeuchuna tuu, hushituki wala husisimki

[emoji184]Umekaa hutaki kutongoza ukijua kwamba ni dhambi daaaah yaani umekuwa kirohooooo zaidi ya Malaika Gabliel?[emoji4][emoji4]

[emoji184] Mzee hii time isipite wanakungoja CHUKUA mmoja sema naye atakukubali tuu
Nenda kwa Pastor wako mwambie kuwa umepatia mrembo wala hatakuuliza kama malaika kakuletea taarifa za huyo mrembo au vipi,
Wala hutaulizwa bali utamsikia Pastor anakwambia....."Oooh hallelujah Bwana amekutendea"

Shituka acha kuwafanya mabinti kila siku wanafunga na kuomba huku wakilia kwamba Mungu awatendee muujiza na kumbe muujiza wenyewe ndiye wewe hapo alafu umeenda tuu.....Jiongeze

Nafikiri Ipo Clear kabisa
FB_IMG_1578324467798.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom