Brg Gen Mwakanjuki afariki dunia

Pole kwa familia,jamaa na marafiki.Ni habari ya kusikitisha.Pumzika kwa amani brg Gen Adamu Mwakanjuki..RIP
 
Kama wanaitana vile hawa "Men in Uniforms'. Utadhani wanajiondokea baada ya kuona uozo umezidi mno nchini na hakuna mwelekeo wala dira ya kulivusha taifa hili kutoka katika limbi la ufisadi, jambo ambalo halikuwapo enzi za Mwalimu. Pumzika kwa amani Mkuu.
 
RIP Brg Gen Adam Mwakanjuki, hata mie nimewahi kuonana na mtu huyu alikuwa mtu wa watu haswaa!!
Hakuwahi kuwa mnafiki!
Poleni wafiwa....poleni wazenji, poleni wa TZ!
 
Waziri wa zamani katkia SMZ Brg Gen Mstaafu amefariki dunia mchana wa leo ktk hosp ya jesh Lugalo!!
Nilikuwa hapo punde pata habari hizi, sijui alikuwa anasumbuliwa nanini mwanasiasa huyu mkongwe!

Mungu awape faraja familia yake, Agness Mwakanjuki pole sana kwa kufiwa na baba mpenzi wangu. nakutakia faraja kipindi chote hiki na wanafunzi wote wa Ashira girls(1994-1997) wako pamoja na wewe my dear.
 

Alikuwa mkristu Muangilikan...............

Na asili yake ni Tukuyu Mwakaleli siyo Kyela, anaundugu na Prof Mwandosya kiaina.
 
RIP Brg Gen Adam Mwakanjuki, hata mie nimewahi kuonana na mtu huyu alikuwa mtu wa watu haswaa!!
Hakuwahi kuwa mnafiki!
Poleni wafiwa....poleni wazenji, poleni wa TZ!
mwanachama wa ccm yeyote yule lazima aanze kuwa mnafiki kwanza.La sivyo huyo ataundiwa zengwe.Mimi simwamwini mwanachama wa ccm yeyote hadi cdm iingie madarakini.
 
R.I.P umemaliza kazi sehemu iliyobaki ni yetu kumalizia na hata sisi tutawaachia wengine
 
Poleni sana ndugu jamaa na marafiki wote wa marehemu, and especially so kwa ndugu yangu na rafiki yangu Willy Karia wa raha pamoja na mkewe Mama shangwe; binti wa marehemu. tunawaombea subira katika wakati huu mgumu sana.
rest in peace General
 
Alikuwa makini sana Nyerere alimtegemea kwa vitu vingi sana ili kuiendesha na kupata habari za znz.Mungu akuweke mahali pema.

Mkuu kuwa makini na kauli zako.. Sio kijiwe cha kahawa hapa.. :blabla:
RIP Brigedier General Mwakanjuki..
 
R.I.P, Br. Gen. Mwakanjuki

Mbona jina kama wanyakyusa vile? Kama atazikwa Mbeya ccm isijisumbue ku-Kanumbanize msiba wa mpendwa wetu Mwakanjuki itaambulia patupu huku. R. I. P, Mwakanjuki. Ukaghone syepwa ubapenie bosa kubusyuka
 
..R.I.P Adam Mwakanjuki.

NB:

..marehemu ana mwanae ambaye ni mwanachama wa muda mrefu wa JF.

..nampa pole sana kwa kuondokewa na Baba yake mzazi.

Mkuu unaweza kutufahamisha ID ya mwanaJF mwenzetu huyu ili tuweze kumfahamu?

btw, ninawapa pole familia, ndugu jamaa na marafiki wa Marehemu "Malafyale" Brg. Gen. Adam Mwakanjuki.
 
mwanachama wa ccm yeyote yule lazima aanze kuwa mnafiki kwanza.La sivyo huyo ataundiwa zengwe.Mimi simwamwini mwanachama wa ccm yeyote hadi cdm iingie madarakini.

Kamanda una misimamo!! Wale wa zamani walikuwa na nafuu mkuu hawakuwa wote wanafiki!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…