Brexit imegonga Mwamba, kiini macho cha Demokrasia!

Mkuu
Uingereza walishajitoa siku ile walipo trigger article 50.
Hivyo baada ya miaka 2 baada ya ku trigger article 50 uanachama wao ndani ya EU unakoma automatically. Hayo majadiliano ni jinsi tu ya ku deal na common interests kama vile wananchi wa EU walioko UK itakuwa je na kinyume chake vilevile. Na kwa mfano watavyotozana ushuru ktk soko la pamoja la EU. Hivyo wajadiliane ama wasijadiliane baada ya miaka miwili UK anakuwa nje ya EU kwa style ya hard exit.

Brexit begins: The UK now has two years to untangle itself from the European Union
Brexit begins: The UK now has two years to untangle itself from the European Union
Hivi umesoma hili bandiko uliloleta au ?
Yaani umetuletea maoni kama ya Jingalao ndio unayafanya kama reference...halafu ninyi ndio mnatutisha kuwa siasa za UK ni maji marefu.
 
Mtoa mada yupo sahihi Waziri Mkuu Theresa May aliitisha uchaguzi wa haraka ili apate mandate kubwa katika kujitoa EU. Lakini baada ya uchaguzi na chama cha conservative kupoteza wingi wa wabunge itabidii waziri mkuu aunde serikali ya mseto. Kunauwezekano mkubwa huyu mama asiendelee kuwa waziri mkuu. Itabidi serikali ya UK wa review katika masuala ya kujitoa EU
Mkuu kuna vitu viwili tulivyojadili

1. PM May alliitisha uchaguzi ili apate mandate ya kutekeleza mipango yake ikiwemo Brexit

2. Mleta mada anasema PM aliitisha uchaguzi kwasababu Brexit imegonga mwamba.!!!! Ney

Mleta mada haukujua article 50 ya Lisbon Treaty wala hakujua March 29 UK ilisha trigger article 50
Alichosema, Brexit imekwama kwasababu ya uchaguzi! si kweli kabisa.
Alitaka ku justify hoja yake ya kiini macho cha demokrasia akidhani ni siasa za Lumumba

Kwa taarifa leo taehe 11 PM May ameongea na Merkel akimweleza utayari wa kuendelea na negotiations
Hapa hana maana kuanza mchakato wa kujitoa bali ni kuendelea na mchakato ulioanza na article 50 ya Lisbon treaty

Kujiondoa kwa UK si mara ya kwanza. Lakini pia UK ni uchumi mkubwa na ilikuwa ni gate ya EU na financial hub
Haiwezekani kuamka asubuhi na kusema leo basi! Wenzetu wanafanya mambo kitaalam si ki Lumumba
 
Usijifanye una uelewa mpana. Kura ya Brexit ilipigwa kwa ujinga wa Cameron na km ingekuwa ni nchi km US au Israel angekuwa shot toka anaanza kuwaza juu ya kuitisha kura.Mataifa yameundwa kwa akili kubwa za wachache.

Mambo ya msingi ya nchi yanaamuliwa na wachache ambao akili zao zimedhihirika kuwa ni kubwa sana sio kwa kura ambazo hata chizi anapiga.
Mkuu , kulikuwa na mjadala wa UK na ushiriki wake ndani ya EU
Kwanza, Waingereza walikataa euro ili wabaki na pound sterling yao. Hilo wakakubaliwa na EU

Pili, kuna wimbi la wahamiaji kutoka nchi za Ulaya mashariki waliofurika UK na kuleta tatizo la ajira

1. wingi waoulifanya kazi kuwa ngumu kupatikana na pia kipato kutoongezeka kwa kanuni ya 'supply and demand'
2. wahamiaji walipewa fursa kama wakaazi wa UK na kupelekea mzigo katika maeneo kama healthcare system
3. UK ilikuwa inabeba mzigo kutokana na uchumi wake kwa formula ya kuchangia huduma za Brussels
4. Waingereza 'asilia' hawakupendezwa na sheria kutungwa Brussels na kutishia umuhimu wa Buckingham Palace

Manung'uniko yalikuwa makubwa kiasi cha PM Godon Brown kuomba EU wajadili masilahi ya UK ndani ya EU (Special)
Majadiliano yalianza lakini baadhi ya nchi wanachama waligoma kuona UK inapewa kipaumbele sana
Ilifika mahali mataifa kama Ujerumani na France nao wakata kuwa na 'special' considerations

Hilo likatishia uwepo wa EU na mapendekezo mengi ya Godon yakagonga mwamba
Kwavile ilikuwa issue katika jamii, David Cameron akaichukua na kuiweka kama agenda ya Ilani yake

Alitumia agenda iliyokuwa na mambo makubwa matatu akisema anataka ku address manung'uniko ya watu wa UK
1. Kuhakikisha Scotland inafanya referendum ili kumaliza manung'iko ya Wascotch
Hilo alifanikiwa ingawa lilikuwa na matatizo kwani kura ilikuwa karibu sana. Kama unakumbuka ali kampeni kubaki UK

2. Ilikuwa kuwapa washirika wa UK fursa ya kuamua mustakabali wa Engalnd, Wales na Ireland
Ukiondoa Scotland wengine hawana nguvu za kujitawala nao wakadai wapewe mamlaka fulani
Hili alikuwa anaendelea nalo kwani lilikuwa complicated kama unavyoona Tanganyika na ZNZ, sasa wao ni wanne

3. Ilikuwa kura ya maoni ya UK ndani ya EU. Cameron alifahamu wazi kuwa EU ni mwiba, lakini alishinda uchaguzi kama agenda yake na asingeweza kuendelea kutawala kama asingesimamia hilo

Kwa mwelekeo wa haraka wengi walitaka UK ibaki EU kutokana na fursa. Walichosahau ni kuwa vijijini kuna watu waliokereka sana na uwepo wa EU kwasababu tullizoeleza hapo juu.

Nigel Farage kiongozi wa UKIP aliendesha kampeni ya kujitoa EU akichochea uzalendo zaidi. Chama chake ni cha aina ya 'white supremacists' ndiyo maana wanaelewana sana na Trump kwa mitazamo iwe ya wazi au siri

Kosa walilofanya wengi na hasa vijana ni kuchukulia for granted kuwa UK itabaki EU wakijua wasiotaka ni wachache
Kwa bahati mbaya wachache walijitokeza kupiga kwa 100 na wengi walijitokeza wakiwa chini ya hapo

Matokeo yalishangaza wengi ndiyo maana baada ya hapo kulikuwa na reaction ya kutaka uchaguzi tena
Hilo lilikuwa kama shtuko kwa wale waliodhani UK haiwezi kutoka na pengine hawakushiriki kupiga kura

Kwa mwendo wa siasa maji marefu za UK, jambo hufuatwa 'to the letter' . Jitihada za kutumia house of common kulipinga suala la kujitoa EU lilishindikana kwasababu mbili kubwa

House of common inafanya kazi kwa maoni ya wapiga kura 'constituents'. Kwa hili la EU, referendum ndiyo 'constituents' na ni unlikely house of common ingekwenda kinyume

Sababu ya pili ni kuwa maoni ya kujitoa au kutojitoa hayakuwa na chama. Yaligawa vyama kiasi kwamba liliachwa kuwa suala la kila Rais bila kujali itikadi za kisiasa 'non partisan'. Kwa mantiki hiyo hakukuwepo na organization ambayo ingepinga UK kisheria kwani vyama vya siasa havikuwa na ufungamano

Kwahiyo unaposema ni kosa la Cameron, lazima pia uangalie tatizo lilianza wapi na Cameron aliingiaje na kwanini
Kwavile alitekeleza ilani ya uchaguzi, gharama zilizompata ndiyo matokeo ya sera alizohubiri, si kosa hata kidogo
 
Tatizo watu hapa hawaelewi chanzo cha Brexit ni nini. Swala la Theresa May apate majority of seat or not Brexit IPO palepale Brussels's wanaeasubiri hawa watu waje negotiations zianze. Theresa May abacho kimempata ni baada ya upepo kubadilika watu wapo more concerned na homeland security baada ya kutokea hizi terrorist attacks Sikh za karibuni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom