Brexit imegonga Mwamba, kiini macho cha Demokrasia!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Wananchi wa Uingereza hawataki kuwa Wanachama wa Umoja wa Ulaya na walipiga kura ya maoni ya kujitoa, sasa kwa hali ya kawaida na kidemokrasia ilipaswa kura yao iheshimiwe na nchi ya Uingereza kujiondoa mara moja!

Lkn kinyume chake kimetokea maelite walikuwa hawataki Uingereza iondoke EU na sasa wamefanikiwa, Waziri Mkuu wa nchi hiyo ameitisha Uchaguzi ambapo alijua kbs angeshindwa na sasa anaunda Serikali na Chama ambacho hakitaki Uingereza ijitioe EU, ina maana sasa haiwezekani tena, na mara nyingine Wananchi wamedanganywa na maelite kwamba wanaishi kwenye Demokrasia na kwamba wao ndiyo wanaamua jinsi wanavyotaka kuishi kumbe ni danganya Toto na kiini macho!

Sasa najiuliza ile kura ya maoni ilikuwa ya kazi gani kama walijua hawawezi kutekeleza matokeo yake?

1497009835888071.jpg
 
"Barbarosa, post: 21539330, member: 284899"]Wananchi wa Uingereza hawataki kuwa Wanachama wa Umoja wa Ulaya na walipiga kura ya maoni ya kujitoa, sasa kwa hali ya kawaida na kidemokrasia ilipaswa kura yao iheshimiwe na nchi ya Uingereza kujiondoa mara moja!
Nenda kasome kitu kinaitwa article 50 of Lisbon treaty. Ukikosa rejea nzuri unaweza kupitia hapo chini huenda ukaokota kitu kuliko hali yako ya sasa

Duru-Ulaya: Kura ya maoni 'brexit'

Lkn kinyume chake kimetokea maelite walikuwa hawataki Uingereza iondoke EU na sasa wamefanikiwa, Waziri Mkuu wa nchi hiyo ameitisha Uchaguzi ambapo alijua kbs angeshindwa
Hujui kwanini aliitisha uchaguzi akiwa na majority na alitaka kupata nini
Kaa kimya kabisa

na sasa anaunda Serikali na Chama ambacho hakitaki Uingereza ijitioe EU, ina maana sasa haiwezekani tena, na mara nyingine Wananchi wamedanganywa na maelite kwamba wanaishi kwenye Demokrasia na kwamba wao ndiyo wanaamua jinsi wanavyotaka kuishi kumbe ni danganya Toto na kiini macho!Sasa najiuliza ile kura ya maoni ilikuwa ya kazi gani kama walijua hawawezi kutekeleza matokeo yake?
Sentensi ya mwisho ni nzuri, ungesema unauliza ili upate shule
Hayo mengine ni uzushi mtupu, hujuia Brexit ilikuwa non partisan

Tafadhali mambo yaliyokuzidi kimo yaache, usijaze mtandao. Kaa kimya katika hili na futa bandiko
Ipo siku utalisoma nakubaini si kuwa ulikuwa hujui au mjinga huenda kuna tatizo linalohitaji msaada zaidi

Yaweza kuwa umefuatilia habari kwa lugha usioielewa au inaweza kuwa ulihadithiwa hukusubiri hadithi ikaisha au asubhi hii umeamka na njozi za BREXIT ukaamua kutusimulia

Futa bandiko lako, utaondoa mashaka kwa wenye shaka juu yako. Please

Ahsante
[
 
H
Nenda kasome kitu kinaitwa article 50 of Lisbon treaty

Hujui kwanini aliitisha uchaguzi akiwa na majority na alitaka kupata nini
Kaa kimya kabisa

Sentensi ya mwisho ni nzuri, ungesema unauliza ili upate shule
Hayo mengine ni uzushi mtupu, hujuia Brexit ilikuwa non partisan

Tafadhali mambo yaliyokuzidi kimo yaache, usijaze mtandao. Kaa kimya katika hili na futa bandiko
Ipo siku utalisoma nakubaini si kuwa ulikuwa hujui au mjinga huenda kuna tatizo linalohitaji msaada zaidi

Ahsante
[

Hakuna Brexit, utaleta articles zote unazotaka lkn mwisho wa siku Uingereza haiondoki EU, kitakachotokea ni kusogeza mbele na kuarisha mazungumzo kwa muda usiojulikana, kwa mfano tarehe 19/6 ilipaswa mazungumzo ya Brexit yaanze lkn sasa haitawezekana kwa sababu Malkia ataongea hiyo siku na pilika pilika za kuunda Serikali mpya zitaanza, hivyo hiyo tarehe imesogezwa mbele na watafanya hivyo kwa miaka 5-10 ijayo!

Kwa nini waliitisha kura ya maoni kama walijua ni ngumu kutekeleza? Kura ya maoni ni hatua ya mwisho na kidemokrasia maana yake baada ya matokeo hakuna mjadala tena isipokuwa kutekeleza tu!
 
Ndiyo maana nakuambia kaa kimya. Kama hujui article 50 unajadili nini kuhusu Brexit
Kama hujui PM aliitisha uchaguzi kwasababu gani unajadili nini kuhusu brexit?

Please hili si la Lumumba, hizi ni siasa maji marefu sana, kwa uelewa wako unajitwisha zigo bila sababu

Tujadili bei ya maembe imeshuka, mananasi ya kiwangwa na kisamvu cha Morogoro, brexit unaweza kupata brain injury hasa ukizingatia nafasi ndogo iliyopo ku accomodate mambo mazito kama haya
 
Barbarosa ndugu, umefuatilia vizuri issue za uchaguzi wa UK na Brexit kwa ujumla?!

Kwa uchache sana, MP wa UK alichanga karata zake vibaya!! Alikuwa na uhakika wa kupata viti vingi zaidi tofauti na madai yako kwamba aliitisha uchaguzi huku akifahamu angeshindwa!!

Na suala la Brexit lipo pale pale!!! Kura ya kutoka ilishapita na kilichobaki ni negotiations tu za hapa na pale!! Ni kama wewe uwe umempa mkeo talaka lakini kinachobaki suala zima la maslahi ya kile mlichonacho!!!
 
Kwa Hili nakubaliana na wewe . Inaonesha hakuna dhamira ya dhati ya kujiondoa EU . Kwa ufupi Cameroon alibugi alipobip Na wananchi wakampigia na sasa mama ana haha maana washaona watapoteza sana kwa kujitoa EU. Wanatamani kughushi matokeo lakini not possible. WAMELIAMSHA DUDE WENYEWE
 
Ndiyo maana nakuambia kaa kimya. Kama hujui article 50 unajadili nini kuhusu Brexit
Kama hujui PM aliitisha uchaguzi kwasababu gani unajadili nini kuhusu brexit?

Please hili si la Lumumba, hizi ni siasa maji marefu sana, kwa uelewa wako unajitwisha zigo bila sababu

Tujadili bei ya maembe imeshuka, mananasi ya kiwangwa na kisamvu cha Morogoro, brexit unaweza kupata brain injury hasa ukizingatia nafasi ndogo iliyopo ku accomodate mambo mazito kama haya

Najua sababu kwa nini aliitisha Uchaguzi isitoshe sijakuita wala kukulazimisha uchangie hivyo acha kunipangia cha kuandika!
Na sababu huyo Waziri Mkuu ni sehemu ya establishment ambao hawataki Brexit hivyo aliitisha Uchaguzi huku akijua matokeo yake ili kusabotage Brexit, nani anakubali kuitisha Uchaguzi ili hali opinion zinamuonyesha yuko chini? Huyo mama anasabotage brexit na hkn kingine, na ninauhakika miaka 5-10 ijayo hakuna Brexit watakuwa bado wanavutana!
 
Mkuu punguza dharau...elimu haina mwisho..mueleweshe tu ataelewa pamoja na wana JF wengine ambao hawaelewi kinachoendelea...kujua siasa za UK sio sifa ya uongozi Tanzania kama ambavyo sio sifa ya uongozi kwa Theresa May kujua siasa za Afrika au Tanzania.
 
Mkuu siyo dharau ndiyo maana nimemsifia kwa sentensi ya mwisho aliyouliza. Kilichokera ni kama anaeleza kitu anachojua na si kuuliza kitu asichojua

Hebu soma kichwa cha habari na habari nzima. Nikamshauri akatafute article 50 imsaidie.
Jibu lake halikuonyesha kama anataka kuelewa. Mkuu kuuliza ni jambo jema, kuzungumza kama anajua ni jambo jingine. Nisaidie kujua anataka kujua nini kinaendelea brexit au anatueleza nini kinaendelea?
 
Najua sababu kwa nini aliitisha Uchaguzi isitoshe sijakuita wala kukulazimisha uchangie hivyo acha kunipangia cha kuandika!
Na sababu huyo Waziri Mkuu ni sehemu ya establishment ambao hawataki Brexit hivyo aliitisha Uchaguzi huku akijua matokeo yake ili kusabotage Brexit, nani anakubali kuitisha Uchaguzi ili hali opinion zinamuonyesha yuko chini? Huyo mama anasabotage brexit na hkn kingine, na ninauhakika miaka 5-10 ijayo hakuna Brexit watakuwa bado wanavutana!
Ujinga unakuelemea sana!!!!
Waziri mkuu hataki yeye, wananchi kupitia kura ya maoni wameshaielekeza serikali wanachokitaka!!! Brexit
Hiyo siyo serikali yenu ya ccm inayotekeleza majukumu yake kwa utashi wake badala ya utashi wa wananchi.
 
Barbarosa ndugu, umefuatilia vizuri issue za uchaguzi wa UK na Brexit kwa ujumla?!

Kwa uchache sana, MP wa UK alichanga karata zake vibaya!! Alikuwa na uhakika wa kupata viti vingi zaidi tofauti na madai yako kwamba aliitisha uchaguzi huku akifahamu angeshindwa!!

Na suala la Brexit lipo pale pale!!! Kura ya kutoka ilishapita na kilichobaki ni negotiations tu za hapa na pale!! Ni kama wewe uwe umempa mkeo talaka lakini kinachobaki suala zima la maslahi ya kile mlichonacho!!!

Swali langu ni kwa nini huyo Mama aliitisha Uchaguzi wkt ambapo majadiliano ya kujitoa EU ndiyo yalikuwa yaanze? Yalipaswa yaanze Juni 19, sasa haiwezekani tena, kwa maana hiyo siku Malkia ataongea na kuanza kuunda Serikali mpya ndiyo maana naamini huyo Mama ni sehemu ya establishment na pro EU, na kitakachotokea ni kwamba wataiahirisha hiyo Brexit na kuisogeza mbele forever!
 
Waziri Mkuu wa nchi hiyo ameitisha Uchaguzi ambapo alijua kbs angeshindwa

Hapo kwa bold haikuwa hivyo, ungeandika ...angeshinda tena kwa kishindo...

Kifupi ni alichotaka hajafanikiwa... ni
bonge la blunder, kapoteza control ya parliament...

Hung parliament hiyo

Inasikitisha kwangu sababu ni mwanamke ila huyo mama anamaamuzi ambayo huwa hasikilizi mengine kisa kujiamini na sasa hili limemtia doa kubwaaaaaa sana. Ni kwamba aliitisha uchaguzi akiwa na imani kuwa atashinda kwa kishindo kwa kupata viti vingiiiii zaidi... ila kamari imebackfire big time... wanampango wa kumuondoa ndani ya miezi 6, labda aondoke haraka mwenyewe au maajabu yatokeee.
 
Najua sababu kwa nini aliitisha Uchaguzi isitoshe sijakuita wala kukulazimisha uchangie hivyo acha kunipangia cha kuandika!
Na sababu huyo Waziri Mkuu ni sehemu ya establishment ambao hawataki Brexit hivyo aliitisha Uchaguzi huku akijua matokeo yake ili kusabotage Brexit, nani anakubali kuitisha Uchaguzi ili hali opinion zinamuonyesha yuko chini? Huyo mama anasabotage brexit na hkn kingine, na ninauhakika miaka 5-10 ijayo hakuna Brexit watakuwa bado wanavutana!
Hapa ndipo nakuambia kuwa huna ufahamu ingawa unajitutumua.

Kwanza, the establishment unaosema (na sijui kama unajua maana yake) ndio wanaosema hawataki sheria kutoa Brussels.

Pili, Cameron alipoingia madarakanai aliahidi kushughulikia vitu vitatu.
Kwanza kura ya maoni ya Scotland ambayo alisimama kama PM kulinda union jack.
Huyu ni PM kutoka Tory au conservatives

Pili, atashughulikia referendum ya EU. Akiwa PM alisimama na serikali kutaka UK isijitoe

Tatu,akasema atashughulikia 'wanachama' wengine wa UK, (England, Wales na Ireland) kupewa mamlaka kama ilivyo kwa Scotland ili kupunguza malalamiko ndani ya UK.

Scotland haikujitoa hivyo akawa na mandate ya kushughulikia mengine kama Brexit

Kura ya Brexit ikaamua wajitoe, yeye akiwa PM aliona hawezi kusimamia mchakato aliyoupinga wa kujitoa EU. Hakuwa na namna bali kujiuzulu

Conservative wakamchagua PM May kuziba nafasi kwa utaratibu wao.
Barbarosa ulihoji demokrasia ya chama kutoa PM na si wananchi. Tulikueleza utaratibu wao ulivyo

PM May akajikuta analazimika ku trigger article 50 of Lisbon Treaty inayoeleza mwanachama anavyojitoa. Treaty inaeleza muda ambao kwa kalenda ni takribani miaka 2

PM may alikuwa na majority katika house. Alichokifanya ni timing akijua uchaguzi ukifanyika atapata majority na kupata mandate ya kuongoza mchakato wa kujitoa kutoka kwa wananchi na si chama chake. Matokeo amepoteza majority na sasa anaunda serikali ya minority

Kwanini amepoteza?Waingereza wengi hawakuchukulia Brexit serious hivyo kutopiga kura.

Matokeo yalipotoka ikabidi yaheshimiwe. Nchi za EU zikaweka msimamo kuwa nchi inayojitoa haitaruhusiwa kuwa na mahusiano mengine tofauti ili kuzuia nchi nyingine kuendelea kujitoa

Kiuchumi hilo linaathiri sana UK kwavile inafungamana na nchi za EU kiuchumi.

Wananchi wameanza kuona matatizo mbele ya safari. Uchaguzi wa juzi waliokuwa wanadharau walipiga kura kama ishara ya kumwambia PM May kuhusu suala la kujitoa

Pamoja na hayo mchakatato utakuwa complicated lakini utaendelea.
Kama kutakuwa na mbadiliko ni jambo ambalo halijulikani hadi sasa

Barbarosa anaposema kwanini hawakujitao siku moja, hajui maana ya article 50, alipaswa kulijua

Kura ya Brexit haikuwa na chama ndiyo maana wapo labour waliokataa wapo Tory waliounga mkono n.k. Hilo ndilo tunasema non partisan kwa maana kuwa mtu hafungwi na msimamo wa chama

Hayo niliyokueleza hapo ni kwa uchache sana, kama kitone tu.
Siasa za magharibi zimekomaa si za kueleza bila kuwa na ufaahamu kama zetu za Lumumba
 
Nimekupata vizuri kiongozi...Na According to BBC hiyo jana....mchakato wakujitoa unaanza rasmi 19/06/2017 na unatarajiwa kuisha 19/06/2019
Ingawa kuna wanaona kwamba inaweza ikachukua muda mrefu..
Mfano mfanyabiashara mashuhuri Mmarekani Soros kadai Process ya kujitoa itachukua si chini ya miaka Mitano.
Kujitoa kuko palepale tu
 
Swali langu ni kwa nini huyo Mama aliitisha Uchaguzi wkt ambapo majadiliano ya kujitoa EU ndiyo yalikuwa yaanze? Yalipaswa yaanze Juni 19, sasa haiwezekani tena, kwa maana hiyo siku Malkia ataongea na kuanza kuunda Serikali mpya ndiyo maana naamini huyo Mama ni sehemu ya establishment na pro EU, na kitakachotokea ni kwamba wataiahirisha hiyo Brexit na kuisogeza mbele forever!
Mkuu hebu yaelewe haya mambo. Kama unakumbuka Lisbon treaty inataka nchi inayojitoa ku trigger article 50.

Hiyo maana yake ni kueleza nia ya kujitoa na PM May alisha trigger hiy March 29 2017.

Majadiliano hayahusu kujitoa, bali namna gani UK itaondoka katika EU.

Elewa hapo si kujitoa kwani tayari imesha trigger article 50, bali kuangalia vitu kama gharama , michango na madeni n.k. ili kuwe na smooth tranistion.

Kumbuka UK ni mwanachama mwenye nguvu sana na hilo walijua.
Haiwezi kuamka asubuhi na kusema tumejitoa.

Athari zake kwa uchumi na usalama wa dunia ni kubwa sana na ndio msingi wa kuwa na Lisbon treaty

Brexit haina uhusiano wa moja kwa moja na uchaguzi.
Uhusiano uliopo ni PM May alitaka mandate ya wananchi ya kuongoza nchi si aliyopewa na conservative.

Hapa kuna uhalali wa kisiasa katika kusimamia mambo ya nchi.

Hilo alifanya akijua conservative ni 'popular' na angepata wabunge wengi 'majoirty'.
Tofauti ikawa Hung parliament yaani serikali ya minority

Kwanini amepoteza majority? Kuna mengi .
Suala la ugaidi na yeye alikuwa waziri wa mambo ya ndani limechangia kuonyesha hana mbinu mpya

Pili kuna suala la Brexit linalowagusa watu kwa namna tofauti.
Scotland haitaki kujitoa EU, wakati wanachama wengine wa UK wakiwa wamegawanyika.

Tatu, uhusiano wa May na Trump ambao unaonekana kuwa wa 'karibu' umemgharimu hasa pale Trump alipomshambulia Mayor wa London baada ya shambulio la ugaidi.

Nne, wengi hawaoni kama PM May anaweza kuongoza UK kupata deal nzuri na EU

Haikutisha uchaguzi kwasababu ya Brexit tu kama unavyodhani. Ni zaidi ya hapo ndugu yangu
 
Wananchi wa Uingereza hawataki kuwa Wanachama wa Umoja wa Ulaya na walipiga kura ya maoni ya kujitoa, sasa kwa hali ya kawaida na kidemokrasia ilipaswa kura yao iheshimiwe na nchi ya Uingereza kujiondoa mara moja!

Lkn kinyume chake kimetokea maelite walikuwa hawataki Uingereza iondoke EU na sasa wamefanikiwa, Waziri Mkuu wa nchi hiyo ameitisha Uchaguzi ambapo alijua kbs angeshindwa na sasa anaunda Serikali na Chama ambacho hakitaki Uingereza ijitioe EU, ina maana sasa haiwezekani tena, na mara nyingine Wananchi wamedanganywa na maelite kwamba wanaishi kwenye Demokrasia na kwamba wao ndiyo wanaamua jinsi wanavyotaka kuishi kumbe ni danganya Toto na kiini macho!

Sasa najiuliza ile kura ya maoni ilikuwa ya kazi gani kama walijua hawawezi kutekeleza matokeo yake?
Uingereza wameshajitoa EU baada ya ku trigger article 50. Hii inamaana baada ya miaka miwili kama hakuna negotiations yoyote kati ya EU na UK, by design UK inakuwa imetoka kwa style ya hard exit. Yani eu itadeal na UK kama inavyodeal na Tanzania. Yani Ita default kwa deal zote mwanzo zilizokuwapo tu null
 
Nimekupata vizuri kiongozi...Na According to BBC hiyo jana....mchakato wakujitoa unaanza rasmi 19/06/2017 na unatarajiwa kuisha 19/06/2019
Ingawa kuna wanaona kwamba inaweza ikachukua muda mrefu..
Mfano mfanyabiashara mashuhuri Mmarekani Soros kadai Process ya kujitoa itachukua si chini ya miaka Mitano.
Kujitoa kuko palepale tu
Tatizo kubwa la huyu Waziri mkuu litaletwa kutokana na muungano wake na DUP,ambao hawataki same sex marriages,hawataki kabisa Ireland mbili ziwekewe border controls sababu wanasema ni ndugu-tatizo Ireland mmoja iko EEU-sasa bila controls any person from the other side ataingia tuu.Kwa vyovyote hii marriage of convenience italeta cracks maana DUP,lazima kuna mambo atayataka ambayo conservative hatapendezewa but yet atakuwa powerless kuyazuia maana DUP anaweza kutishia kujiondoa katika muungano na uchaguzi ukafanyika tena-Conservatives wengi wameliona hili tatizo ambalo latamfanya Theresa May kuwa mpole and hence kushindwa kutimiza majukumu
Wanadai sababu mambo yame backfire kashindwa kupata majority ambayo mwanzoni alikuwa nayo,awajibike,ajiuzuru
 
Back
Top Bottom