Uchaguzi wa kielektroniki katika kukuza Utawala Bora na demokrasia nchini F Tanzania

Imma_Magira

Member
Jan 8, 2022
18
26
Na Emmanuel Magira.

BHRM-Mzumbe University.

UTANGULIZI.
Katika karne hii ya 21, mapinduzi na mageuzi ya teknolojia yamechangia maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali. Miongoni mwa maendeleo hayo ni pamoja na kuwepo kwa mifumo wezeshi inayorahisisha ununuzi, utoaji huduma kwa wananchi na kadharika.

Pamoja na kwamba Tanzania imetambua umuhimu wa teknojia katika kurahisisha upatikanaji wa huduma miongoni mwa sekta muhimu kama afya, madini, usafirishaji nakadharika. Lakini ajabu ni kwamba, serikali haijatambua umuhimu wa teknolojia katika mchakatoi wa upatikanaji wa viongozi (uchaguzi mkuu). Ukweli usio wa kupepesa macho ni kwamba uchaguzi mkuu ndio kiini kikubwa cha kuwepo kwa utawala bora na demokrasia nchini, lakini tofauti na hivyo hakuna nguvu au mchakato uliowekwa kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa na misingi ya uwazi na usawa kwa kuwepo mifumo thabiti ya teknojia au elektroniki itakayohakikisha upatikanaji wa misingi hiyo.

KWANINI MIFUMO YA KIELEKTRONIKI KATIKA UCHAGUZI MKUU?
Mbali na kwamba teknolojia ya mifumo ya kielektroniki imekuwa mkombozi katika nyanja tofautitofauti, lakini pia ina uwezo mkubwa wa kuboresha mchakato wa upatikanaji wa viongozi bora katika uchaguzi mkuu. Uwepo wa mifumo katika uchaguzi mkuu unagusia moja kwa moja kuimarisha demokrasia na utawala bora nchini. Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu yanayoweza kuchagizwa na uwepo wa mifumo ya elektroniki katika uchaguzi mkuu ili kukuza demokrasia na utawala bora.

1. Kuongeza uwazi na uwajibikaji. Kwa miaka kadhaa sasa, Tanzania imekuwa ikifanya uchaguzi lakini kipimo cha uwajibikaji kimekuwa ni hafifu kwani viongozi hawawajibiki kwa nafasi walizopo. Hivypo nafkiria mifumo hii mipya inaweza kuwa mwarobaini wa tatizo hili ingawa hatuna uhakika wa moja kwa moja. Mfano Mifumo ya kierektoniki inaweza kutumika kuhesabu kura kwa usahihi na kurekodi matokeo kwa uwazi. Hii inaweza kupunguza uwezekano wa udanyanyifu katika uchaguzi. (kama ambavyo chama tawala kimekuwa kikishutumiwa).

2. Kupunguza gharama za uchaguzi; Ni mara moja tu Tanzania imefanikiwa kuendesha uchaguzi mkuu kwa fedha za ndani, na hii ilikuwa kipindi cha hayati DKT. JOHN POMBE MAGUFULI. Ingawa hatuna uhakikia kuwa hali itaendelee kuwa hivyo, aidha uwepo wa mifumo hii wezeshi itapunguza gharama za uendeshaji wa uchaguzi na badala yeke fedha na rasilimali nyingine zinaweza kuelekezwa katika miradi mingine ya maendeleo. Mifumo ya kielekroniki inaweza kutumika kuhesabu kura tofauti na kuhesabu kura kwa njia ya kawaida.

3. Kuokoa muda na kurahisicha mchakato; Mifumo hii inaeza kutumika kurahisisha mchakato na kuokoa muda kwa ujumla, hii itaambatana na usajili wa wapiga kura, upigaji kura wenyewe, uchambuzi na uhakiki wa data, vilevile kurahisiha mawasiliano baina ya maafisa wa uchaguzi. Mambo yote haya yakifanyika yataokoa muda unaotumika wakati wa uchaguzi.

(Nimegusia kwa juu juu umuhimu wa mifumo ya kielektroniki ingawa umuhimu wake ni mkubwa)

KIPI KIFANYIKE KABLA YA KUANZISHA UCHAGUZI WA KIELEKTRONIKI?
Ukweli ni kwamba upande wa pili wa sarafu, yaani teknolojia inaweza kuleta athari hasi endapo ikikosa udhibiti wa kina katika kutumika kwake.

Sambamba na hilo nature ya eneo husika (Tanzania), inaweza/linaweza kusababisha utekelezaji huu kuwa mgumu zaidi. Yafuatazo ni mambo ambayo ni vyema kutatuliwa mapema kabla ya uanzishwaji wa mifumo ya kielektroniki katika uchaguzi mkuu.

1. Teknolojia thabiti; Habari ya kusikitisha ni kwamba Tanzania tuko nyuma katika teknojia, hali ni ngumu katika uanzishwaji wa mifumo hii ya elekroniki katika uchaguzi mkuu. Mfano huduma za internet hazipatikani maeneo yote ya Tanzania, hali hii ni kikwazo cha ufanikishwaji wa jambo hili.

2. Kuwepo kwa miundombinu rafiki ya uchaguzi wa kielekroniki; Ili mifumo hii itumike vyema na kuleta matokeo chanya, Tanzania ni vyema kuweka miundombinu mizuri kama nishati. Mfano Tanzania sasa inapitia kipindi kigumu cha kukatika umeme hali hii sio rafiki kwa teknolojia itakayotumika uchaguzi mkuu.

3. Usalama wa mtandao (cybersecurity safety); Kwasababu tuko katika mageuzi makubwa ya teknojia ya sayansi ya komputa na mifumo endeshi, ni vyema kama serikali kuzingatia mifumo ya usalama wa mtandao ili kuzuia udukuzi na uharifu wa mitandao, hii ni kuhakikisha usalama wa data(kura).

4. Elimu katika matumizi ya vifaa vya kielekroniki; Hadi kufikia Januari 2023 ni asilimia 31.6 tu sawa na watanzania millioni 19.8 ambao wanaweza kutumia huduma ya intaneti. Idadi hii ni ndogo katika kufanikisha uchaguzi wa kielektroniki. hivyo kinachotakiwa kufanywa ni kuwepo na mifumo ya kielekroniki itakayowekwa katika vituo maalumu, kisha baadhi ya wasiokuwa na uwezo wa kupata huduma ya intaneti kwenda maeneo hayo na kuwasilisha kura zao.

(Manbo ya kuzingatia yanaweza kuwa ni mengi kulingana na nyakati zinavyobadilika, hayo ni baadhi tu)

HITIMISHO.
Ni kweli hatuna uhakika kama dhana hii ya uwepo wa mifumo ya kierektoniki inaweza kuleta matokeo chanya, lakini ni vyema kama serikali ikilifanyia utafiti na kulijaribu pia. Kwani hata hivyo mfumo wa uchaguzi unayotumika sasa hauna matokeo ya uhakika katika kukuza demokrasia na utawala bora nchini.

Sambamba na hilo uwepo wa vyuo vikuu mbalimbali nchini unaweza kusaidia upatikanaji wa wataalamu wa mifumo na sayansi ya kompyuta. Aidha ushirikishwaji wa wataalamu hawa utatoa fursa ya uvumbuzi na nafasi ya kuonyesha uwezo wao binafsi.
 
Na Emmanuel Magira.

BHRM-Mzumbe University.

UTANGULIZI.
Katika karne hii ya 21, mapinduzi na mageuzi ya teknolojia yamechangia maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali. Miongoni mwa maendeleo hayo ni pamoja na kuwepo kwa mifumo wezeshi inayorahisisha ununuzi, utoaji huduma kwa wananchi na kadharika.

Pamoja na kwamba Tanzania imetambua umuhimu wa teknojia katika kurahisisha upatikanaji wa huduma miongoni mwa sekta muhimu kama afya, madini, usafirishaji nakadharika. Lakini ajabu ni kwamba, serikali haijatambua umuhimu wa teknolojia katika mchakatoi wa upatikanaji wa viongozi (uchaguzi mkuu). Ukweli usio wa kupepesa macho ni kwamba uchaguzi mkuu ndio kiini kikubwa cha kuwepo kwa utawala bora na demokrasia nchini, lakini tofauti na hivyo hakuna nguvu au mchakato uliowekwa kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa na misingi ya uwazi na usawa kwa kuwepo mifumo thabiti ya teknojia au elektroniki itakayohakikisha upatikanaji wa misingi hiyo.

KWANINI MIFUMO YA KIELEKTRONIKI KATIKA UCHAGUZI MKUU?
Mbali na kwamba teknolojia ya mifumo ya kielektroniki imekuwa mkombozi katika nyanja tofautitofauti, lakini pia ina uwezo mkubwa wa kuboresha mchakato wa upatikanaji wa viongozi bora katika uchaguzi mkuu. Uwepo wa mifumo katika uchaguzi mkuu unagusia moja kwa moja kuimarisha demokrasia na utawala bora nchini. Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu yanayoweza kuchagizwa na uwepo wa mifumo ya elektroniki katika uchaguzi mkuu ili kukuza demokrasia na utawala bora.

1. Kuongeza uwazi na uwajibikaji. Kwa miaka kadhaa sasa, Tanzania imekuwa ikifanya uchaguzi lakini kipimo cha uwajibikaji kimekuwa ni hafifu kwani viongozi hawawajibiki kwa nafasi walizopo. Hivypo nafkiria mifumo hii mipya inaweza kuwa mwarobaini wa tatizo hili ingawa hatuna uhakika wa moja kwa moja. Mfano Mifumo ya kierektoniki inaweza kutumika kuhesabu kura kwa usahihi na kurekodi matokeo kwa uwazi. Hii inaweza kupunguza uwezekano wa udanyanyifu katika uchaguzi. (kama ambavyo chama tawala kimekuwa kikishutumiwa).

2. Kupunguza gharama za uchaguzi; Ni mara moja tu Tanzania imefanikiwa kuendesha uchaguzi mkuu kwa fedha za ndani, na hii ilikuwa kipindi cha hayati DKT. JOHN POMBE MAGUFULI. Ingawa hatuna uhakikia kuwa hali itaendelee kuwa hivyo, aidha uwepo wa mifumo hii wezeshi itapunguza gharama za uendeshaji wa uchaguzi na badala yeke fedha na rasilimali nyingine zinaweza kuelekezwa katika miradi mingine ya maendeleo. Mifumo ya kielekroniki inaweza kutumika kuhesabu kura tofauti na kuhesabu kura kwa njia ya kawaida.

3. Kuokoa muda na kurahisicha mchakato; Mifumo hii inaeza kutumika kurahisisha mchakato na kuokoa muda kwa ujumla, hii itaambatana na usajili wa wapiga kura, upigaji kura wenyewe, uchambuzi na uhakiki wa data, vilevile kurahisiha mawasiliano baina ya maafisa wa uchaguzi. Mambo yote haya yakifanyika yataokoa muda unaotumika wakati wa uchaguzi.

(Nimegusia kwa juu juu umuhimu wa mifumo ya kielektroniki ingawa umuhimu wake ni mkubwa)

KIPI KIFANYIKE KABLA YA KUANZISHA UCHAGUZI WA KIELEKTRONIKI?
Ukweli ni kwamba upande wa pili wa sarafu, yaani teknolojia inaweza kuleta athari hasi endapo ikikosa udhibiti wa kina katika kutumika kwake. Sambamba na hilo nature ya eneo husika (Tanzania), inaweza/linaweza kusababisha utekelezaji huu kuwa mgumu zaidi. Yafuatazo ni mambo ambayo ni vyema kutatuliwa mapema kabla ya uanzishwaji wa mifumo ya kielektroniki katika uchaguzi mkuu.

1. Teknolojia thabiti; Habari ya kusikitisha ni kwamba Tanzania tuko nyuma katika teknojia, hali ni ngumu katika uanzishwaji wa mifumo hii ya elekroniki katika uchaguzi mkuu. Mfano huduma za internet hazipatikani maeneo yote ya Tanzania, hali hii ni kikwazo cha ufanikishwaji wa jambo hili.

2. Kuwepo kwa miundombinu rafiki ya uchaguzi wa kielekroniki; Ili mifumo hii itumike vyema na kuleta matokeo chanya, Tanzania ni vyema kuweka miundombinu mizuri kama nishati. Mfano Tanzania sasa inapitia kipindi kigumu cha kukatika umeme hali hii sio rafiki kwa teknolojia itakayotumika uchaguzi mkuu.

3. Usalama wa mtandao (cybersecurity safety); Kwasababu tuko katika mageuzi makubwa ya teknojia ya sayansi ya komputa na mifumo endeshi, ni vyema kama serikali kuzingatia mifumo ya usalama wa mtandao ili kuzuia udukuzi na uharifu wa mitandao, hii ni kuhakikisha usalama wa data(kura).

4. Elimu katika matumizi ya vifaa vya kielekroniki; Hadi kufikia Januari 2023 ni asilimia 31.6 tu sawa na watanzania millioni 19.8 ambao wanaweza kutumia huduma ya intaneti. Idadi hii ni ndogo katika kufanikisha uchaguzi wa kielektroniki. hivyo kinachotakiwa kufanywa ni kuwepo na mifumo ya kielekroniki itakayowekwa katika vituo maalumu, kisha baadhi ya wasiokuwa na uwezo wa kupata huduma ya intaneti kwenda maeneo hayo na kuwasilisha kura zao.

(Manbo ya kuzingatia yanaweza kuwa ni mengi kulingana na nyakati zinavyobadilika, hayo ni baadhi tu)

HITIMISHO.
Ni kweli hatuna uhakika kama dhana hii ya uwepo wa mifumo ya kierektoniki inaweza kuleta matokeo chanya, lakini ni vyema kama serikali ikilifanyia utafiti na kulijaribu pia. Kwani hata hivyo mfumo wa uchaguzi unayotumika sasa hauna matokeo ya uhakika katika kukuza demokrasia na utawala bora nchini. Sambamba na hilo uwepo wa vyuo vikuu mbalimbali nchini unaweza kusaidia upatikanaji wa wataalamu wa mifumo na sayansi ya kompyuta. Aidha ushirikishwaji wa wataalamu hawa utatoa fursa ya uvumbuzi na nafasi ya kuonyesha uwezo wao binafsi.
Mfumo wa kielektroniki? Kamwe CCM hawawez kubali!! 👇👇Wanaelewa madhara yake.
 
Attachments

  • Screenshot_20230408-204546.png
    Screenshot_20230408-204546.png
    151.8 KB · Views: 2
Mkuu hili bandiko linaibua mjadala mpana sana, ni kweli uchaguzi wa kielektroniki una faida kubwa sana ila Kuna masuala muhimu kama usalama, je kiasi gani mifumo itakua secured kuepuka kura kuwa intercepted au kuongezwa kimagendo?

Kingine Kuna suala la privacy mfano umepiga kura Yako kwa mgombea wa upinzani ilihali ni mtumishi wa umma je kivipi mfumo utatunza Siri kutovuja?

Kuna concern ya wapiga kura hewa kupigiwa kura au kutumia robots kupiga kura kwa kutumia ID za watu halisi ambao hawakupiga kura siku ya uchaguzi. Siku hizi Kuna AI na analytics tools kali sana zinaweza predict matokeo kabla kura hazijapigwa hzii algorithm zinaweza tumiwa kuandaa model za regression zinazoweza manipulate kura za wananchi kama zilivyotumika uchaguzi wa Kenya 2013 kumuibia Odinga.

Nachoshauri mfumo wa kielektroniki utumike sambamba na manual kama USA au Kenya ambapo matokeo yanakuepo both electronically na manually Ili verification ifanyike kwa urahisi kwamba matokeo ya manual yafanane na electronic.
 
Mifumo ya kierektoniki inaweza kutumika kuhesabu kura kwa usahihi na kurekodi matokeo kwa uwazi. Hii inaweza kupunguza uwezekano wa udanyanyifu katika uchaguzi. (kama ambavyo chama tawala kimekuwa kikishutumiwa).
Ccm hawawezi kukubali hili kirahisi maana ni kujitia kitanzi.

Hii mifumo pia ni rahisi kuchezewa hasa kwenye dunia ya sasa, hivyo itahitaji udhibiti mkali sana na bado wanaweza wasifanikiwa 100%.
 
Back
Top Bottom