Tetesi: Brenda William Lukuvi kugombea ubunge jimbo la Isimani

Tetesi: Brenda William Lukuvi kugombea ubunge jimbo la Isimani

Hii mada imeanzishwa na mkuu 'tpaul'?

Tanzania kamwe haitaepuka maajabu; hasa tukiwa chini ya himaya ya kundi hili la watu waovu!

Hakuna litakalozuia kuiondoa Tanzania katika uduni huu.
Msaliti
 
CCM ina wenyewe n wenyewe ndio hao n watoto wao n kizazi chao TU.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Katika kuonesha ari ya kupokea kijiti cha baba yake na kuendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo la Isimani, mtoto wa marehemu William Lukuvi (Brenda Lukuvi) anatarajia kuchukua fomu ya kuwatumikia wapigakura wa jimbo la Isimani. Jimbo hili limekuwa likishikiliwa na baba yake kwa zaidi ya miaka 30 (1995-2026) kabla mbunge huyo nguli wa CCM kufariki dunia mwanzoni wa mwezi Machi, 2026.

"Kwa kuzingatia utamaduni wa chama chetu, kamati ya ushauri inapendekeza Brenda Lukuvi achukue fomu na kuendelea kuliongoza jimbo la Isimani amalizie kazi nzuri iliyofanywa na baba yake", alisema kigogo mmoja wa CCM kutoka Isimani ambaye hakupenda kuweka jina lake hadharani.
View attachment 3564064
Mh Brenda Lukuvi (mbunge wa Isimani ajaye)

MAONI YANGU
Mimi nashauri binti huyu akabidhiwe jimbo. Kwa kuwa baba yake amelifanyia mambo makubwa jimbo la Isimani, sioni sababu ya mtu mwingine kushika kijiti cha baba yake. Naunga mkono chama cha mapinduzi jimbo la Isimani kupendekeza jina la Brenda kuongoza jimbo la Isimani. Kwanza huyu ni msomi na amejifunza mambo mengi kutoka kwa baba yake. Namuunga mkono hoja 💯%.
Naunga mkono hoja
 
Yeah. Nimeanzisha mimi tpaul mkuu. Nikiwa mwanaIsimani mwandandamizi, nampigia chapuo Brenda kupokea kijiti cha babaye.
Ninaisikitikia sana Tanzania yetu hii, mkuu wangu 'tpaul' kwa mwelekeo huu tunaoenda nao sasa hivi.

Lakini najuwa, matumaini yapo, tena sana ya kuliondoa taifa hili kwenye balaa hili. linalolizonga.
 
Back
Top Bottom