tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 26,021
- 25,422
Katika kuonesha ari ya kupokea kijiti cha baba yake na kuendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo la Isimani, mtoto wa marehemu William Lukuvi (Brenda Lukuvi) anatarajia kuchukua fomu ya kuwatumikia wapigakura wa jimbo la Isimani. Jimbo hili limekuwa likishikiliwa na baba yake kwa zaidi ya miaka 30 (1995-2026) kabla mbunge huyo nguli wa CCM kufariki dunia mwanzoni wa mwezi Machi, 2026.
"Kwa kuzingatia utamaduni wa chama chetu, kamati ya ushauri inapendekeza Brenda Lukuvi achukue fomu na kuendelea kuliongoza jimbo la Isimani amalizie kazi nzuri iliyofanywa na baba yake", alisema kigogo mmoja wa CCM kutoka Isimani ambaye hakupenda kuweka jina lake hadharani.

Mh Brenda Lukuvi (mbunge wa Isimani ajaye)
MAONI YANGU
Mimi nashauri binti huyu akabidhiwe jimbo. Kwa kuwa baba yake amelifanyia mambo makubwa jimbo la Isimani, sioni sababu ya mtu mwingine kushika kijiti cha baba yake. Naunga mkono chama cha mapinduzi jimbo la Isimani kupendekeza jina la Brenda kuongoza jimbo la Isimani. Kwanza huyu ni msomi na amejifunza mambo mengi kutoka kwa baba yake. Namuunga mkono hoja 💯%.