Breakin News....PM Pina asitisha bomoa bomoa nchi nzima

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,020
691
Wapenda nipo kwenye msafara wa PM katika mkoa wa Kagera.Amehutubia wananci hapa chato na kuagiza kusitishwa kwanza zoezi la bomoa bomoa kando ya barabara na lile zoezi la mabango kupigwa alama ya X nalo limesitishwa kwanza.......

tupo pamoja

mb
 
Sasa hii mbona ni conflict ndani ya baraza la mawaziri?
Alitakiwa awasiliane na aliyetoa amri hiyo kwa mara ya kwanza ili yeye mwenyewe atumike kusitisha kama kuna ulazima zaidi ya mambo ya siasa.
Vpi kwenye msafara kuna NYOMI kama lile letu?
 
basi wakati muafaka wa Doctor wa ukweli JOHN P MAGUFULI kuachana na ccm!huwezi kupata maendeleo bila sacrifice!babu zetu walihenyeshwa na wajerumani kufyeka misitu ndio tukapata reli ambayo ccm imeiua!sasa namna hii miundombinu itajengwaje?kwa nini hawa watu wa ccm wanakauli zinazokinzana?baraza la mawaziri likikutana huzungumzia nini na kuwa na tamko la pamoja kama serikali?
 
Kama hii issue ni kweli mh. pombe inabidi atoke......PM alichokifanya ni kinyume kabisa na utendaji wa pamoja na ni kumdhalilisha waziri wake!!!!!! :A S 13:
 
Hii inategemewa kwa serekali isiyona msingi wa kujiendesha...

... Kila mtu anaatoka kivyake!
 
Hawa Mafisadi wanapinga wenyewe kwa wenyewe, Chadema inatishia amani ya Mafisadi wa ccm. Wengine wanakuja na kauli za kutishia wananchi au wanachimba mkwala kwa chadema wengine wanaomba msaada kwa vibaraka wao wakina Shimbo na Mwema. Subirini Mafisadi wakina Kikwete na Majambazi wenzake wanajinyea nyea kwenye masuruali yao ya vijisenti. :wink2:
 
Hii cabinet imejaa vigeugeu yaani mtu anatoa maamuzi ya maana kwa maslahi ya taifa wao kwa ujinga na maslahi ya matumbo yao wanazuia! Nikisikia tena mtu anamuita Pinda eti ni mtoto wa Mkulima....namtukan....
 
Tupate uhakika kwanza. Nimeangalia Taarifa ya Habari ya ITV hakuna hio habari. Lazima ingekuwa ni front 'Screen' (page!) News. Sana Sana nimemsikia PM wetu eti naye 'ANASIKITIKA' wananchi wa Kagera kuuziwa sukari kilo 1 Shs 2000!
ANasikitika!! Badala ya KUCHUKUA HATUA yeye anasikitika! Sisi wananchi tunasikitika na Waziri Mkuu naye anasikitika badala ya kuchukua hatua!! Ati anasema kesho ataenda kumuuliza mwenye kiwanda cha sukari Kagera kwa nini anawauzia wananchi sukari kilo shs alfu2!!! Atakosa sababu??? Hawa jamaa kweli ni wasanii na kiongozi wao mkuu.
 
Pinda na nitoke vipi! Eti ni ajabu watu wa kagera wanauziwa sukari sh 2000, je amefanya nini baada ya kugundua hilio! Yale yale!
 
Tupate uhakika kwanza. Nimeangalia Taarifa ya Habari ya ITV hakuna hio habari. Lazima ingekuwa ni front 'Screen' (page!) News. Sana Sana nimemsikia PM wetu eti naye 'ANASIKITIKA' wananchi wa Kagera kuuziwa sukari kilo 1 Shs 2000! .

Wananchi wa Kagera ningewashauri kwenye mikutano ya PM msisahau ndoo za kukingia machozi maana baada yaPM kusikitikia matatizo yenu soon ataanza kulia kama kawaida yake.
 
Wapenda nipo kwenye msafara wa PM katika mkoa wa Kagera.Amehutubia wananci hapa chato na kuagiza kusitishwa kwanza zoezi la bomoa bomoa kando ya barabara na lile zoezi la mabango kupigwa alama ya X nalo limesitishwa kwanza.......

tupo pamoja

mb

haya anatumia madaraka yake kunusuru serikali maana wananchi wamechukizwa na bomoa bomoa kwa vile serikali yenyewe ilifanya uzembe huko nyuma
 
Back
Top Bottom