Bosi wangu ananuka mdomo, nifanyeje?

Bosi wangu ananuka mdomo, nifanyeje?

Hivi mnafikiri ni rahisi kumwambia mtu ananuka mdomo?Labda muwe mmeshibana sana.
Kuna rafiki yangu alikuwa na hilo tatizo. Sasa ile hali watu hawaipendi hasa akiwainamia ili kuelekezana jambo na kumwambia ikiwa ngumu sana. Nikafuatwa niongee nae. Nilishindwa kumchana live ikabidi niende nae pharmacy nikanunua PK nae nikampa moja. Nikamwambia tumiaga hizi ni nzuri kwenye kukupa confidence. Sasa sijui kama alielewa dhumuni husika.
 
Mwambie lets drink mouthwash...joking

Mnunulie dawa ya mswaki,mswaki na mouthwash muwekee ofisini kwake bila ye kujua wala asikuone mtu

Type ujumbe😱ngeza usafi wa kinywa mkuu
Usiandike jina wala nini muachie hapo we jikausheee
 
Kuna kunuka mdomo kunakotokana na visababishi mfano kula nyama sana,kula vitunguu swaumu na vitunguu vya kawaida,Kunywa pombe hasa pombe kali uvutaji wa tumbaku.Lakini matatizo ya visababishi huwa yana muda wake sio ya kudumu yanaisha yenyewe au mtu akitumia mswaki na dawa na mouth wash.Kuna upande mwingine mtu ananuka mdomo kwa ugonjwa ugonjwa huu kitaalamu unaitwa HALITOSIS.
Mtu mwenye hali hii anahitaji kumuona daktari sio kumcheka ni ugonjwa kama magonjwa mengine.Ila kuzuiya hii kitu kwa muda kuna kutumia vitu vya kienyeji mfano maziwa mgando kunywa na kunywa maji ya ukoko wa ugali
Kumbukeni kuna watu pia wanaonuka mwili hata akioga mara ngapi yote haya ni matatizo ya ugonjwa tusichekane
 
Ugonjwa wa kunuka mdomo unaongezeka, ukitaka kuthibitisha chunguza ndani ya daladala au mwendokasi, na hata wakati mwingine makanisani.

Sijajua watu wanaugua hivi kwa nini lakini nijuacho ni kwamba hakuna watu wakorofi kama wanaonuka mdomo hasa ukiwaambia wananuka mdomo.

Sasa ugonjwa huu umeanza kuvamia na maofisini. Bosi wangu ananuka mdomo, sijui ni kwa sababu hapigi mswaki au ana matatizo ya kiafya.

Nimesema walivyo wakorofi wanaonuka mdomo. Sasa kama bosi ukimwambia kuwa ananuka mdomo, basi ndiyo kabisa, afadhali na wale wa kwneye daladala.

Nisaidieni jinsi ya kumfanya bosi wangu ajijua kuwa ananuka mdomo, maana inanikera.
Mnunulie dawa km forever mpatie mwambie umepew zawadi nyingi hizo ukaona umgawie na yeye.
 
Ugonjwa wa kunuka mdomo unaongezeka, ukitaka kuthibitisha chunguza ndani ya daladala au mwendokasi, na hata wakati mwingine makanisani.

Sijajua watu wanaugua hivi kwa nini lakini nijuacho ni kwamba hakuna watu wakorofi kama wanaonuka mdomo hasa ukiwaambia wananuka mdomo.

Sasa ugonjwa huu umeanza kuvamia na maofisini. Bosi wangu ananuka mdomo, sijui ni kwa sababu hapigi mswaki au ana matatizo ya kiafya.

Nimesema walivyo wakorofi wanaonuka mdomo. Sasa kama bosi ukimwambia kuwa ananuka mdomo, basi ndiyo kabisa, afadhali na wale wa kwneye daladala.

Nisaidieni jinsi ya kumfanya bosi wangu ajijua kuwa ananuka mdomo, maana inanikera.
Tena wakorofi mno tena mno. Ila tatizo ni uchafu wa meno, akienda kusafisha anapona kabisa. Labda jifanye ulienda kusafisha meno, then mwambie faida yake umshauri aende.
 
Sio tatzo kupiga mswaki tu tatzo halafu inatoka tumbon kwani kuna baadhi ya watu hunywa kiasi kidogo cha maji hata kama atapiga mswak atakuwa ananuka tu
Hilo nalo somo jipya umenipa nilikuwa sijui. Mbona hatujawataja wala ugoro na wavutaji wa sigara? Siku hizi nasikia vijana wengi wanakula ugoro hivi kweli?
 
Hivi vijiwe Huwa vinaharufu kali ajabu aseh alafu ni kama Huwa vinatoka vyenyewe tu vikifika size flani
Watu wengi huswaki juujuu tu...

Anaetaka nimfundishe jinsi anifuate PM....

WATU WAZEMBE SANA...

NI SAWA TU NA MANAMKE YANAYOSHINDWA OSHA K ZAO.
 
Midomo kunuka inabidi kupiga mswaki kila unapomaliza chakula iwe asubuhi, mchana na jioni. Mswaki si meno bali gums na hasa ulimi maana ndo unabeba uchafu mwingi. Vikwapa ni kununua Deodorants kama huwezi basi tumia limau au hakikisha huna nywele kwenye vikwapa na utumie sabuni inayonukia. Mimi siyo daktari ila ni uzoefu wangu tu.
Me napiga mswaki asubuhi kwa asubuhi lakini sinuki mdomo. Nini sababu?..
Nikioga asubuhi mpaka napolala na bado mchana hata iweje siwezi nuka jasho ingawa naweza toka maji/jasho, ni tatizo pia!?..
 
Hilo nalo somo jipya umenipa nilikuwa sijui. Mbona hatujawataja wala ugoro na wavutaji wa sigara? Siku hizi nasikia vijana wengi wanakula ugoro hivi kweli?
ugoro ndio umekuwa mbadala wa viroba
 
Me nakushauri nunua line mpya ya simu, kisha mtext kwa kutumia hiyo namba mpya ukimueleza hilo tatizo lake kisha muelekeze clinic ya magonjwa ya kinywa iliyopo karibu ili aende kutibu tatizo linalomsibu.

Ni vema kumsaidia mtu anapokuwa na tatizo badala ya kumkalia kimya maana ukikaa kimya huwezi jua labda na yeye hajijui au ameshindwa kujua suluhu.
 
Me napiga mswaki asubuhi kwa asubuhi lakini sinuki mdomo. Nini sababu?..
Nikioga asubuhi mpaka napolala na bado mchana hata iweje siwezi nuka jasho ingawa naweza toka maji/jasho, ni tatizo pia!?..
Ha ha ha wewe umenichekesha. Kuna watu tangu wazaliwe wanatumia mkaa tu na hawanuki. Vyakula unavyokula na lifestyle yako ni nzuri ila namfahamu mtu hanywi pombe anakula organic food na ni mtu asiye na makuu, hana kisukari kama mchangiaji mmoja alivyosema lakini akifunua mdomo kuongea, unaangalia pembeni.
 
Pole mkuu, hata nyinyi humu JF wapo wanaonuka midomo nadhani. Siyo hiyo tu hata vikwapa.

Midomo kunuka inabidi kupiga mswaki kila unapomaliza chakula iwe asubuhi, mchana na jioni. Mswaki si meno bali gums na hasa ulimi maana ndo unabeba uchafu mwingi. Vikwapa ni kununua Deodorants kama huwezi basi tumia limau au hakikisha huna nywele kwenye vikwapa na utumie sabuni inayonukia. Mimi siyo daktari ila ni uzoefu wangu tu.
Kuna magonjwa kama constipation na halitosis....
Haya hata upige mswaki mara 20 kwa siku, tatizo halikuachi na linazidi kuwa kubwa kila uchao......
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom