Boris Johnson akashifu wanawake wavaa hijab

okay thanks a bunch, sasa kwamba hiyo ni kashfa kwa wavaa hijab ni mawazo yako wewe! Hakuna mahala rasmi pameandikwa Boris Johnson awakashifu wavaa hijab. Kwa sababu hawakubaliani Waingereza wote kwamba hijab ni njema, wapo wanaomtetea Boris Johnson.

tamaduni za Magharibi ni tofauti na utamaduni wa waarabu, tusilazimishe kuwamezesha kooni matamaduni ya kigeni wenyeji wanapotukaribisha tuishi kwao.

hakuna mahala Quran Takatifu imeongelea kuvaa hijab, niqab wala burka

in fact, hakuna mahala popote kwenye Quran Takatifu pameongelewa uvaaji wa Muislam period.

kwa hiyo ukiona mtu Kariakoo kavaa suruali ya dont-tachi na barakashia na kanzu, huo sio uislam, ni ma-utamaduni ya Uarabuni tumeyabuguia jumla. On the other hand huwezi kwa miaka milioni kukuta muarabu kavaa kitenge cha Mswahili au lubega la Mmasai...

facial expression, eye contact and positive identification of who the hell you are in public space are time-honored values of the western culture...

Hijab, Niqab, Burka zimepigwa marufuku Morocco, Cameroon, Chad, Republic of the Congo, Gabon, Austria, Denmark, France, Belgium, Tajikistan, Latvia, Netherlands pamoja na China
This is a fat white lie..
 
Mbona jamaa yuko sawa tu,Waisilamu bana,ulaya mbali sana hata hapa bongo, mtu akija kwako,sio yeye akupangie ufanye nini bali anatakiwa kufata taratibu za familia yako,kama saa moja wote mnatakiwa kuwa nyumbani inatakiwa iwe hivyo na si vinginevyo,hutaki nenda kwako,kuanzia kubishana na mwenye mji ati kisa imani yako wakati ni kinyume na utamaduni wake ni kukosa akili tu,mbona wengine tunavaa kanzu ingawa sio imani yetu sababu tu usimkwaze mwenyeji wako,hii dunia yetu nikubwa kuna watu huu ukristo au uisilamu hawaujui kabisa usipokubadili kubadilika utapata tabu sana ni bora ukae hapo ulipo tu
Ishu sio wanapangiwa nini cha kufanya. Ishu ni kukashifu. Hata hapa Bongo ukisema Wamasai yale mashuka yao yanafanana na miti utakuwa umekashifu.....
 
And BTW Kwanini waislam ulazimisha tamaduni zao kufuatwa hata kwenye nchi zisizo za kiislam /kidini ilhali wanaokwenda kwao uheshimu mila na desturi za huko?
Mzee baba... hivi mvaa hijab kutaka uvaaji wake wa hijab kuheshimiwa ni kulazimisha ufuatwe?

mtu kavaa kaambiwa anafanana na jambo fulani kalazimisha.

mmasai kuvaa shuka New York then akatukanwa kwa kuvaa shuka kalazimisha New York nao wavae? sijui hata sikuelewi
 
True that..actuallly hata hao wanajidai kumtaka Boris aombe msamaha moyoni wanawaza kingine. Wazungu huwaambii kitu kwa tamaduni zao, ndio maana Germany,Netherlands na kwingineko wala hawafichi..kwao koleo ni koleo na kijiko ni kijiko.. Ukitaka kuishi kwetu fuata tamaduni zetu au la rudi kwenu
Jamani hivi huko Netherlands na German mmefika?mbona watu wanavaa hijabu kama kawa. Ila kwa baadhi ya ofisi za serikali ikiwa were Ni mfanyakazi mfano:, nesi, lakini kilakona watu wanavaa..
Halafu kitu mnapaswa kujua ni kuwa, uislamu kwa dunia ya sasa so Wa waarabu tu. Sasa hivi kuna wimbi kubwa LA wazungu wazaliwa halisi wanaingia katika uislamu na wanaupractise uislamu kuliko hao waarabu. Ndio maana unaona kelele za haki za waislamu ulaya zimezidi.. Sababu wana haki katika mataifa yao kama watu wengine..
 
Mkuu umekuwa unatumia humu neno "utamaduni" ila sielewi huo utamaduni unaouzungumzia ni upi?

Hebu tueleze ni utamaduni gani unaouzungumzia ambao unasema unatakiwa ufuatwe? au unataka kusema waingereza wana aina zao maalumu za mavazi(kama wamasai) ambazo ndio utamaduni wao?

Sio wa Mwingereza, wa Muarabu.

Utamaduni wa Muarabu, wa mavazi au wa chochote .

Unaenda Uingereza unasema mimi ni Mhangaza wa Karagwe, utamaduni wetu tunaoa wake saba, nataka Uingereza isiingilie uhuru wa utamaduni wangu. Such height of ingratitude and absurdity.

Well, kama utamaduni wako ni muhimu sana, kama ni lazima uoe, ulale, uzae na wanawake wanne, saba, hapa hatuna huo ustaarabu, NENDA KWENU!

Baibui na halua ni muhimu sana kwako, kwa dini yako, nenda kaombe makazi ISLAMIC REPUBLIC OF IRAN!

Unaona Irani mbali, okay, HAMIA ZANZIBAR!

Lakini Zanzibar third world, kuna njaa, unataka kuishi kwa wazungu ule vizuri, ukishashiba ndio unakumbuka dini na utamaduni. Baniani mbaya kiatu chake dawa.
 
Nimekuuliza ni utamaduni gani hapo uingereza ambao unapingana na uvaaji wa hijab? halafu sijui kwanini unazungumzia wahamiaji tu wakati kuna wanawake waingereza wengi tu huingia kwenye uislamu,sasa hawa nao wakivaa hijab wanakuwa wameenda kinyume na utamaduni wao upi?
 
London ni multiculturalism
Kuna kila aina ya watu kuna sehemu utakuta sehemu kubwa ina wayahudi na wanaheshimiwa vazi lao bila bughudha tena wao jumamosi they don't operate anything kwa hiyo hata kubonyeza kwenye mataa ya kukatisha watu huwa hawagusi jumamosi badala yake anakuwepo police au warden kusimamisha magari wanapotaka kukatisha
Hebu fikiria kitu kama hiki hapo ndio utajua kuna uhuru wa kuamini unachokiamini.
Maadam huvunji sheria

Ukipita maeneo ya Oxford street au Knightsbridge ambapo kuna Harrods utakuta waarabu wamejiachia na baadhi wamevaa ninja.
Kuna utajiri wa hali ya juu maeneo hayo ambapo wamewekeza haswa na kufanya transformation ya hali ya juu yaani ile London ya zamani imebadilika kabisa kwa hela za hao boris anaowatukana

Likija suala la biashara watawaomba wanunue kila kitu kwao na leo maeneo mengi yanamilikiwa na waarabu tangu wakati wa recession
Boris hawezi kubadilisha kitu kwani kuna uhuru wa kila kitu maadamu huvunji sheria full stop
 
Nimekuuliza ni utamaduni gani hapo uingereza ambao unapingana na uvaaji wa hijab? halafu sijui kwanini unazungumzia wahamiaji tu wakati kuna wanawake waingereza wengi tu huingia kwenye uislamu,sasa hawa nao wakivaa hijab wanakuwa wameenda kinyume na utamaduni wao upi?

Hulka na mazoea ya watu wa Magharibi wa kutaka kuonana macho kwa macho, kusomana facial expression pia watu kuweza kukutambua wewe ni nani unapokuwa kwenye public space, yote haya yanapingana na utamaduni wa mwarabu wa kujifunika mashuka gubigubi hadharani.

Wao wamezoea kuona wanaovaa masks ni wavamizi wa benki, sasa ukivaa burka au niqab tunashindwa kukutambua kama ni jambazi au ni vipi, hawana utamaduni huo.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kupitia Jeshi la Polisi la Tanzania, walipiga marufuku uvaaji wa baibui za kujifunika gubigubi kwa wanaoendesha magari.
 
nionyeshe ambapo hao BBC wameandika "Boris Johnson awakashifu wanawake wavaa Hijab"
Tumia akili uliyopewa na Mungu bila kumlipa chochote!

Hivi Mr. X akisema Taso amefanana na nguruwe; halafu gazeti likaandika "Mr. X amesema Taso amefanana na nguruwe"; ina maana kwa akili yako ni kwamba hapo X hajakukashifu kwa sababu tu gazeti halijaandika "Mr. X amkashifu Taso...." Kumbe hoja yako ni huko kukosekana kwa Keyword "kashifu...!"

Too low!!!
 
Hulka na mazoea ya watu wa Magharibi wa kutaka kuonana macho kwa macho, kusomana facial expression pia watu kuweza kukutambua wewe ni nani unapokuwa kwenye public space, yote haya yanapingana na utamaduni wa mwarabu wa kujifunika mashuka gubigubi hadharani.

Wao wamezoea kuona wanaovaa masks ni wavamizi wa benki, sasa ukivaa burka au niqab tunashindwa kukutambua kama ni jambazi au ni vipi, hawana utamaduni huo.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kupitia Jeshi la Polisi la Tanzania, walipiga marufuku uvaaji wa baibui za kujifunika gubigubi kwa wanaoendesha magari.
Hoja ya hovyo kabisa hii!!!

Ndugu; hoja ni kwamba Borisi amesema wanaovaa burka wanaonekana kama masanduku ya barua au waporaji wa benki!!

That has nothing to do na huo utamaduni wa Magharibu unaosema as if unaufahamu peke yako!!

Hakuna ambae angepingana na Boris endapo hoja yake ingekuwa ni kupinga uvaaji wa burka kwa sababu hilo ni jambo la kawaida! Asingekuwa wa kwanza kupinga kwa sababu wapo hata Waislamu wanaopinga uvaaji wa burka!!!

Kinyume chake, ni ile kuwafananisha wavaa burka na bank robberies au masanduku ya barua!!
 
Mzee baba... hivi mvaa hijab kutaka uvaaji wake wa hijab kuheshimiwa ni kulazimisha ufuatwe?

mtu kavaa kaambiwa anafanana na jambo fulani kalazimisha.

mmasai kuvaa shuka New York then akatukanwa kwa kuvaa shuka kalazimisha New York nao wavae? sijui hata sikuelewi
Mzee baba....msimu wa mfungo Zanzibar na nchi nyingine za kiislam migahawa ufungwa,hakuna kura,kunywa wala kudance hadharani,wasio waislam ufuata bila kinyongo sababu wanajua na kuheshimu mila na tamaduni za kiislam na wala hawathubutu kuvunja wala kulazimisha. They believe ule usemi wa 'While in Rome do what the Romans do"
 
Tumia akili uliyopewa na Mungu bila kumlipa chochote!
tumia akili ya kuto assume kwamba kila mtu anaamini kuna Mungu anaegawa akili...

At least umeelewa kwamba BBC haijasema, haiwezi kusema, Johnson awakashifu wavaa Burka
 
okay thanks a bunch, sasa kwamba hiyo ni kashfa kwa wavaa hijab ni mawazo yako wewe! Hakuna mahala rasmi pameandikwa Boris Johnson awakashifu wavaa hijab. Kwa sababu hawakubaliani Waingereza wote kwamba hijab ni njema, wapo wanaomtetea Boris Johnson.

tamaduni za Magharibi ni tofauti na utamaduni wa waarabu, tusilazimishe kuwamezesha kooni matamaduni ya kigeni wenyeji wanapotukaribisha tuishi kwao.

hakuna mahala Quran Takatifu imeongelea kuvaa hijab, niqab wala burka

in fact, hakuna mahala popote kwenye Quran Takatifu pameongelewa uvaaji wa Muislam period.

kwa hiyo ukiona mtu Kariakoo kavaa suruali ya dont-tachi na barakashia na kanzu, huo sio uislam, ni ma-utamaduni ya Uarabuni tumeyabuguia jumla. On the other hand huwezi kwa miaka milioni kukuta muarabu kavaa kitenge cha Mswahili au lubega la Mmasai...

facial expression, eye contact and positive identification of who the hell you are in public space are time-honored values of the western culture...

Hijab, Niqab, Burka zimepigwa marufuku Morocco, Cameroon, Chad, Republic of the Congo, Gabon, Austria, Denmark, France, Belgium, Tajikistan, Latvia, Netherlands pamoja na China
hijab haijawahi kupigwa marufuku nchi yoyote ile..labd niqab au burka
 
But guys let's be realistic here, mtu anakuja let say dukani au ofisini kwako humjui na kajifunika mwili mzima na hii dunia ya kujiripua, ni salama kweli?
Kama hupendi jifungie chumbani kwako hautawaona....Au jinyonge lakini hawataacha kuvaa
 
Mzee baba....msimu wa mfungo Zanzibar na nchi nyingine za kiislam migahawa ufungwa,hakuna kura,kunywa wala kudance hadharani,wasio waislam ufuata bila kinyongo sababu wanajua na kuheshimu mila na tamaduni za kiislam na wala hawathubutu kuvunja wala kulazimisha. They believe ule usemi wa 'While in Rome do what the Romans do"
Hayo ya Zanzibar ni taratibu zao wao kama Zanzibar na ndiyo maana huku bara wasio waislamu hula mchana Wa ramadhani kama kawaida.
 
Hulka na mazoea ya watu wa Magharibi wa kutaka kuonana macho kwa macho, kusomana facial expression pia watu kuweza kukutambua wewe ni nani unapokuwa kwenye public space, yote haya yanapingana na utamaduni wa mwarabu wa kujifunika mashuka gubigubi hadharani.

Wao wamezoea kuona wanaovaa masks ni wavamizi wa benki, sasa ukivaa burka au niqab tunashindwa kukutambua kama ni jambazi au ni vipi, hawana utamaduni huo.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kupitia Jeshi la Polisi la Tanzania, walipiga marufuku uvaaji wa baibui za kujifunika gubigubi kwa wanaoendesha magari.
Kwanza mkuu mie nazungumzia hijab,sasa hayo ya kufunika uso sio nayozungumzia.
 
BURKA na NIQAB ndio subject matter ya Boris Johnson alyesema zinakufanya unakuwa kaa mvamia benki.

Kwa kule lakini, sio hapa kwetu. Majambazi wa Ulaya ndio wanavaa kininja, kwa hiyo jamii ikiona Burka na Niqab inaleta taharuki, hawajazoea.
 
Basi tulikuwa hatujaelewana toka mwanzo.

OK sawa kumbe kuvaa kininja ni tamaduni zao huko ulaya kwa ajiri ya ujambazi na ndiyo maana hali hiyo imewathiri kwa kudhani kila avae ninja ni jambazi kama walivyowazoea majambzi wao huko.

Basi mie nilidhani inapingwa hijab.
 
Imani gani, ya kipagani?

Quran Takatifu haijasema popote wanawake wavae hijab, niqab wala burka

In fact, Quran Takatifu haijasema lolote kuhusu uvaaji wa muislam wa namna yeyote.

Unaweza kuvaa ki-mini na ukawa hujavunja matakwa ya Quran Takatifu.

Kwa hiyo let us not conflate imani na utamaduni

Utamaduni wa Muingereza haukubaliani na kumfunika mwanamke gubigubi. Kwa wao, burka wanaliona kwa waporaji mabenki.
USIPOTEZE WATU KWA KUJIFANYA UNACHAMBUA QUR-AAN TUKUFU WAKATI HUJUI KITU. UNAWEZAJE KUSEMA MTU ATAKAEVAA KIMINI HAJAENDA KINYUME NA QUR-AAN WAKATI QUR-AAN IMEELEKEZA WANAWAKE KUSHUSHA JILBAAN ZAO???!!! TAMBUA KUUMIZA IMANI ZA WATU WENGINE NI KOSA KIKATIBA.
 
Back
Top Bottom