Boris Johnson akashifu wanawake wavaa hijab


ebwana weee ndio umeongea. hutaki rudi kwenu kwani unalazimishwa kwenda kuishi uingereza. kila nchi ina haki yakuwaambia wageni nini wafanye na nini wasifanye. simple.
 
Ningependa Malcom Lumumba na chige waione respond hii yako.
 
Wanasemaga jambo usilokua na elimu nalo usiliongelee.
 
Mtu ka Boris Johnson anawakilisha mawazo ya wanasiasa wengi wa chama chake kuanzia Waziri mkuu mwenyewe sema kinafiki wanajifanya wanampinga.
 
Sikuelewi hata.....
 
Mbona jamaa yuko sawa tu,Waisilamu bana,ulaya mbali sana hata hapa bongo, mtu akija kwako,sio yeye akupangie ufanye nini bali anatakiwa kufata taratibu za familia yako,kama saa moja wote mnatakiwa kuwa nyumbani inatakiwa iwe hivyo na si vinginevyo,hutaki nenda kwako,kuanzia kubishana na mwenye mji ati kisa imani yako wakati ni kinyume na utamaduni wake ni kukosa akili tu,mbona wengine tunavaa kanzu ingawa sio imani yetu sababu tu usimkwaze mwenyeji wako,hii dunia yetu nikubwa kuna watu huu ukristo au uisilamu hawaujui kabisa usipokubadili kubadilika utapata tabu sana ni bora ukae hapo ulipo tu
 
Wewe ni mwerevu.
 
Mkuu Consigliere,

Nimesoma posts mbalimbali za huyu Taso, nimeshindwa kufahamu hata anachomaanisha au anachokataa hasa ni nini hasa!! Ajabu zaidi, ni kama anataka kutuambia kwamba hata media kama BBC na zenyewe zimeandika uongo kuhusu kauli ya Boris!
 
when in rome do as romans.., hizi cultural differences kwenye nchi za watu ndio zinalleta resentment, ukiamua kuamia kwa watu basi atleast assimilate
 
Anaweza Kashifu anavyotaka coz sio dini yake na ana chuki ya asili ambayo iko ndani ya mioyo ya majority ya wale ambao sio waislam ila kwa ushauri tu hao wanawake pamoja na waislam wote wampotezee tu yani wasimpe kiki sababu hana madhara yeyote ni kiumbe mdogo mno hawezi utikisa uislam
 
But guys let's be realistic here, mtu anakuja let say dukani au ofisini kwako humjui na kajifunika mwili mzima na hii dunia ya kujiripua, ni salama kweli?
 
And BTW Kwanini waislam ulazimisha tamaduni zao kufuatwa hata kwenye nchi zisizo za kiislam /kidini ilhali wanaokwenda kwao uheshimu mila na desturi za huko?
 
Mkuu ...Ajabu zaidi, ni kama anataka kutuambia kwamba hata media kama BBC na zenyewe zimeandika uongo kuhusu kauli ya Boris!

nionyeshe ambapo hao BBC wameandika "Boris Johnson awakashifu wanawake wavaa Hijab"
 
Mkuu umekuwa unatumia humu neno "utamaduni" ila sielewi huo utamaduni unaouzungumzia ni upi?

Hebu tueleze ni utamaduni gani unaouzungumzia ambao unasema unatakiwa ufuatwe? au unataka kusema waingereza wana aina zao maalumu za mavazi(kama wamasai) ambazo ndio utamaduni wao?
 
And BTW Kwanini waislam ulazimisha tamaduni zao kufuatwa hata kwenye nchi zisizo za kiislam /kidini ilhali wanaokwenda kwao uheshimu mila na desturi za huko?
Kwahiyo hayo mavazi wanayovaa wanawake wa kiislamu ni kinyume na tamaduni za waingereza? hebu tuambie huo utamaduni wa waingereza ni upi ambao ndio ni kinyume na mavazi ya wanawake wa kiislamu?

Mi najua wamasai wana mavazi yao na ndio utamaduni wao,je hao waingereza mavazi ya utamaduni wao ni upi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…