Chaliifrancisco
JF-Expert Member
- Jan 17, 2015
- 23,528
- 70,390
Mkuu nipe connection nioe Tanga.Depends unaoa nani na kwa sababu gani
Mkuu nipe connection nioe Tanga.Depends unaoa nani na kwa sababu gani
Ndugu usioe Tanga,Mimi ninakuambia,BORA NIKAOE TANGA
Bora nikaoe Tanga, tena binti wa Pangani,
Yule anovaa kanga, na mitandio kichwani,
Aongea kwa kuringa, na lafudhi ya kipwani,
Awe na kauli njema, kwangu na kwa ikhwani.
Pangani nikimkosa, natafuta wa Handeni,
Niweze peleka posa, nioe niweke ndani,
Naenda haraka hasa, nisichelewe njiani,
Nitampenda kwa dhati, upendo toka moyoni.
Au nishuke Muheza, nikamsake mwandani,
Apate kuniliwaza, na uchovu wa kazini,
Najua hatanikwaza, kuniumiza moyoni,
Niliwazwe hasahasa, ili niwe wa thamani.
Au awe wa Lushoto, tena kule milimani,
Alozoea msoto, kupanda kushuka chini,
Azijua changamoto, zilizopo maishani,
Siku nikisema sina, asiende kwa jirani.
Au niende Korogwe, nimpate wa ubani,
Mchuzi atie ngogwe, nyanya chungu za mjini,
Nisemwe au nirogwe, sisikii na sioni,
Nitalia kwa makeke, akimtwaa fulani.
Wa Kilindi simpiti, na yeye namthamini,
Aweze kunidhibiti, ili nisitoke ndani,
Masham matashtiti, kwa udi pia ubani,
Katu asinisaliti, nikiwa na hali duni.
Ndugu zangu wa Mkinga, naomba nipokeeni,
Nakuja kutia nanga, nimsake wa moyoni.
Asiwe wa kujivunga, aishike sana dini,
Sio kama nabagua, natafuta mke mwema.
Au nibakie Tanga, nioe pale mjini,
Walipojaa nyakanga, wafundao wari ndani,
Panauzwa hadi shanga, sijui za kazi gani,
Kama nyumba nitajenga, hata kule mikanjuni.
Hapa sasa naishia, mawazo tele kichwani,
Wapi nitajipatia, mke yule mwenye shani,
Nipate kufurahia, raha ya ndoa ndoani,
Ila atokee Tanga, mjini au wilayani.
Noma sana kweli ushairi wa kiswahili utaishi mileleNdugu usioe Tanga,Mimi ninakuambia,
Hao watu wanaringa, Kisa tu kuwasifia,
Sio kwamba nakupinga, ukweli nakuambia,
Bora uje kwetu Njombe,kuna Wanawake wema,
Uje uoe mkinga,mpangwa au Mbena,
Maisha mtayapanga,na kufanikiwa sana,
Uchumi mtaujenga, tena pasipo hiana,
Heko Mabinti wa Njombe,Kwa tabia yenu njema,
Mkuu upo vizuri, Dada zako wakibena nawaelewa sana, wanajua kupenda.Ndugu usioe Tanga,Mimi ninakuambia,
Hao watu wanaringa, Kisa tu kuwasifia,
Sio kwamba nakupinga, ukweli nakuambia,
Bora uje kwetu Njombe,kuna Wanawake wema,
Uje uoe mkinga,mpangwa au Mbena,
Maisha mtayapanga,na kufanikiwa sana,
Uchumi mtaujenga, tena pasipo hiana,
Heko Mabinti wa Njombe,Kwa tabia yenu njema,
Karibu Tanga...BORA NIKAOE TANGA
Bora nikaoe Tanga, tena binti wa Pangani,
Yule anovaa kanga, na mitandio kichwani,
Aongea kwa kuringa, na lafudhi ya kipwani,
Awe na kauli njema, kwangu na kwa ikhwani.
Pangani nikimkosa, natafuta wa Handeni,
Niweze peleka posa, nioe niweke ndani,
Naenda haraka hasa, nisichelewe njiani,
Nitampenda kwa dhati, upendo toka moyoni.
Au nishuke Muheza, nikamsake mwandani,
Apate kuniliwaza, na uchovu wa kazini,
Najua hatanikwaza, kuniumiza moyoni,
Niliwazwe hasahasa, ili niwe wa thamani.
Au awe wa Lushoto, tena kule milimani,
Alozoea msoto, kupanda kushuka chini,
Azijua changamoto, zilizopo maishani,
Siku nikisema sina, asiende kwa jirani.
Au niende Korogwe, nimpate wa ubani,
Mchuzi atie ngogwe, nyanya chungu za mjini,
Nisemwe au nirogwe, sisikii na sioni,
Nitalia kwa makeke, akimtwaa fulani.
Wa Kilindi simpiti, na yeye namthamini,
Aweze kunidhibiti, ili nisitoke ndani,
Masham matashtiti, kwa udi pia ubani,
Katu asinisaliti, nikiwa na hali duni.
Ndugu zangu wa Mkinga, naomba nipokeeni,
Nakuja kutia nanga, nimsake wa moyoni.
Asiwe wa kujivunga, aishike sana dini,
Sio kama nabagua, natafuta mke mwema.
Au nibakie Tanga, nioe pale mjini,
Walipojaa nyakanga, wafundao wari ndani,
Panauzwa hadi shanga, sijui za kazi gani,
Kama nyumba nitajenga, hata kule mikanjuni.
Hapa sasa naishia, mawazo tele kichwani,
Wapi nitajipatia, mke yule mwenye shani,
Nipate kufurahia, raha ya ndoa ndoani,
Ila atokee Tanga, mjini au wilayani.
Amen.Nilianza kupenda utunzi wa mashairi tangu nikiwa mdogo kabisa.Noma sana kweli ushairi wa kiswahili utaishi milele
Ndugu nakukaribisha, Njombe kwetu maskani,Mkuu upo vizuri, Dada zako wakibena nawaelewa sana, wanajua kupenda.
Watamu haoWanawake wa kitanga ni aina ya wanawake wenye kukidhi vigezo vizuri vya wastani vinavyopendwa na wanaume wengi.
Mwanamke wa kitanga;
-anajua kumsikiliza Mwanaume
Hakosi kuwa na adabu na heshima kwa Mwanaume
Umaridadi na usafi ni hadhi zao
Anajua kupika
Anajua huba
Anajua kumsitiri Mwanaume
Anajua mambo ya kitandani.
Anajua ukarimu kwa ndugu wa mume na
majirani.
Anaelewa lugha ya kuluzu
N.k.
Swadakta kabisa Shadeeya. Tanga ni njema atakae na aje. Mahaba shatashata WallahMaajabu. Yaani leo wote mnaongea lugha moja kwa huu uzi juu ya wanawake wa Tanga. Lol
Haya muwe na kila la kheri.
#Wajaleokuondokamajaliwa.
Cc. Sesten Zakazaka
Kwa kweeli.Swadakta kabisa Shadeeya. Tanga ni njema atakae na aje. Mahaba shatashata Wallah
Nimewahi kuwa na experience isiyofutika na mtoto wa Kitanga.Maajabu. Yaani leo wote mnaongea lugha moja kwa huu uzi juu ya wanawake wa Tanga. Lol
Haya muwe na kila la kheri.
#Wajaleokuondokamajaliwa.
Cc. Sesten Zakazaka
Hongera zako Mtani. Huwa naonaga wanakandia tu lakini leo kila mmoja anasema mleta uzi aende akaoe Tanga.Nimewahi kuwa na experience isiyofutika na mtoto wa Kitanga.
Aligoma kubadili diniHongera zako Mtani. Huwa naonaga wanakandia tu lakini leo kila mmoja anasema mleta uzi aende akaoe Tanga.
Vipi lakini ulimuweka ndani?
Duuh!! Hivyo imebakia story tu Mtani.Aligoma kubadili dini