Bora nikaoe Tanga

poleni

JF-Expert Member
Mar 9, 2013
229
1,000
Bora nikaoe Tanga, tena binti wa Pangani,
Yule anovaa kanga, na mitandio kichwani,
Aongee kwa kuringa, na lafudhi ya kipwani,
Awe na kauli njema, kwangu na kwa ikhwani.

Pangani nikimkosa, natafuta wa Handeni,
Niweze peleka posa, nioe niweke ndani,
Naenda haraka hasa, nisichelewe njiani,
Nitampenda kwa dhati, upendo kutoka moyoni.

Au nishuke Muheza, nikamsake mwandani,
Apate kuniliwaza, na uchovu wa kazini,
Najua hatanikwaza, kuniumiza moyoni,
Niliwazwe hasahasa, ili niwe wa thamani.

Au awe wa Lushoto, tena kule mlimani,
Alozoea msoto, kupanda kushuka chini,
Azijua changamoto, zilizopo maishani,
Siku nikisema sina, asiende kwa jirani.

Au niende Korogwe, nimpate wa ubani,
Mchuzi atie ngogwe, nyanya chungu za mjini,
Nisemwe au nirogwe, sisikii na sioni,
Nitalia kwa makeke akimtwaa fulani.

Wakilindi simpiti, na yeye namthamini,
Aweze kunidhibiti, ili nisitoke ndani,
Masham matashtiti, kwa udi pia ubani,
Katu asinisaliti, nikiwa na hali duni.

Ndugu zangu wa Mkinga, naomba nipokeeni,
Nakuja kutia nanga, nimsake wa moyoni,
Asiwe wa kujivunga, aishike sana dini,
Sio kama nabagua, hiyo yangu tamaduni.

Au nibakie Tanga, nioe pale mjini,
Walipojaa nyakanga, wafundao wari ndani,
Panauzwa hadi shanga, sijui za kazi gani,
Kama nyumba nitajenga, hata kule Mikanjuni.

Hapa sasa naishia, mawazo tele kichwani,
Wapi nitajipatia, mke yule mwenye shani,
Nipate furahia, raha ya ndoa ndoani,
Ila atokee Tanga, mjini au wilayani.
 

KARANJA 007

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
6,011
2,000
Njoo lushoto wamezoea shda, kupanda na kushka milima kila siku!
Daaah,umemaliza aisee,hasa uliposema wamezoea shida,kupanda na kushuka mlima kila siku,loooh afanareeeek mjomba hiyo kupanda nakushuka ndio subiani yenyewe,yaani mpaka asali unaisikilizia kisogoni,ukiila lazima ushuke ngomani nauicheze huku ukila taaabani,ila kumbuka taabani ni jini subiani,mimi malenga wa Mrima naangusha kalamu ili iangukie Ngamiani.
 

madhabaunyeusinyeusi

JF-Expert Member
Dec 31, 2016
200
225
Kaka tambua tanga kunani ukioa uko utfaidi Shekhe wangu mi nimechukua uko full mahabati Mkuu afu wana mtindo Wa kudeka ila sio wote waweza wja Leo na warudi Leo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom