Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
Meya wa zamani wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob kupitia ukurasa wake wa Twitter ametoa malalamiko yake akidai Serikali inacheza mchezo wa Kimafia kuhusiana na kesi ya Rufaa ya Wabunge 19 walifukuzwa uanachama CHADEMA ila bado wakiendelee kuingia Bungeni.
Ameandika “Serikali inacheza Mchezo wa Kimafia sana. Tumetuma Mawakili Mahakama Kuu, pale Ofisini Kwa Msajili Wa Mahakama Wakakama Hakuna Kesi ya Kina Mdee. Mawakili wetu wakajifanya Wameondoka Kumbe wamejificha. Wamekuta Saa 8:00 Kesi ya kina Mdee Inasikilizwa Kwa Jaji Mgeta Kimya Kimya”
Katika tweet nyingine iliyofuata, akaandika “CHADEMA wala Mawakili wa CHADEMA hawajapewa Summons ya Mahakama Kuhusu Kesi ya Kina Mdee inayosemekena Kufunguliwa Siku Nne nyuma. Masijala ya Mahakama Wanasema hawaijui. Kumbe Walipanga isikikizwe Upande Mmoja Kimya Kimya,Mchana huu. Mungu Mkubwa Adv Malya ameingia ndani tayari“
Ameongeza “Wakili Peter Kibatala na Wakili John Malya tayari wapo ndani ya Chumba Cha Mahakama Mbele ya Jaji Mgeta 😂😂😂😂😂. Hawakujua sisi Wahuni pia Kuliko wao, Mahakama Kuu ilikuwa na Makachero wa Chama tangu Saa 1 Asubuhi. Mikakati ya Kusikilizwa Kesi Upande Moja bila CHADEMA imefeli“