Mdee na Wabunge wenzake 18 kuchuana na CHADEMA leo tena Mahakamani

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Kesi Kesi hiyo leo inatarajiwa kuendelea tena baada ya kusimama kwa miezi miwili, tangu Mei 17, mwaka huu. Siku hiyo kesi hiyo haikuendelea Kwa kuwa Jaji Cyprian Mkeha anayeiskilizwa hakuwepo, kwani alikuwa kwenye semina ya majaji ndipo ikapangwa kuendelea leo.

Wabunge hao akiwemo Halima Mdee ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), na wenzake 18 wamefungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama, kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama (Judicial Review).

Kwa sasa kesi hiyo iko katika hatua ya mahojiano baina ya mawakili wa kina Mdee, Ipilinga Panya, Aliko Mwamanenge, Edson Kilatu na Emmanuel Ukashu na wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Chadema.

Pamoja na mambo mengine mahojiano hayo yanahusiana na uhalali wa utaratibu uliotumika kuwavua uanachama kina Mdee.

Tayari mawakili hao wameshamhojj mmoja wa wajumbe hao, Dk. Azavery Lwaitama. Wengine wanaotarajiwa kuhojiwa ni, Silivester Masinde, Ruth Mollel, Mary Florian Joachim, Francis Joseph Mush, Maulida Anna Komu na Ahmed Rashid Hamis.

Awali, jopo la mawakili wa Chadema linaloongozwa na Wakili Peter Kibatala liliiomba mahakama ikaelekeza Mdee na wenzake Saba kati ya hao 19, wafike mahakamani ili kuwahoji kuhusiana na ushahidi wao walioutoa katika kiapo chao.

Mbali na Mdee, wengine walioitwa walikuwa ni Nusrati Hanje, Ester Matiko, Ester Bulaya, Grace Tendega, Jesca Kishoa, Cecilia Pareso na Hawa Mwaifunga..

Hata hivyo mawakili wa Chadema waliamua kufunga mahojiano bila kuwahojj Mdee Bulaya na Matiko licha ya kuitwa.

Katika kesi hiyo wanapinga uamuzi wa Baraza Kuu la Chadema kutupilia mbali rufaa zao za kupinga uamuzi wa Kamati Kuu kuwafukuza uanachama kwa tuhuma za kuapishwa kuwa wabunge bila ridhaa ya Chama.

Kamati Kuu iliwavua uanachama wa Chama hicho Novemba 27, 2020. Walikata rufaa Baraza Kuu kupinga uamuzi huo wa Kamati Kuu lakini Baraza Kuu katika uamuzi wake wa Mei 11, 2022, kulitupilia mbali rufaa yao hiyo.

Baada ya uamuzi huo wa Baraza Kuu kutupilia mbali rufaa yao, ndipo wakakimbilia mahakamani ambako kwanza waliomba na wakapata kibali kufungua shauri hili.

Wanapinga uamuzi wa Baraza Kuu pamoja na mambo mengine wakidai kuwa hawakupewa haki ya kusikilizwa, ambayo ni haki ya msingi.

MWANANCHI
 
Kesi Kesi hiyo leo inatarajiwa kuendelea tena baada ya kusimama kwa miezi miwili, tangu Mei 17, mwaka huu. Siku hiyo kesi hiyo haikuendelea Kwa kuwa Jaji Cyprian Mkeha anayeiskilizwa hakuwepo, kwani alikuwa kwenye semina ya majaji ndipo

MWANANCHI
Wawafukuze bungeni hao COVID Ili tufurahie tusahau mjadala wa bandari.
 
Yale ya Rostam kuhusu mahakama yanaendelea..

Jaji Ramadhani amaewahi kusema "Mnyonge kupata haki, ni mwenye nguvu kupenda" CCM wanawataka COVID hooks and crooks.

CDM ingeachana nao tu, technically ni kama umebak mwaka 1 tu..

Na CCM inawahitaji sana kwa ajili ya kuombea loan... yani ni kama collateral flani hivi....
 
Kesi Kesi hiyo leo inatarajiwa kuendelea tena baada ya kusimama kwa miezi miwili, tangu Mei 17, mwaka huu. Siku hiyo kesi hiyo haikuendelea Kwa kuwa Jaji Cyprian Mkeha anayeiskilizwa hakuwepo, kwani alikuwa kwenye semina ya majaji ndipo ikapangwa kuendelea leo.


MWANANCHI
Siri ya hiyo kesi aijuaye ni Mbowe na Mnyika!
 
Back
Top Bottom