Bondia Mandonga adhibitiwe kauli zake za kihuni zisije kuchafua Mchezo wa Ngumi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,636
108,992
"Nimepigwa na huyu Bondia Golola kwakuwa nimegundua ni Mganga wa Kienyeji, kwani nilikuwa naona mauzauza tupu ulingoni. Leo mnaniletea Mganga wa Kienyeji ipo siku mtaniletea hata majini ili kupigana nami sitaki jamani." Amesema Bondia Mandonga jana baada ya kupigwa kwa KO na Bondia Fundi Moses Golola kutoka nchini Uganda.

GENTAMYCINE huko nyuma (hapa hapa JamiiForums) niliwahi kuonya kuwa hii tabia ya Bondia Mandonga kupigana kila wiki Kinyume na utaratibu, kuna siku ama atapigwa vibaya au hata kufia ulingoni. Kama kawaida Mfalme wa Maono mimi sikueleweka ila taratibu naanza kukiona kwa mbali kile ambacho nilikiona (nilikitabiri) kinaenda kutokea.

Halafu nimejiuliza sana, hivi hawa Waandishi wa Habari wanaopenda kumhoji huyu Bondia muhuni na wa Hovyo Karim Mandonga ni Professionals na wamepita Vyuoni kweli?

Hii kauli yake ya kihuni na isiyo ya Kimchezo ambayo inaweza pia kudhoofisha juhudi za kuuridisha katika kiwango chake Mchezo wa Ndondi ilipaswa kupelekwa hewani au hata tu kupewa kipaumbele kwa Afya ya Mchezo?

Endeleeni tu kumlea hovyo Mandonga huku mkionyesha kupenda kauli zake za uvutaji wa bangi/bange zilizomuathiri ubongo kisha augharimu na mchezo wenyewe.
 
"Nimepigwa na huyu Bondia Golola kwakuwa nimegundua ni Mganga wa Kienyeji kwani nilikuwa naona mauzauza tupu Ulingoni. Leo mnaniletea Mganga wa Kienyeji ipo Siku mtaniletea hata Majini ili Kupigana nami sitaki Jamani" amesema Bondia Mandonga jana baada ya Kupigwa kwa KO na Bondia Fundi Moses Golola kutoka nchini Uganda.

GENTAMYCINE huko nyuma ( hapa hapa JamiiForums ) niliwahi Kuonya kuwa hii tabia ya Bondia Mandonga kupigana kila Wiki Kinyume na Utaratibu kuna Siku ama atapigwa vibaya au hata Kufia Uwanjani kama kawaida Mfalme wa Maono Mimi sikueleweka ila taratibu naanza kukiona kwa mbali kile ambacho nilikiona ( nilikitabiri ) kinaenda Kutokea.

Halafu nimejiuliza sana hivi hawa Waandishi wa Habari wanaopenda Kumhoji huyu Bondia Muhuni na wa Hovyo Karim Mandonga ni Professionals na wamepita Vyuoni Kweli?

Hii Kauli yake ya Kihuni na isiyo ya Kimchezo ambayo inaweza pia Kudhoofisha juhudi za Kuuridisha katika Kiwango chake Mchezo wa Ndondi ilipaswa kupelekwa Hewani au hata tu kupewa Kipaumbele kwa Afya ya Mchezo?

Endeleeni tu Kumlea hovyo Mandonga huku mkionyesha kupenda Kauli zake za Uvutaji wa Bangi / Bange zilizomuathiri Ubongo kisha augharimu na Mchezo Wenyewe.
Usilalamike sana. Ngumi ndio zilivyo.

Kusema hovyo ni sehemu ya mchezo, ndio zinazonogesha hasa mchezo wenyewe wa ndondi.

Ndio maana, Mandonga anakua maarufu kwa maneno yake ya shombo
 
"Nimepigwa na huyu Bondia Golola kwakuwa nimegundua ni Mganga wa Kienyeji kwani nilikuwa naona mauzauza tupu Ulingoni. Leo mnaniletea Mganga wa Kienyeji ipo Siku mtaniletea hata Majini ili Kupigana nami sitaki Jamani" amesema Bondia Mandonga jana baada ya Kupigwa kwa KO na Bondia Fundi Moses Golola kutoka nchini Uganda.

GENTAMYCINE huko nyuma ( hapa hapa JamiiForums ) niliwahi Kuonya kuwa hii tabia ya Bondia Mandonga kupigana kila Wiki Kinyume na Utaratibu kuna Siku ama atapigwa vibaya au hata Kufia Uwanjani kama kawaida Mfalme wa Maono Mimi sikueleweka ila taratibu naanza kukiona kwa mbali kile ambacho nilikiona ( nilikitabiri ) kinaenda Kutokea.

Halafu nimejiuliza sana hivi hawa Waandishi wa Habari wanaopenda Kumhoji huyu Bondia Muhuni na wa Hovyo Karim Mandonga ni Professionals na wamepita Vyuoni Kweli?

Hii Kauli yake ya Kihuni na isiyo ya Kimchezo ambayo inaweza pia Kudhoofisha juhudi za Kuuridisha katika Kiwango chake Mchezo wa Ndondi ilipaswa kupelekwa Hewani au hata tu kupewa Kipaumbele kwa Afya ya Mchezo?

Endeleeni tu Kumlea hovyo Mandonga huku mkionyesha kupenda Kauli zake za Uvutaji wa Bangi / Bange zilizomuathiri Ubongo kisha augharimu na Mchezo Wenyewe.
We kama huwezi waache wanaoweza,mwili wake maisha yake,kama vipi omba naye pambano tuone nani atawahi kwenda akhera...
 
Mandonga amekuwa famous si kwamba ni talented boxer sana kuzidi wengine hapa bongo ila ni kutokana na kujua kutumia trash talking ku-hype mapambano take kama ilivyokuwa kwa mabondia wengi wa zamani huko mbele mfano Muhammad Ally wakati anapigana na bondia ngumi jiwe Sonny Liston mwaka 1964..Ally alitoa trash talks balaa kiasi Cha kufanya Kila mtu kuwa na shauku kuona jinsi Gani bwana mdogo Ally, atakavyochezea ngumi nzito za Sonny Liston...!! Pambano lilijaza balaa na Muhammad Ally aliushangaza ulimwengu kwa kumtwanga Sonny.

Mabondia wengi wa bongo hawajui kutumia Tambo kiasi Cha kuvutia vyombo vya habari viwafuatilie. Waige mfano mzuri wa bondia Connor Mcgregory ambaye ana Tambo nyingi kiasi Cha kufanya apewe pambano dhidi ya Mayweather na kupelekea kupata pesa nyingi.

Boxing ni ngumi na Tambo.

Kumpa mapambano mawili mfululizo ndani ya wiki moja si sawa kabisa kwa afya ya bondia.
 
Mandonga kasema ukweli,
Kuna ngumi ukipigwa lazima mauzauza
Kama uliwai pigwa ngumi ya skio utathibtisha
Haya mambo yalianzia kwa Mada Maugo.Baada ya kupigwa na Fransis Cheka, alisema ule ulikuwa uchawi si kawaida. Mada Maugo aliongeza kuwa, ngumi alizopigwa ni aheri kupigwa na mawe siyo ngumi nzito namna hiyo, zaidi hizi ngumi zilikuwa zinaleta maruerue.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom