Bomu la Lowassa: Tumeligundua, Tunaliteguaje?

Mkuu Jasusi vipi ukahamia Unguja bado utaonekana mtanzania hasa baada ya tetesi upo uwezekano wa mafuta huko ?.Je hudhani hii sera ya majimbo [CDM] inaweza kupelekea mikoa ya Lindi na Mtwara kutamani kujitenga ?.

.
[/QUOTE]

Mkuu Ngongo,
Siwezi kuhamia Unguja wakati tuna Tanga. Sera ya majimbo haiwezi kupelekea Lindi na Mtwara kutamani kujitenga kwa sababu watawezeshwa ku-control maliasili zao kwa kutumia sehemu kubwa kwa maendeleo ya majimbo hayo na kuchangia pia kwenye keki ya taifa. Kwanza wajitenge waende wapi? Pia usisahau hakuna jimbo linaloweza kusimama peke yake bila kutegemeana na jirani.
 
Mchambuzi,

..Dr.Kaberuka wa ADB aliwahi kusema kwamba Afrika[Tanzania] kuna tatizo la "Urbanization without Industrialization."

..binafsi nadhani SERIKALI inapaswa kuanza ku-invest tena kwenye VIWANDA kwasababu WAWEKEZAJI wa ndani na nje peke yao wameshindwa kubeba jukumu la kufanikisha mapinduzi ya viwanda nchini.

..pia mazingira ya uwekezaji Tanzania yanapaswa kuboreshwa. matatizo ya umeme, maji, na miundombinu kama barabara, reli, na bandari, yanapaswa kuboreshwa haraka sana.

..kuhusu ELIMU naamini vijana wengi, hata wale waliofeli, wanaweza kabisa kuajiriwa kufanya kazi ktk assembly lines za viwanda kama vya nguo, ngozi, food processing, etc etc. kama viwanda vya China vinapeta with child labor, basi bila shaka viwanda vya Tanzania vinaweza kushamiri kwa nguvu kazi ya wahitimu wa sekondari za kata, mpaka hapo tutakaporekebisha mambo.

..pamoja na hayo lazima niongeze kwamba tunapaswa kuubadilisha MTAALA WETU WA ELIMU ili uweze kwenda na wakati, na uweze kukidhi malengo yetu ya kiuchumi na maendeleo ya muda mrefu. sasa maadamu tumeazimia kujenga taifa linalotegemea viwanda basi ELIMU YA UFUNDI inapaswa kutiliwa mkazo.



NB:

..majuzi nilikuwa naangalia program moja kuhusu matatizo ya uchumi wa USA. sasa wakawa wanaeleza kwamba kitendo cha serikali ya USA kuto-subsidize viwanda vya chuma ndicho kilichosababisha viwanda vya ujenzi wa meli za kibiashara kuhamia South Korea ambako serikali ya huko ilikuwa actively engaged kwa muda mrefu.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi, mie nina kaswali kadogo sana/au hoja

Hiyo ya 80% ya watanzania kutegemea kilimo kama ajira inanitatizza sana, maana kwa kuangalia juu-juu tu, urban population kwa sasa, jobless even in rural areas, nk

Data hizi ni za wapi?? isije ikawa kama zile za waislamu na wakristu

Takwimu hizi ni kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kama vile World Bank, UNDP, GOT n.k; Lakini pia zipo takwimu zinazo onyesha kiwango hiki kinashuka kwa kasi, na kuna makadirio kwamba pengine sasa ni kama 70% kwani kama unavyosema rural - urban migration katika kipindi cha miaka kumi iliyopita imekuwa kubwa sana, na watanzania wengi wanakimbia kilimo kwani hakilipi, na badala yake wanaingia into informal sector - hasa on services and trading;

Lakini ni muhimu tutofautishe kati ya percentage ya watanzania wanaoishi vijijini na percentage ya watanzania wanaotegemea kilimo, hivi ni vitu viwili tofauti kwani vijijini kuna jamii nyingine wao ni wafugaji n.k;

Percentage of watanzania wanaioshi vijijini inaangalia umri kuanzia 0-65+; In terms of watanzania wanaotegemea kilimo, kinachozungumziwa hapa ni labor force participation katika sekta mbalimbali, na ni kwenye age group kati ya 15 and 60 years of age; Mtoto chini ya miaka 15 haesabiwi kuwa sehemu ya labour force;
 
Tupe idadi kama hizo hizo za mwaka wowote kati ya 1961-1985 na za mwaka wowote kati ya mwaka 1986-1995 na za mwaka wowote kati ya 1996-2005. Tujiridhishe na uchambuzi wako.

Ukiweza kuziweka kama ulivyoziweka hizo hapo juu, ntakujuwa kweli umechambuwa, ukishindwa najuwa hizo ni porojo tu na hazina maana yoyote kwani hazina "comparison", nimeitaja hiyo miaka ya awamu tofauti za uongozi wa nchi hii.
 
Takwimu hizi ni kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kama vile World Bank, UNDP, GOT n.k; Lakini pia zipo takwimu zinazo onyesha kiwango hiki kinashuka kwa kasi, na kuna makadirio kwamba pengine sasa ni kama 70% kwani kama unavyosema rural - urban migration katika kipindi cha miaka kumi iliyopita imekuwa kubwa sana, na watanzania wengi wanakimbia kilimo kwani hakilipi, na badala yake wanaingia into informal sector - hasa on services and trading;

Lakini ni muhimu tutofautishe kati ya percentage ya watanzania wanaoishi vijijini na percentage ya watanzania wanaotegemea kilimo, hivi ni vitu viwili tofauti kwani vijijini kuna jamii nyingine wao ni wafugaji n.k;

Percentage of watanzania wanaioshi vijijini inaangalia umri kuanzia 0-65+; In terms of watanzania wanaotegemea kilimo, kinachozungumziwa hapa ni labor force participation katika sekta mbalimbali, na ni kwenye age group kati ya 15 and 60 years of age; Mtoto chini ya miaka 15 haesabiwi kuwa sehemu ya labour force;

Thanks mkuu, i was inclined to 70% kwa simple calculations

Janjaweed
 
Dotto,

Nashukuru sana kwa mchango wako;
Mimi naona kitu hapa katika hoja zako hapo juu:
Uwezo wa Viongozi- Hii hasa ni baada ya kushindwa katika ule mfumo wa ujamaa na tukiwa na viwanda vyetu. Baada ya huu mfumo mpya wa mixed Economy hatujapata uongozi imara unaoendana na mfumo huo. ZAidi sana wauza nchi.

Ni kweli; Tatizo kubwa tulilonalo hivi sana ni kwamba hatuna dira kama taifa juu ya wapi tunataka kwenda na tufikaje huko, hasa ni uchumi wa aina gani tunataka kuujenga kwani soko huria na ubepari sio tatizo, tatizo ni kujipanga kutumia fursa zinatozukuja na mfumo huo huku tukijipanga kupambana na mapungufu yanayoendana na mfumo huo;

Dira iliyopo sasa ni ile Vision 2025 ambayo ni copy and paste tu, and it is not home grown prepared and determined by the Washington Consensus (WorldBank, IMF, WTO); Hii ni tofauti na wakati wa Ujamaa kama taifa tulimiliki our ‘development agenda’ na tulikuwa katika nafasi ya kuamua vipaumbele n.k; Kama unakumbuka Mwalimu aliwahi kutamka kwamba kupanga ni kuchagua, na ali execute vizuri sana dhana hii na nchi yetu ilipaa sana kiuchumi katika kipindi cha 1970 – 1977; Nyakazi hizi, hata kupanga hatupangi, na mbaya zaidi, tunachaguliwa;

Sasa hivi hatuna ownership tena ya development agenda, kwani zilipoanza reforms wakati ule mzee Mtei alipotofautiana na Mwalimu kutokana na uchumi kuporomoka, World Bank na IMF took over under their Structural Adjustment Programmes ambazo essentially zililenga to stabilize uchumi HOI, kwa njia kama kuondokana na inefficiency State Owned Entreprises, kupunguza matumizi makubwa ya serikali, kulegeza masharti ya biashara ili bidhaa za nje zijae madukani kutokana na uhaba wa bidhaa kutoka kwenye viwanda vyetu vilivyoanza kufa, kulegeza masharti ya kifedha ili mitaji toka nje iweze ingia nakuamsha uchumi n.k; Tatizo ni kwamba hadi sasa tunategemea sana mitaji toka nje na mikopo toka kwa wahisani, hivyo ili kupata vyote hivi, ni lazima tutii masharti ya worldbank na IMF…, hasa juu ya uwekezaji, ubinaifishaji n.k;

Uchumi wetu hivi sasa unaendeshwa chini ya Kanuni ya Privatization, Liberalization & Marketization, ambapo serikali inatakiwa ikae pembeni na kuachia nguvu za soko zitawale uchumi, kwa imani kwamba hivyo ndivyo resources zitakuwa allocated kwa ufanisi kuliko serikali kuingilia huko na kufanya bad investments, white elephant projects n.k; Lakini kama tunavyoona, miaka 18 ya Ujamaa ilikuwa bora kwa ‘an average’ Tanzanian kuliko miaka 27 ya soko huria na ubepari;

Tunahitaji Dira Mpya, na tunahitaji kumiliki our development agenda, lakini sio kwa kuondokana na soko huria, bali kuja na itikadi na dira ambayo itapelekea uwepo wa uvumilivu baina ya Soko Huria na Welfare State; Ni muhimu serikali irudi kwenye usukani wa uchumi kwani hakuna uchumi duniani ulioendelea bila nguvu ya serikali; Lakini ili kufanikisha hilo, tunahitaji viongozi wa kweli; Kiitikadi mimi nina amini kwamba Ujamaa wa kidemokrasia ndio suluhisho kwani itasaidia kurudisha serikali katika uchumi, hasa kwenye maeneo ambayo soko limeshindwa kunufaisha walio wengi;

Mikataba ya kinyonyaji- Baada ya kushindwa katika viwanda na ujamaa wa wakati huo, kitu pekee tulichokuwa tumebaki nacho na ambacho awamu mbili za mwanzo hawakudhubutu kugusa ni madini rasilimali asili za nchi. Kama mikataba ingefungwa kwa nia njema ya uzalendo wa kiutu leo hii tusingekuwa tumeumia sana na hata hivyo viwanda vingefufuliwa kwa mtazamo mpya na siyo kuviuza kwa matapeli. Mfano. Mkataba wa Richmond.
Symbion ni kielelezo kwamba masuala haya ya ufisadi hata wakubwa wanayabariki kwani wakubwa wa nje wapo hapa kwa ajili ya mambo makuu matatu: Kwanza, kutukopesha kama njia ya kuzungusha their surplus izae huku pia wakitumia mikopo hiyo kuingia uhuru wetu wa kisera, hasa kiuchumi; Pili, kuwekeza kwenye miradi, hasa resource based kwani hiyo inarudisha fedha haraka; Na Tatu, kuhakikisha fedha wanazotukopa zinarudi kwao kwa njia ya manunuzi ya capital goods, kuanzisha miradi mikubwa kwa kushirikiana na serikali n.k, kwani hakuna biashara nzuri duniani kote kama ya kufanya na serikali; Na haya ndio ya symbioni;
Rushwa- Ni tatizo kubwa maana limeathiri hata katika mikataba mikubwa ambayo ingelinufaisha taifa( wananchi) na kupunguza matatizo ya uchumi. Rushwa hii imejikita kwa kuanzia na kununua uongozi na katika taasisi zote za kiserikali. Inawezekana kabisa kuna wawekezaji ambao wangekuja kuwekeza katika sekta ya viwanda hapa nchini na wameshindwa kufanya hivyo kwa sababu ya rushwa ambayo imejenga urasimu mkubwa. Kiongozi anayeingia kwenye uongozi kwa rushwa awezaondoa tatizo hili?? KAma mimi mwekezaji nilianza biashara yangu kwa rushwa je, naweza pia kulipa kodi??
Grand corruption ni ngumu kuimaliza Afrika, sana sana tunaweza kuipunguza tu vinginevyo chanzo chake ni ubepari uchwara na soko huria holela ambalo tumeliiga tu kutoka huko nje na kuja kulipandikiza kwenye jamii ambayo haikuwa imejipanga kitaasisi kuhusu masuala ya utawala wa sheria n.k; Ndio maana ilikuwa ni muhimu kwa wakubwa kuliua azimio la Arusha na kuleta azimio la Zanzibar, na kazi hii ilifanikiwa kwa kushirikisha wakubwa wa nje kwani bila azimio la Zanzibar, suala la ten percent unalozungumzia lingeleta matatizo;

Power - Tanzania imekuwa na tatizo la umeme kwa muda mrefu na kikubwa na maslahi binafsi katika shirika hili la Tanesco. badala ya kujenga uwezo wa kuwa na umeme wa uhakika, kikubwa kinachofanyika ni mshiko kwanza yaaani 10%. Je, mwekezaji gani anaweza kuja kuwekeza katika mazingira ambayo hakuna umeme wa uhakika??!!.

Ni kweli; Umeme wa dharura una ulaji wa uhakika zaidi kuliko miradi ya kudumu, na tumeshaliona hili kwa undani sasa; Watawala wetu wanaweka maslahi binafsi mbele ya maslahi ya taifa; Tumeishiwa viongozi wenye Uzalendo na nchi yao, mimi sioni hata mmoja ndani ya ccm, wote ni wachumia tumbo tu; wanachopishana labda ni tarehe;
Mgongano wa kimaslahi - Leo hii tumeshuhudia wafanyabiashara wakubwa katika nchi hii ni viongozi wa serikali. Je, wanaweza kufanya kazi zao zilizo rasmi bila kuwa na mgongano wa kimaslahi.
Tatizo kama hili ni kielelezo kikubwa kwanini Azimio La Arusha (sio lote) bado linahitajika; Mwalimu alipata sana shida miaka michache baada ya uhuru kuwaweka sawa viongozi wenzake ndani ya TANU kwamba wapo kwa ajili ya kutumikia nchi, sio matumbo yao; Kwenye TANU NA RAIA (1962) Nyerere anatamka kwamba:
[…kilichokuwa kikituuma ni kwamba ubwana na ufahari wa wazungu waligawana wenyewe tu, bila kutugawia sisi pia; baadhi yetu hatukuwa tunadai uhuru ili uwapunguzie watu wetu mzigo huu wa ubwana na ufahari, bali tamaa yetu ilikuwa ni kukalia viti vile vya ubwana na ufahari. Tamaa yetu haikuwa kushika vyeo tu, vilivyokuwa vimeshikiliwa na wazungu hapo zamani, tulitaka na mishahara pia iliyokuwa ikifuatana na vyeo hivyo, bila kujali kama watu wetu wanaweza kulipa mishahara hiyo, bila kujali maisha ya watu wetu…”]
 
Mdau mwenzetu Mzalendo80 ameshindwa kupata access ya kuchangia humu baada ya mjadala huu kuhamishiwa kwenye jukwaa la great thinkers kutoka kwenye jukwaa la siasa; MODs, hasa invisible na wengineo, tafadhali naomba m-grant access kwa mzalendo80 humu, ana mawazo mazuri na imebidi niyapokee kwa njia nyingine; Anasema hivi:

Sikubahatika kuchangia huu uzi
Bomu la Lowassa: Tumeligundua, Tunaliteguaje? na wala sababu sijui ila nilikuwa anataka kusema haya.

Bomu la Lowassa: Tumeligundua, Tunaliteguaje?

With limited jobs available and a soaring youth-unemployment rate, one would expect the unemployed youths of Tanzanian to seek alternative forms of employment..

The Government it needs to do more to create a positive entrepreneurial culture that supports a fruitful business environment in which young entrepreneurs can flourish. Encouraging entrepreneurship amongst this generation could serve as a very viable solution to the rising youth-unemployment rate, income inequality and rising poverty levels.

This can be done by promoting and recognizing entrepreneurs who have not only been successful in their own right, but also in doing so have benefited others.

But I don't expect this to be done on Kikwete government, because himself he his failure and his disgrace to our Nation. He never show to be serious of issue unemployment or to be concern about rising of number of the young Tanzanian who are unemployed

Our government must come to grips soon with the growing number of unemployed young people or it risks increasing social problems or even violence in our Nation.

Asante kwa mchango wako mzalendo80, ntakurudia muda sio mrefu kujibu hoja zako muhimu;
 
Tupe idadi kama hizo hizo za mwaka wowote kati ya 1961-1985 na za mwaka wowote kati ya mwaka 1986-1995 na za mwaka wowote kati ya 1996-2005. Tujiridhishe na uchambuzi wako.
Unaposema "TUPE", niwape kina na nani, na niwape kama nani? Kwanini usifanye utafiti wako kama nilivyofanya mimi kisha uje na takwimu zako ili tuweze jenga mjadala mzuri zaidi kwa manufaa ya taifa? Kujiita MCHAMBUZI haikuwa na maana kwamba najiona ni nguli, ilikuwa ni urahisi tu wa kutafuta jina kujiunga humu miaka mitano iliyopita baada ya ile jamboforums kufungwa; Vingineyo ni muhimu ukaelewa kwamba I AM HERE TO REASON IN ORDER TO SEEK THE TRUTH, NOT TO WIN ARGUMENTS; Tafadhali, tushirikiane katika kufikia ukweli katika hili, lakini kama nia yako ni to reason ili kushinda, sidhani kama wewe na wenzako unaowajua mna washindani; Siku zote nyinyi ni washindi;

Ukiweza kuziweka kama ulivyoziweka hizo hapo juu, ntakujuwa kweli umechambuwa, ukishindwa najuwa hizo ni porojo tu na hazina maana yoyote kwani hazina "comparison", nimeitaja hiyo miaka ya awamu tofauti za uongozi wa nchi hii.
This is so low of a comment katika mjadala muhimu kama huu; hauwezi ku discredit reputable sources kama hizi za worldbank, norad n.k; Ulichotakiwa kufanya ni kuniulizia references; vinginevyo nia yangu haikuwa kufanya comparison bali baada ya kuona hoja za wachangiaji fulani fulani, i took the initiative and effort kwenda kutafuta takwimu na hizo ndio nilizopata kwa haraka haraka; kama nyingine zipo, zitapatikana tu, vinginevyo ufisadi ni ufisadi, hata takwimu ya mkupuo mmoja tu wa EPA kwa mfano, tayari ni ufisadi; haina haja ya kufanya comparative analysis kubaini hilo;
 
Unaposema "TUPE", niwape kina na nani, na niwape kama nani? Kwanini usifanye utafiti wako kama nilivyofanya mimi kisha uje na takwimu zako ili tuweze jenga mjadala mzuri zaidi kwa manufaa ya taifa? Kujiita MCHAMBUZI haikuwa na maana kwamba najiona ni nguli, ilikuwa ni urahisi tu wa kutafuta jina kujiunga humu miaka mitano iliyopita baada ya ile jamboforums kufungwa; Vingineyo ni muhimu ukaelewa kwamba I AM HERE TO REASON IN ORDER TO SEEK THE TRUTH, NOT TO WIN ARGUMENTS; Tafadhali, tushirikiane katika kufikia ukweli katika hili, lakini kama nia yako ni to reason ili kushinda, sidhani kama wewe na wenzako unaowajua mna washindani; Siku zote nyinyi ni washindi;


This is so low of a comment katika mjadala muhimu kama huu; hauwezi ku discredit reputable sources kama hizi za worldbank, norad n.k; Ulichotakiwa kufanya ni kuniulizia references; vinginevyo nia yangu haikuwa kufanya comparison bali baada ya kuona hoja za wachangiaji fulani fulani, i took the initiative and effort kwenda kutafuta takwimu na hizo ndio nilizopata kwa haraka haraka; kama nyingine zipo, zitapatikana tu, vinginevyo ufisadi ni ufisadi, hata takwimu ya mkupuo mmoja tu wa EPA kwa mfano, tayari ni ufisadi; haina haja ya kufanya comparative analysis kubaini hilo;

Nilijuwa huwezi, kwani itakuwa umejichinja mwenyewe.

Utafiti bila "comparison"? ni utafiti au porojo tu? kwi kwi kwi teh teh teh.
 
Mwalimu had his strong points and weak points; naamini kwamba nia ya Azimio la Arusha ilikuwa nzuri – the END was JUSTIFIED, tatizo ilikuwa ni the MEANS, hasa katika Utekelezaji wa sera nyingi za Ujamaa; Kwa mfano, zipo taarifa kwamba wakulima walikuwa wanarushiwa tu magunia ya mbolea kwenye milango yao majumbani huko vijijini na TRDB (later CRDB), ovyo ovyo tu bila proper stocking, training jinsi ya kutumia which led to a lot of wastage; mabwana shamba pia walikuwa ni watalii tu huko vijijini na pikipiki zao za serikali; ;

Mkuu hakuna kitu chochote duniani ambacho ufanikiwa bila ya utekelezaji, na ukija kwenye suala la maendeleo ufuatiliaji/utelekelezaji is the catalyst ya hayo maendeleo. Sasa basi wewe unaweza kuona matatizo yalikuwa ya wakulima labda sijui hawakusoma au kutofahamu namna ya kutumia mbolea vizuri, ways to stock them na mengineo au uzembe wa bwana shamba.

Vyote hivyo vina fall into poor execution of the policy and it shows a luck of mission to achieve the desired outcome, au hata hawakupanga (expecting a certain desirable outcome).

Kutokana na hayo pengine ndio ukawa mwanzo wa uzembe wa mabwana shamba sidhani kama wao walijua ni what was expected of them from the central government, kwenye desired results and even if their perfomances where measured.
Sasa kama msimamizi au mshauri hafanyi kazi zake na kageuka mtalii, kweli unategemea mkulima hataelewa taratibu au mbinu ambazo zinahitajika hili ajue kujiendeleza.

Mtu unaweza pengine sema hiyo sera ya kilimo ilitaka tu watu wale kwa kuwa wengi walikuwa hawana hela na kilimo ndio njia pekee ilikuwa ya kuweza lisha vijiji.

Lakini as to expect, kilimo kilete mageuzi ya maendeleo kwa uliyouaelezea it was impossible. The mission was bound to fail from the outset not because of the farmers lack of motivation, but rather poor execution strategy from those responsible with the policy.

No wonder waka amua kupeleka much efforts kwenye siasa, na hapo ndio wengine tunasema akili ya mwalimu ilikuwa inawaza sana udikteta kuliko maendeleo mbona huko alifanikiwa umeshawahi jiuliza kwanini, ukweli ni kwamba alikuwa na hands on approach kwenye utawala wake wa serikali na apparently hakuwa hivyo kwenye kilimo orelse bwana shamba asingegeuka mtalii.

Pia allegedly kulikuwa na section ya bureaucrats ambao constantly walikuwa wanashirikiana na imperialists to undermine Ujamaa kwa kuvuruga state owned companies ili zionekane zinaendeshwa kwa hasara, pia serikali ilipanuka ghafla kimatumizi to meet political objectives kuliko development objectives baada ya ndoa ya ASP na TANU 1977, ambayo ilipelekea Katiba mpya (1977), ambapo CCM ilishika hatamu na serikali kuanza to finance state activities ambazo nyingine zilikuwa ni za kisiasa zaidi na nyingine counterproductive; pia ikaja Vita ya Kagera ambayo iligharami nchi zaidi ya USD 500 Million; Yapo mengi ambayo yaliupa Ujamaa wakati mgumu hence the eventual collapse;
Hayo ndio ninayoita majibu yenye adorations kuliko yenye kutaka kuelezea ukweli, sio kwamba pengine haikuwa hivyo kama unavyotaka kutuamisha. Lakini kuna suala la ukaguzi na kupitia mafanikio yako na kutafuta solution kama kuna matatizo.

Hiwapo walishaona wamejaribu na mambo hayapo sawa na the evidence was in their (kutokana na tabu za maisha na kufa kwa viwanda), hiwapo sababu hazikuhusiani na hali ya uchumi wa ndani na wala wa njee surely the blame was visible.

To me the management who were responsible to oversee those policies basi ndio watakuwa wakufukuzwa na huo muda wa kuaribu nisingewapa. Again inaonesha udhaifu wa mwalimu kwenye masuala ya maendeleo, hila kwenye kuongoza ki-udikteta hakushindwa.

Point zingine nitazirudia for the purpose of shortening my reply.
 
Nilijuwa huwezi, kwani itakuwa umejichinja mwenyewe.

Utafiti bila "comparison"? ni utafiti au porojo tu? kwi kwi kwi teh teh teh.

Siwezi kufanya nini? Kuleta takwimu za UFISADI 1961-1985 and so forth kwa demand yako? Wewe unazijua kwani? Kama hauzijui kwanini? Kama unazijua, zikwapi ili uzijengee hoja yako kulinda utawala unaokusudia? Anwyays, tunahitaji hizo za nini? Kwani title ya mada hii ni "A HISTORICAL ACCOUNT OF GRAND CORRUPTION IN TANZANIA?"

Hivi mnapewa nini na CCM mpaka mnakosa kabisa logic kwenye vitu ambavyo ni common sense? Watu kama nyie ndio mnafanya wana CCM wote tuonekane hatunazo;

Vinginevyo sijaja na uchambuzi wowote wa ufisadi from a historical point of view bali nilikuwa najaribu kuchangia hoja muhimu sana ya janjaweed ambayo nadhani wewe binafsi umekosa namna ya kuizamia na kuichokonoa Ki-CCM; isitoshe umerukia hoja katikati, hata hauelewi janjaweed alikuwa anajaribu kujenga hoja gani; Vinginevyo awamu ya kwanza kulikuwa na rushwa, awamu ya pili kulikuwa na rushwa, awamu ya tatu kulikuwa na rushwa, na awamu ya nne pia kuna rushwa; Tofauti iliyopo baina ya awamu ya kwanza na zilizofuatia ni political will to defeat it; Nakushauri uliangalie hili kwa upeo huo kuliko kuulizia takwimu za rushwa wakati wa nyerere, na kufananisha na mwinyi, mkapa na Kikwete;

Kama wewe ni mtu wa makamo, ntaelewa kwanini hoja zako ni za kupambapamba tu CCM kwani itakuwa unakaribia kustaafu hivyo unajiwekea mazingira mazuri ya pensheni, vinginevyo kama wewe ni kijana, achana na mafisadi hao, hawana zaidi ya miaka 15 kwenye siasa, wakiondoka utaficha uso wako wapi wakati utakuwa ndio kwanza pengine umeingia mwaka wa 50?

You have a chance to choose the right side of history and that time is now; Vinginevyo anzisha uzi wa comparative analysis ya ufisadi huku ukikinga utawala wako, na sisi tutakuja tu kuchangia;
 
Sekta ya kilimo ilikuwa inazalisha sana lakini less and less was re-invested in agriculture, na hii ni kinyume na inavyotakiwa katika mchakato wa agricultural transformatiom; Hii ikapunguza sana Ari ya wakulima kuendelea kuzalisha mazao ya biashara ambayo ndio yalikuwa yanaleta fedha za kigeni kwa serikali kuendesha mambo yake; Serikali ilifanya kosa kutumia kilimo zaidi kama sekta ya kuchota fedha from exports ya agro products, na kuzitumia kuendesha a huge and inefficient public sector, kuwaweka sawa wasomi na wakazi wa mijini in terms of employment kwenye parastatals na pia kuwapatia social services nzuri ili wasi revolt against the party and government, huku wakulima wakiwa wanaumia kupitia unfavourable producer prices; ;
Hapo kwenye red nadhani nimepagusia hawali na my thinking nimekuelezea kilimo hakikikuwa priority ya maendeleo then na wala sasa kama unavyoona utupaji wa hela unaoendelea kwenye sera ya ‘kilimo kwanza'.

Na so far hatujaelezewa mafanikio ya hiyo sera ni ‘dejavu' za sera za kilimo Tanzania, hatuwezi kuendela kutegemea watu wakitumie kilimo kutuletea maendeleo especially kikiwa kama uti wa mgongo. There is no incentive ya maendeleo hapo isipokuwa ni maslahi ya wajanja wachache kukwepua pesa tu. Amna wakati wowote katika historia yetu tunaweza tukasema kilimo kilimwinua mtanzania wa chini na kuweza kujisadia yeye na familia yake na kumpa a sustainable life.
Hayo ni matokeo ya sera mbovu za kilimo tangia uhuru wa taifa hili, lakini ardhi hii hii ndio iliyowatijarisha wazungu na kilimo walichokifanya africa.

Suluhisho hapo ni kuwapatia ardhi watu wenye nia ya kukifanyia kazi kilimo hili kilete ajira na kuweza kusaidia taifa, linakuja swali la kusema hata wakikuza hayo mashamba leo kuna sera gani za kukuza viwanda so far amna pengine tutegemee kuuza kwenye soko la ndani la dunia soko ambalo lin an already saturated global market (new challenges arise tunalima nini and for what known global advantages), kama ni kulima for the sake of it watu kama hawana shida na maembe yako watakupa bei mbuzi hutaki wacha yakuozee, yaani it's a cycle of failures na hizi siasa zetu.

Hapa ulikuwa unazungumzia privatization, hasa on how most former state owned enterprises ended up going bankrupt and eventually land in the hands of foreigners; Internal factors zilichangia sana kuliko external factors, lakini hili nimejadili kidogo hapo juu; Vinginevyo palikuwa hakuna jinsi bali privatize these SOEs, lakini nadhani kulikuwa na namna bora zaidi ya kufanya hivyo ambayo ingeleka a win-win situation; Again, just as Ujamaa , pia Liberalization, Privatization and Marketization were Justified, tatizo ni MEANS, hasa the implementation bit; Pengine ni kutokana na severity ya hali mbaya ya uchumi we failed to own the Reform Agenda; ;
That is another way of saying ujamaa failed misery despite our arrogance, most of us in the society could not raise capital to turn those failing industries and farm into inside private entities, the only way out was to go through that outside investment and I believe this were the poor economical policies were born na mambo ya mikataba uchwara fro a desparate nation needing investment.

Sasa why do we need to look back and try to embellish that chapter of our history knowing were it left the nation not just us, but many who had similar visions?

Why cant we just focus on finding a better mechanism to adapt with the world flow of the economic pattern to our advantage. Instead the of never ending disruption with people always referring to our failed past as a model for our future prospects?

Lakini pia hapa nashangaa kwanini Sir George Kahama alipewa kazi ya kuwa MD wa kwanza wa NDC ambayo ndio ilikuwa na jukumu to industrialize the country, na baada ya failures za baadae, reforms zikaja na ikaanzishwa Investment Promotion Centre (IPC), ambayo sasa ni TIC, na huyu huyu Kahama akawa MD wa kwanza wa hii parastatal iliyokuwa inatekeleza sera za de-industrialization; was it a coincidence kwa mtu kupewa wadhifa kusimamia industrialization then later de-industrialization? kulikuwa na mantiki katika hili?
Hapa sielewi ni fikra za waliomteua ndio watajua kwanini, all I can ni kwamba umenipa shule kuhusu huyu mjamaa.


Hapa ulikuwa unazungumzia the second industrialization in Tanzania; Nakubaliana na wewe katika hili, ndio maana all along, ingawa sio vizuri kuwa skeptical on such issues, I have been very skeptical kwani as you rightly put it, hali ya wakati ule haina tofauti na sasa, pengine it has gone worse in terms of effects za globalization whereby mfumo wetu mzima umekuwa dismantled kabisa na kuwa tegemezi; it would need a lot of work to re-industrialize Tanzania tena, lakini hatua ya kwanza muhimu ni political will;
Lakini pia hapa nashindwa kuelewa – kuna viwanda ambavyo vilikuwa very successful and very profitable to the state – textiles, food processing, leather, oil, lakini as soon as protection barriers were taken out, they were the ones hit the hardest; what is your view on this – au kwa hili you would sustain your argument on the quote above?
Pia kuna sehemu umenijibu hivi:

Hapa tunaweza ona sawa kama unavyosema, hila mimi napendekeza vita mbele na si kurudi nyuma kujaribu kujenga maendelo kupitia ujamaa, kwakuwa unadumaza na hau ecourage innovation and responsibilities kama historia hilivyo tufundisha sio kwetu tu pekee bali kote kuliko jaribu hilo namna hiyo.
 
JokaKuu,

Una hoja za msingi sana kwenye bandiko lako namba 42; Kimsingi tupo pamoja katika hoja zako; Ningependa kuchangia kidogo mawazo yangu kama ifuatavyo, kuendana na jinsi hoja zako zilivyoamsha ubongo wangu:

Nadhani inabidi tuje na industrial policy ya maana, sio hii ya sasahivi ya ubabaishaji na inayotegea capital inflows kutoka nje ambazo kwanza hazina guarantee, pili zinakuja na masharti yasiyokuwa na manufaa kwa watanzania walio wengi, na tatu, zinaangalia maeneo ambayo yanaleta short term profits, hasa natural resources; capital inflows zinazoenda kwenye manufacturing sector ni kidogo sana;

Tukirejea kwenye industrial Policy yetu i.e. Sustainable Industrial Development Policy (SIDP), inatamka kwamba:

The main purpose is to design a plan for industrializing Tanzania so that, by 2025, the country has become semi-industrialized in such a way that industry can be said to account for over 40% of the GDP.

Swali linalofuatia ni je, tunafikaje huko? Jibu ni kwamba:

"The Tanzania SIDP agrees with and encourages the ideas of a market-led economy and, to this end, states that the Tanzania industry sector will be able to succeed with increased private sector participation in the decision making and implementation practices."

"In order to comply with these findings, the government of Tanzania has agreed to continue to provide a welcoming, attractive, stable and encouraging environment for investors who are interested in examining the private sector opportunities within the country."

Ukitazama kwa makini hapo, focus ipo zaidi katika kutegea mitaji kutoka nje (FIDs), sio kutengeneza mazingira ambayo yatazalisha indigenous capitalist/entrepreneurs, na kwa kuanzia, kwa kufanyia kazi kwanza maeneo uliyoyataja kama vile education curriculum n.k; Kwa kifupi, bila ya aibu, sera yetu ya industrialization ni ya mgeni njoo mwenyeji apone;

Watawala wetu wanashindwa kuelewa kwamba kinachotenganisha nchi maskini na nchi tajiri katika dunia ya le ya utandawazi sio just the disparity in CAPITAL and other resources, lakini pia THE GAP IN KNOWLEDGE; Ni muhimu sana tukaja na industrial policy ambayo inalenga ku - promote technology , ku-enhance our competitiveness ili tuweze ongeza our exports na kuongeza uwezo wetu to compete with foreign imported goods; Kuna mchumi mmoja alipata tamka kwamba:

"It makes no difference whether the economy produces potato chips or computer chips, the economy should produce whatever maximizes GDP."

Swali muhimu at this juncture ni: Je, What role should our government play in this context?

Kama tulivyokwisha jadili awali, ujio wa economic liberalisation uliondoa serikali katika shughuli za uchumi; Lakini kama ulivyoelezea hapo juu, hakuna uchumi unaofanikiwa bila mkono wa serikali; It remains to be true for South Korea, India, Brazil, na hata mataifa makubwa kama marekani, UK, France n.k; Kwa mfano, bila mkono wa serikali ya Obama during the economic slump ya 2008, tungekuwa tunazungumza mengine leo hii; Na iwapo taifa kubwa kuliko yote kiuchumi na kinara wa ubepari na soko huria (MAREKANI), leo anahubiri juu ya umuhimu wa serikali kuwekeza katika elimu, utafiti n.k, kwanini wakubwa hawa hawa ambao IMF na WorldBank ndio nyumbani kwao hawaoni umuhimu wa hilo katika nchi zetu maskini, ambazo literally zimekuwa kwenye economic depression since independence?

Baada ya uhuru 1961, tuliambiwa na wakubwa hawa kwamba sababu kwanini tupo nyuma kiuchumi ni kwamba - tuna uhaba wa mitaji (lack of capital), ingawa tuna abundant labour (nguvu kazi); Na ili tuendelee, ni muhimu tuka karibisha mitaji kutoka nje, lakini kwanza kwa kutengeneza mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji (This was 1960s), na ni lazima tuweke the necessary incentives kama vile tax holidays, easy repatriation of profits, labour laws kali kali ili ku-discipline workers wasilete migomo n.k; Tukafanya haya yote by 1962; Lakini cha ajabu, kipindi cha 1962 - hadi 1966, hakuna FDIs za maana zilizoingia nchini, na cha ajabu zaidi ni kwamba, Mitaji mingi ikaanza kuja baada ya azimio la arusha mwaka 1967, na mitaji hii ilitoka nchi mbalimbali kama UK, US, Sweden, huku World Bank wakilisifia sana Azimio La Arusha;

Miaka ya 1960s-1970s our industrial policy chini ya ujamaa ikawa ina swing kati ya import substitution na export oriented industrialization huku tukitumia mitaji ya UMMA (hasa mapato kutoka mauzo ya mazao ya kilimo nje), pia kulikuwa na local private capital kidogo, lakini mitaji mikubwa ilikuwa ni ile kutoka nje kwa njia za mikopo kutoka WorldBank etc, na vile vile tulikuwa tunalipa mataifa ya nje fedha nyingi sana in terms of management contracts kuendesha viwanda vyetu; Mazingira kama haya yanajieleza yenyewe kuhusu nini kilichangia viwanda vingi kuanza kufa;

Lakini cha ajabu ni kwamba mass goods industries kama vile viwanda vya nguo (textiles), ngozi, oil, bia, sigara, vilifanikiwa sana na viwanda hivi vilitegemea zaidi mitaji yetu ya ndani kuliko mitaji kutoka nje; Yalipokuja mageuzi ya uchumi ambapo vitu vya msingi vilivyohimizwa vilikuwa ni Privatization, Marketization na Liberalization, chini ya WorldBank na IMF, ghafla tukaanza ku-undergo de-industrilization kwa kasi ya ajabu hata katika viwanda hivi vya mass goods ambavyo hakivukuwa vikiendeshwa kwa hasara; Cha ajabu ni kwamba, viwanda hivi ndio vikawa hit the hardest, WHY?

Muda sio mrefu, tukaanza kuambiwa hadithi zile zile za miaka ya 1960s kwamba – ooh, nyinyi hamjaendelea kwa sababu hamna mitaji, ingawa mna abundant labour; sasa ili kuendelea, ni muhimu kutengeneza mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji, na ni lazima tuweke the necessary incentives kama vile tax holidays, easy repatriation of profits n.k. Hapa tukaona Investment Promotion Centre (IPC) ikianzishwa kufanikisha hayo, na baadae ikageuzwa kuwa TIC chini ya Sitta;

Matukio haya yalitosha kuwaonyesha viongozi wetu kwamba wakubwa hawa wa nje hawana nia njema na viwanda vyetu, Kwahiyo tusikubali kufuata sera, maagizo na masharti yao kwani yalitufelisha tayari huko nyuma; Walichofanya watawala wetu ni kufungua milango hadi chumbani na kubinaifishwa kiholela tu; Ilitakiwa tuhimiza wawekezaji wakati ule waje kwenye Greenfield projects kwani hizo ndio zina-create new jobs, zinajenga economic linkage kwenye local economy huku wazawa wakipata nafasi ya kushiriki katika supply chains na value chains etc etc; Badala yake, tukawauzia tu wakubwa wan je viwanda na mashirika yetu and what they did wa literally asset stripping, suala ambalo halikupelekea creation of wealth to the economy au creation of jobs;

Ni muhimu kwa serikali kurudi at the centre na kuongoza industrial policy, sio kuachia wawekezaji, WorldBank/IMF/WTO, na Soko kuongoza suala hili; Role of the government ni muhimu, lakini wakubwa hawa wanataka the government to be rolled rolled/pushed back kwa sababu ambazo tunazielewa – kufanya hivyo kunawapa nafasi wakubwa hawa to control our economic policies, resources n.k, kwa faida yao kwa mwendo ule ule wa ukoloni, ila katika nyakazi hizi, ina diplomatic way;

Kama ulivyoanisha, ni muhimu kwa serikali to play a central role katika uchumi katika maeneo muhimu, kama vile financing SMEs (nchi za nje, hasa marekani wana kitu kinaitwa Small Business Administration [SBA], na FEDEX alizaliwa kwa hilo); Pia serikali iwekeze kwenye Research, kwani hili haliwezi kufanywa na private sector, na hata marekani na kwingine, kwa mfano technology ya Internet ingesubiria private sectir kuwekeza, tusingekuwa hapa; Research zenye manufaa kwa nchi, financing yake haina collateral au returns ambazo zinajulikana from day one, so this has to be the domain ya serikali; Pia serikali ijikite kuwekeza kwenye elimu, hasa educational curriculum kama ulivyojadili, miundombinu, n.k, kwani haya yoye yatasaidia nchi yetu iweze ku-shape our economy and its competitiveness;

Lazima labour market na education ziwe linked vizuri – kuwepo na life long educational programmes ambazo ni relevant kwa mahitaji ya uchumi (sio ajira tu), education should aim at learning to learn, kwani katika hili sisi hatupo kabisa, we just want to learn to earn; Suala la curriculum ulilozungumza ni muhimu sana, hasa tuibadilishe ili kuwepo na link baina ya University and Industry; Karne ya kumi na tisa, elimu ilielekezwa katika ku-train na ku-discipline nguvu kazi kwa ajili ya industrialization; Pamoja na umuhimu huu, ni lazima pia tujue kwamba katika karne ya 21, kwa wenzetu, education needs are directed towards developing entrepreneurship and the ability to cope with a fast changing world;

Mwisho, uchumi wa kisasa unazidi kuwa ni ule unaoegemea kwenye Service Sector and Knowledge economy; Transformation kutokea kilimo kwenda viwanda ilihitaji a major reorientation, na pia tumeona kwamba katika mataifa makubwa yenye uchumi wa kisasa, transformation from the manufacturing to the new economy nayo imekuwa very dramatic; Lakini kwa bahati mbaya, watawala wetu sidhani kama wanaelewa changamoto tuliyonayo, hasa kuhusu vision on where our economy is going kwani zaidi ya kumumunya mumunya maneno kwamba lengo ni kufikia uchumi wa kati by 2025, hawana lolote la maana wanalofanya;
 
Mtambuzi hoja yako imekaa vizuri ila tumpongeze lowasa kwa lipi ndugu yangu, Rushwa, kuchezea uchumi wa nchi(richmönd) au kujilimbikizia mihela isiyosaidia wtz ?...Tanzania ina kila kitu maji,madini,mafuta/gesi,ardhi,mifugo...tunae adui wa taifa mpya UBINAFSI ambaye anaturudisha kulekule ktk ujinga, maradhi na umaskini...tukiacha ubinafsi ajira zinaweza kutengenezwa/kujitengeneza eg,wtz wanaanzisha machimbo then Wabinafsi wanapeleka ffu kuwatimua na kuwapa wageni kwa kodi za kipumbafu.. Mtambuzi ubinafsi umetufikisha pahala tunadhani hatuwezi kufanya kitu..vijana wa tz wamejaa hamasa na wako tayari kwa fursa itakayojitokeza, nani wa kuonyesha njia,hapa tatizo siyo maamuzi magumu bali MAONO..imeandikwa MBINAFSI HANA MAONO kila anapoangalia ni palipo na tumbo lake tuu.. Wapo wtz wanye uwezo wa kututoa hapa..je wataruka kiunzi cha adui Ubinafsi?

Nachomaamisha ni pongezi kwa lowassa kwa kuamsha viongozi wenzake juu ya hilo, lakini pia kuamsha umma kwani pamoja na kwamba suala hili limejadiliwa na watafiti kwa miaka mingi, ni kama vile lowassa ndio kawafungua macho watanzania walio wengi; Nje ya hapo, sina ubia wowote na Lowassa na wala simuhitaji yeye ili kuendesha maisha yangu, kama ilivyokuwa yeye kuto nihitaji mimi kuendesha maisha yake;

Mimi ninacho furahia, na pengine wengi humu wataniunga mkono katika hili, ni kwamba angalau sasa suala la ukosefu wa ajira kwa vijana linaweza kupata POLITICAL WILL kutokana na intervention ya Lowassa, bila ya kujalisha chama gani au mtu gani ataingia Ikulu 2015, kwani umma sasa umepata ufahamu juu ya suala husika;
 
Mkuu, nimesoma hii post ya jamaa ina mlengo wa limsafisha lowasa, lakini kwa context ya habari yenyewe na data zake, na jinsi watu wanavyochangia ki ukweli wamebase sana kwenye mada, kwa hiyo mleta mada hapa ameshindwa kumsafisha EL.

Na nashukuru umeliona hilo kwani sipo hapa kumsafisha Lowassa na nilishaeleza awali kabisa kwanini nimemtaja Lowassa katika mada hii, na nilihimiza kwamba mjadala wa lowassa juu ya hili una mapengo ambayo nia yangu ni kuyaziba, na hilo litafanyika kwa kujadili hoja, sio mtoa hoja; Sidhani kama umesoma bandiko langu namba moja, vinginevyo sidhani kama ungezungumza haya;

Vinginevyo mimi sina ubia na Lowassa, na sijawahi kumuhitaji na wala sitamuhitaji katika maisha yangu ya fikra huru, na uanachama wangu wa CCM haukutokana na Lowassa, na itaendelea kubakia hivyo;
 
Mkuu hakuna kitu chochote duniani ambacho ufanikiwa bila ya utekelezaji, na ukija kwenye suala la maendeleo ufuatiliaji/utelekelezaji is the catalyst ya hayo maendeleo. Sasa basi wewe unaweza kuona matatizo yalikuwa ya wakulima labda sijui hawakusoma au kutofahamu namna ya kutumia mbolea vizuri, ways to stock them na mengineo au uzembe wa bwana shamba.

Vyote hivyo vina fall into poor execution of the policy and it shows a luck of mission to achieve the desired outcome, au hata hawakupanga (expecting a certain desirable outcome).

Kutokana na hayo pengine ndio ukawa mwanzo wa uzembe wa mabwana shamba sidhani kama wao walijua ni what was expected of them from the central government, kwenye desired results and even if their perfomances where measured.
Sasa kama msimamizi au mshauri hafanyi kazi zake na kageuka mtalii, kweli unategemea mkulima hataelewa taratibu au mbinu ambazo zinahitajika hili ajue kujiendeleza.

Mtu unaweza pengine sema hiyo sera ya kilimo ilitaka tu watu wale kwa kuwa wengi walikuwa hawana hela na kilimo ndio njia pekee ilikuwa ya kuweza lisha vijiji.

Lakini as to expect, kilimo kilete mageuzi ya maendeleo kwa uliyouaelezea it was impossible. The mission was bound to fail from the outset not because of the farmers lack of motivation, but rather poor execution strategy from those responsible with the policy.

No wonder waka amua kupeleka much efforts kwenye siasa, na hapo ndio wengine tunasema akili ya mwalimu ilikuwa inawaza sana udikteta kuliko maendeleo mbona huko alifanikiwa umeshawahi jiuliza kwanini, ukweli ni kwamba alikuwa na hands on approach kwenye utawala wake wa serikali na apparently hakuwa hivyo kwenye kilimo orelse bwana shamba asingegeuka mtalii.

Hayo ndio ninayoita majibu yenye adorations kuliko yenye kutaka kuelezea ukweli, sio kwamba pengine haikuwa hivyo kama unavyotaka kutuamisha. Lakini kuna suala la ukaguzi na kupitia mafanikio yako na kutafuta solution kama kuna matatizo.

Nia yangu haikuwa kutoa lawama au kujaribu kuaminisha watu juu ya jambo lolote, zaidi ya kufafanua tu based on my analysis and view of things kuhusu jinsi gani utekelezaji wa sera ya ujamaa ulikuwa na matatizo, hasa nikijikita zaidi katika kuelezea kwamba THE END WAS JUSTIFIED, TATIZO LIKAWA ON THE MEANS TOWARDS THAT JUSTIFIED END;

inginevyo Ujamaa ulivutia sana hata wakubwa wa nje kwani kwa kiasi kikubwa sana Ujamaa ulikuwa financed na World Bank chini ya the then president - McManara, na pia nchi nyingi za ulaya zilitoa misaada mingi ili kusaidia kufanikisha sera ya ujamaa; Na hata tukitazama takwimu za capital inflows na AID, kipindi cha 1961 - 1966, hizi nflows zilikuwa chache sana, lakini mara tu baada ya ujamaa, hali ilibadilika kabisa; Uchumi ulifanikiwa sana kukua katika kila sekta muhimu, hasa katika kipindi cha 1970-1977; Tatizo likajitokeza towards the late seventies all the way to 1984-85;


Again, moja ya sababu kubwa kwanini ujamaa ulifeli ni kwa sababu Kilimo kilikuwa kinazalisha sana na kusaidia sana ujenzi na uendelezaji wa mass gooods industries kama vile oil, leather, textiles, lakini kwa bahati mbaya, mapato ya viwanda hivi hayakurudi kuendeleza sekta ya kilimo, na badala yake yalitumika kuendesha serikali na sekta yake kubwa sana ya umma, na kutoa huduma za kijamii kwa wingi, hasa mijini, lakini pia vijijini; Ukiachilia huduma hizi, wakulima hawakufaidika sana na kilimo, hasa kupitia favourable producer prices na ni hapo sasa kila kitu kikaanza kuanguka - uzalishaji wa kilimo ukaanza kuporomoka, mapato ya fedha za kigeni kupitia kilimo yakaanza kushuka, uwezo wa serikali kununua vipuri na malighafi muhimu - capitals goods, oil, na pia kulipia management contracts kuendesha viwanda vikaanza kushuka, na taratibu viwanda vikaanza kuzalisha at very low capacity, huku output iki shrink.....and eventual collapse was looming kwani sasa serikali ikaishiwa fedha kuendesha viwanda, kutoa huduma za kijamii, kulipa madeni ya nje...; Yote haya yalitokana na mixture of poor implementation na kwa kiasi fulani external factors;

To me the management who were responsible to oversee those policies basi ndio watakuwa wakufukuzwa na huo muda wa kuaribu nisingewapa. Again inaonesha udhaifu wa mwalimu kwenye masuala ya maendeleo, hila kwenye kuongoza ki-udikteta hakushindwa.

Again, Mwalimu alikuwa na madhaifu yake mengi tu, lakini hakuwa kwene udhaifu juu ya NIA; Ni kweli, moja ya madhaifu hayo ilikuwa ni kuhamisha hamisha General Managers waliokuwa wanaharibu mashirika mbalimbali, lakini tatizo kubwa lililojitokeza ni kwamba hawakuwa na makosa ya moja kwa moja kwani kuanzia 1977 CCM ilishika hatamu na NEC ndio ilikuwa inatoa maamuzi na maelekezo kwa Baraza la mawaziri, benki kuu, na taasisi zote muhimu za uchumi; Mashirika ya UMMA yaliendeshwa kisiasa, na kulikuwa na matawi ya CCM kwenye mashirika yote; Kwa kifupi, siasa zilitawala uchumi kuliko uchumi kutawala siasa;
 
with Tanzania employment system naona tatizo liko kwenye tafiti hasa zilizofanywa kuhusu aina za ajira ambazo tunazo, na aina ya waajiriwa tulionao. sijui kwann kil siku nimekuwa ni mgumu wa kuelewa hili ila labda hapa mtanielewesha zaid juu ya hili.

hivi Mchambuzi kazi ya TAESA ni nini? najua utasema ni uwakala wa ajira lakin je unaweza kuwa wakala pasi kuresearch juu ya aina ya bidhaa unayotaka kuiuza ukajua wateja wake ni wepi , matumizi gani, na kwa wakati gani?

pia hii tume ya ajira nayoa ina fanya nini? je kazi yake ni kupokea barua za waajiri wwenye uitaji wa watumishi na kutangaza kama ubao tu?

mbona hatuoni ikijishughulisha kutengeneza nafasi nyingine za ajira?????? sasa je majukumu yake na TAESA yanatofautiana vipi? sikatai uchumi na nafasi yetu vinampa kijana wakati mgumu sana wa kujiajiri na hii pia ni zao la aina ya elimu tuipatayo mashulen lakn nafikir ingetosha kuwa nyenzo nzuri ya kuanzia kutatua tatizo hili.
 
Last edited by a moderator:
Mzalendo80,

Ulichokisema ni cha msingi sana i.e. kujenga mazingira ya entrepreneurial culture, na sio kiholela holela kama hivi sasa ambapo mtu yoyote asiye na ajira au elimu anajiita mjasiriamali, bali kwa serikali kutengeneza mazingira ya kusaidia small businesses kama vile kwa mfano ilivyo nchini marekani chini ya Small Business Administration (SBA) ambako hata Fedex ilianzia huko;

Key to developing this kind of environment lazima ianze na education ambayo ni muhimu ianze kuwa directed towards developing entrepreneurship and the ability to cope with a fast - changing world; Muhimu zaidi ni kwamba serikali ije na mikakati ambayo itasaidia taifa to keep skilled and well educated population at home kwa kuwajengea mazingira ya kuwajali na ya kuwaendeleza;

Pia ni muhimu kwa serikali kuanzisha industrial parks, incubators, na pia kujenga mazingira ambayo yatasaidia tuwe na financial institutions ambazo zipo more specialized kusaidia small businesses badala ya SMEs kupigana vikumbo for credit na large firms kwenye mainstream institutions; Venture capital ni one of the areas that can be worked on;

Lakini yote haya lazima yatokee ndani ya a comprehensive industrial policy kama nilivyojadili katika majibu yangu kwa jokakuu kwenye bandiko namba 53 la mjadala huu; Kilichopo hivi sasa ni industrial policy ambayo ipo very narrow and external oriented kwa maana ya kwamba - kwanza hailengi katika kutengeneza indigenous capitalists and entreprenuers bali kuweka mitego ya kuwavutia wawekezaji kutoka nje, huku mafisadi wakiishia kuwa ndio local shareholders au mabepari na entrepreneurs uchwara wasio na any value addition kwa uchumi wetu;

Pili, sera yetu ya sasa ya viwanda ipo narrow in the sense kwamba haina any meaningful elements za research and innovation, haina any meaningful linkage ya labour market na education - hasa suala la kufanyia mabadiliko education curriculum ili kuwe na closer links baina ya vyuo vikuu na industry and so forth and so forth;

Ni muhimu pia tujue tunataka nini - transform our economy towards industrialization? au we want to leap frog into service sector and knowledge economy? We are not very specific on this, zaidi ya kuwa na ndoto tu kwamba bu 2025 tutakuwa a middle income country with a significant contribution ya viwanda kwenye GDP; How do we get there? and what are the pre - conditions that we need to meet before we get there? And how do we prioritize our planning? Majibu kwa maswali kama haya hakuna;

Kuhusu JK na uongozi wake wa uchumi, binafsi sidhani kama ni sahihi sana kumtupia lawama yeye, kwani kipindi cha mwinyi, mkapa, kikwete, wananchi wa vijijini hawajaona utofauti wowote mkubwa katika hali zao za maisha; Kuna so many factors at play ambazo hata wakija Chadema watakumbana nazo na kupata wakati mgumu sana wa kuendeleza legitimacy and credibility yao kwa umma;

Tukirudi kwenye hoja kwamba utawala wa JK haua tofauti na Mwinyi na Mkapa, okay, fine, miundo mbinu imeendelea, sekta ya mawasiliano imekuwa, lakini maendeleo yote haya hayajawa na any meaningful impact kwa mwananchi wa kijijini in terms of income growth, improved education and skills za kumfanya awe marketable kwenye soko la ajira n.k; mwanakijiji ni yule yule wa mwaka 1985 Nyerere alipoondoka, na pengine he/she is worse off now kutokana na ujio holela wa soko huria kwani hakuandaliwa bali alishtukizwa na hajui how to cope with it;

Ni muhimu kwa serikali yetu kuja na vision on where it aims to take our economy and this vision should involve participation of the poor and the indigenous private sector in terms of input katika devising this vision; Otherwise vision 2025 sio yetu bali ni ya worldbank, IMF, WTO; We need to once again own our development agenda just as we did under Mwalimu, and this begins with the Political Will;
 
with Tanzania employment system naona tatizo liko kwenye tafiti hasa zilizofanywa kuhusu aina za ajira ambazo tunazo, na aina ya waajiriwa tulionao. sijui kwann kil siku nimekuwa ni mgumu wa kuelewa hili ila labda hapa mtanielewesha zaid juu ya hili.

hivi Mchambuzi kazi ya TAESA ni nini? najua utasema ni uwakala wa ajira lakin je unaweza kuwa wakala pasi kuresearch juu ya aina ya bidhaa unayotaka kuiuza ukajua wateja wake ni wepi , matumizi gani, na kwa wakati gani?

pia hii tume ya ajira nayoa ina fanya nini? je kazi yake ni kupokea barua za waajiri wwenye uitaji wa watumishi na kutangaza kama ubao tu?

mbona hatuoni ikijishughulisha kutengeneza nafasi nyingine za ajira?????? sasa je majukumu yake na TAESA yanatofautiana vipi? sikatai uchumi na nafasi yetu vinampa kijana wakati mgumu sana wa kujiajiri na hii pia ni zao la aina ya elimu tuipatayo mashulen lakn nafikir ingetosha kuwa nyenzo nzuri ya kuanzia kutatua tatizo hili.

Gfsonwin,

Nashukuru kwa mchango wako; Kwa kweli hata mimi sielewi TAESA inafanya shughuli gani ya maana kwa taifa letu kwa sababu kwanza, imejitwisha mambo mengi sana badala ya ku narrow down kwenye suala la employment or job creation, lakini pili, haina nguvu sana, hasa kutokana na uhaba mkubwa wa sheria (Acts) ambazo zingeisaidia kufanikisha majukumu yake vizuri zaidi; Kwa mfano, kuna sheria ngapi za ajira na ni za aina gani? Zinalenga wage earners wa namna gani? Na zinasaidia vipi job seekers? Haya ni maswali ambayo ni mgumu sana kuyapatia majibu;

Kuhusu takwimu, ingawa NBS ipo chini ya wizara ya kazi na ajira, sijawahi kuona jinsi gani takwimu hizi zinatumika kurahisisha shughuli idara hii; kwa ufupi, TAESA ni moja ya idara za serikali ambazo zipo kwa sababu inatakiwa ziwepo;

Mimi nadhani iwapo tutakuja na national vision ambayo ni home grown badala ya huu uchwara wa vision 2025, na pia tukafanya reforms katika sekta yetu ya elimu, na pia tukaja na an effective industril policy kama nilivyojadili awali katika majibu yangu kwa jokakuu bandiko namba 53, hapo ndio tutaweza sasa kuwa na idara kama ya TAESA yenye tija, na pia sheria muhimu ambazo zitasaidia sana idara kama hiyo to carry its functions effectively; vinginevyo kwa sasa, TAESA haina specific purpose zaidi ya orodha ya mambo ambayo ni vague na pia not rellevant na conditions in the labor market;
 
MCHAmbuzi nashukuru kwa clarifications zako, lakini labda tujikumbushe nyuma ambako uchumi wetu ulijikita katika matumizi na uzalishaji wa ndani. hivi wafkiri wakati huo hali yetu ya kiuchumi ilikuwa juu kwasababu gani?

je ni kwasababu ya elimu ya kujitegemea watu waliyokuwa nayo?
je ni kwasababu ya rasilimali tulizo kuwa nazo ama ni kwasabbu ya sera?

tukisha yajua hayo tuje je wakati huo nini kilichotengeneza ajira? ni watu wangapi ambao kwa wakati huo walikuwa wanajua kusoma na kuandika na waliajiriwa? hapo sasa tutaweza kujua adui wetu kwenye ajira na uchumi wa taifa hili viko wapi.

kimsingi huwa nabisha sana niambiwapo kijana anatakiwa ajitengenezee ajira. na nafikiri wewe ni mmoja wapo utakayenibishia ila mantiki yangu iko hapa, utamwambiaje kijana ajitengenezee ajiara katika nchi ambayo creativity haipewi kipaumbele? utajitafutiae ajira katika nchi ambayo localy manufactured goods hazzina ubora/ ziwe na ubora lakin zinakosa soko?

mfan mdogo tu, keko makochi kuna wategenezaji wengi sana wa viti tena vijana wa kitanzania, tujiulize how many pple go and shop there? leo hi nenda nyumban kwa kigogo yyte kam autakutana na sofa ama kiti cha keko kwanini? siku hizi hadi majeneza watu wanaagiza toka nje je unategemea huyu kijana ajiajiri wapi?

ni wazi kwamba fursa pekee unay muachia kijana ni ya kilimo tu, sasa je how worth is it? analima kwa jembe la mkono, mashamba ya kukodisha, maji ya shida manake tuna rely mostly kwenye kilimo cha mvua. siku akivuna sokon anakutana na upinzani mkali sana kwa mazao ya biashara price fluctuation inamwangusha, kwa mazao ya chakula lack of processing industries inamwangusha mwisho wa siku anaishia kupata hasara yeye.

nionavyo mm serikali yetu achilia mbali kisera, kisheria na hata kiuwezeshaji hawajalenga kufungua milango ya ajira kwa tanzanian youths. zimebaki kuwa story amazo watu wanaandikia papers na kufanyia tafiti ili tu watajirike halafu wale sample group inabaki poor.

kimsingi kama kunamahali ambapo vijana na watanzania tunatakiwa kuamka ni hapa, ambapo sasa ifike mahali tudai sera zenye tija na zinazotekelezeka kwenye kila eneo la ajira. tusisubiri eti wakati ufike, hakuna mwenye uchungu na hili at least Lowassa amehubutu but sasa atuambie atalifanyeje hili?
 
Back
Top Bottom