tonge nyama
JF-Expert Member
- Jul 28, 2008
- 380
- 498
Subiri na wewe ubomolewe nyumba yako uone uchungu wake hizo fidia wewe unajuaje kama zinalingana na hali halisi au thamani ya majengo hayo ? Ya Kibamba unayajua? Usianze kumtukana mkunga wakati uzazi ungalipo wengine ni wapangaji wa hizo nyumba zilizo bomolewa je serikali inaweza kufidia hizo hasara walizopata? Najua hayo ni masuala ya Landlord Vs Tenant lakini mbona hawakupewa muda wa kujiandaa? Tafadhali hiki ni kisa cha kusikitisha na sio kufurahia. Hao watu wa ardhi walikuwa wapi wakati jamaa wanajenga? Leo wanataka kupanua Bandari kwa kigezo cha wananchi. Nasikia wanataka kubomoa hata Kanisa la St Joseph pale Posta ya Zamani sasa wewe unayesema maendeleo umetumia kigezo kipi? Elimu , Sayansi na teknolojia au maendeleo ya kifisadi kwa kutumia mikataba haramu huku wananchi wakiumia? Sikukandii ila naomba ufikirie mara mbili kabla ya kusema.
Sio swala la mim kufikiria mara mbili, wewe unaetaka kujenga sehemu ambayo hujaidhinishiwa kwa matumizi hayo ndio wa kufikiria mara mbili kabla ya kutenda. Ziko nyumba zenye thamani ya mamilioni ya shilingi lakini tatizo zimejengwa bila mpangilio. Kama unaweza kujenga nyumba ya milioni thelathini ulishindwa nini kuwaita wapimaji (kwa sh 500,000) kutoka ardhi wakupimie na kisha upewe hati na kama hapawezekani ushauriwe kutafuta pengine? Zipo baabdi ya nyumba tulishindwa kupitisha jeneza kwenda kumzika jamaa kwajinsi nyumba zilivyofungamana, halafu unailaumu serikari hujalipwa fidia ya kutosha. This is the price u'll pay for your negligence bwana.