Bomoabomoa ya kibabe yatikisa Jiji

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,462
VILIO na majonzi vimetawala leo asubuhi eneo la Kurasini baada ya tingatinga kutinga na kuanza kubomoa nyumba huku baadhi ya nyumba zikiwa na mali ndani ambapo vibaka wakivamia grosari na kunywa pombe za bure.

Baadhi ya wakazi walikuwa wakiangua kilio huku kukiwa na ulinzi mkali wa askari Polisi na mbwa ili kuimarisha ulinzi kusitokee vurugu na uporaji.

Ubomoaji huo umefuatilia rufani ya wahanga hao kutupwa na Mahakama Kuu ya Ardhi ambapo wakazi hao walikwisha lipwa fidia ili kupisha upanuzi wa bandari.

Waandishi wa gazeti hili leo asubuhi wameshuhudia askari tingatinga namba T 223 AFD likianza kubomoa nyumba moja baada ya nyingine bila kujali kama kuna mali au lah.

Hali hiyo ilileta utata kwa baadhi ya wakazi ambao walikuwa bado hawajahamisha mali zao kusubiri maamuzi ya mahakama ambapo walilazimika leo kutoka nje na kupisha tingatinga kuendelea na shughuli zake.

Bomoabomoa hiyo imeanzia Kurasini Zamcargo ambapo baadhi ya wakazi walijaribu kugomea operesheni hiyo lakini hata hivyo ilishindikana kwa kuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESC0),walikuwa tayari wamekata umeme ili ubomoaji huo usilete madhara .

Gazeti hili lilishuhudia baadhi ya wakazi wakihamisha mali zao huku vibaka nao wakiwahi kuokota nondo na mali nyingine na kutoweka nazo huku wengine wakivamia katika grosari zilizokuwa wazi na kujipatia vinywaji vya bure.

Umati mkubwa ulifurika kushuhudia operesheni hiyo ambapo baadhi ya wakazi leo alfajiri waliamka na kujisalimisha kwa kuvunja nyumba zao wenyewe na kuokoa baadhi ya mali kwa kushirikiana na ndugu na jamaa.

Nyumba hizo zilitakiwa kuvunjwa kwa muda mrefu ambapo Serikali ilitoa fidia kwaakazi wa eneo hilo ambapo wengine walivunja nyumba zao na kuhama lakini baadhi yao walifungua madai ya nyongeza ya fidia waliyolipwa awali wakilalamika kuwa haiendani na gharama za maisha ya sasa.

Source;Dar Leo.
 
Hivi kweli vitendo kama hivi ni muhimu? Kwanini wasiwape muda wa kuhamisha vitu vyao?

Labda kama watu wamekaidi amri ya mahakama, vinginevyo kwa nchi maskini kama za kwetu, hatutakiwi kabisa kuharibu mali za wananchi kwa njia kama hizi.
 
some times ubabe kama huu unahitajika. Watu tumekuwa na tabia ya kuijaribu nguvu ya serikari. wewe umeshalipwa na umeambiwa uondoke kupisha maendeleo halafu unang'ang'ania kubaki unategemea nini? kwanza nyumba zenyewe zilijengwa kienyeji bila kuzingatia ramani za mipango miji, jamani hamuoni miji ya wenzetu inavyopendeza? cheap things are always expensive bwana.
 
Jamani machungu haya watu chao hawajalipwa ujanja ujanja wa maofisa wa ardhi basi wameamuru watu wabomolewe huku kesi ipo mahakamani hii nchi mmh bora kuwa mkimbizi tu hapa ni uonevu mkubwa we fikiria nyumba mtu kajenga inathamani zaidi ya mil25 anaambiwa asaini form yenye mil.12 wapi na wapi?>???
 
Hivi kweli vitendo kama hivi ni muhimu? Kwanini wasiwape muda wa kuhamisha vitu vyao?

Mtanzania,

uwajuhi waTanzania, ukiwapa muda wa kuhamisha vitu, wao wanakimbilia mahakamani kuweka pingamizi. Kesi hiyo itachukua miezi mingine 6 au hata mwaka, then wanakuja kushindwa!

Jiji likisema tunawapa siku 3 kuhamisha vitu vyenu, wanakimbilia tena mahakamani kukata rufaa nyingine, uchukua tena miezi 6 au mwaka!

Ndio maana Jiji linasubiri mara baada ya hukumu ya mahakama, wao wanaanza bomoa bomoa, maana ukiwapa muda hata wa siku 1 kuhamisha vitu vyao, basi ujue wao hawatahamisha bali kukimbilia tena mahakamani kukata rufaa.

Kosa ni kwamba kwanini walikubali kupokea fidia ya mwanzo! Wangeanza kuigomea hiyo fidia na sio kuipokea halafu unagoma kuondoka unataka nyongeza!!
 
Still....wanaweza kwenda mahakamani tena............kama wanadhani wameonewa....ili mradi wawe wali-document vizuri mali zao....utamaduni ambao wengi wetu hatuna.......
 
some times ubabe kama huu unahitajika. Watu tumekuwa na tabia ya kuijaribu nguvu ya serikari. wewe umeshalipwa na umeambiwa uondoke kupisha maendeleo halafu unang'ang'ania kubaki unategemea nini? kwanza nyumba zenyewe zilijengwa kienyeji bila kuzingatia ramani za mipango miji, jamani hamuoni miji ya wenzetu inavyopendeza? cheap things are always expensive bwana.

Subiri na wewe ubomolewe nyumba yako uone uchungu wake hizo fidia wewe unajuaje kama zinalingana na hali halisi au thamani ya majengo hayo ? Ya Kibamba unayajua? Usianze kumtukana mkunga wakati uzazi ungalipo wengine ni wapangaji wa hizo nyumba zilizo bomolewa je serikali inaweza kufidia hizo hasara walizopata? Najua hayo ni masuala ya Landlord Vs Tenant lakini mbona hawakupewa muda wa kujiandaa? Tafadhali hiki ni kisa cha kusikitisha na sio kufurahia. Hao watu wa ardhi walikuwa wapi wakati jamaa wanajenga? Leo wanataka kupanua Bandari kwa kigezo cha wananchi. Nasikia wanataka kubomoa hata Kanisa la St Joseph pale Posta ya Zamani sasa wewe unayesema maendeleo umetumia kigezo kipi? Elimu , Sayansi na teknolojia au maendeleo ya kifisadi kwa kutumia mikataba haramu huku wananchi wakiumia? Sikukandii ila naomba ufikirie mara mbili kabla ya kusema.
 
Rushwa inanuka kila kona,Nyumba ya milioni 50,alafu unalipwa millioni 12 kwa kigezo kuwa ulishalipwa.Hata kama ni mbumbumbu utagoma kuhama.
Hii ni dhihaka kabisa.
Hivi kwa nini Kila kitu utakuta wananchi ndio wakosaji tu?tugasa!!!!!!!!!!!
Haya maswala yakifumbiwa macho wananchi kudhulumiwa haki na kuonewa nchini kwao basi uwezakano wa kutokea uasi dhidi ya serikali ni mkubwa.
 
Tinga tinga lipo kazini ,Mpaka saizi bomoa bomoa imepamba moto.
1202.jpg
 
Hivi kweli vitendo kama hivi ni muhimu? Kwanini wasiwape muda wa kuhamisha vitu vyao?

Labda kama watu wamekaidi amri ya mahakama, vinginevyo kwa nchi maskini kama za kwetu, hatutakiwi kabisa kuharibu mali za wananchi kwa njia kama hizi.

Siungi mkono watu kubisha uamuzi wa mahakama, lakini sina hakika uwezo wa hiyo mahakama ya nyumba kama kweli ipo, na sijui ni kwanini wananchi wang'ang'anie hata baada ya kulipwa fidia. Uamuzi ukitolewa for the interest of majority and for greater good na ukapewa baraka na mahakama kuu na hata ya rafaa, ni jambo jema.
Lakini political leadership inatakiwa kutumia conviction kuwahamisha watu, na sio kubomoa na kuharibu mali za watu. Nadhani kutakuwa na genuine grounds kama hao jamaa wakilalamikia kuwa mali zao, (sio nyumba) zimeharibiwa in process kwa hiyo wanaweza dai fidia.
 
Tinga tinga lipo kazini ,Mpaka saizi bomoa bomoa imepamba moto.
View attachment 1974

Tatizo hao watu wa mipango miji, hiyo miji hivi waliipanga llini? baada ya watu kujenga kiholela au? Je hao watu walipokuwa wakiuziana viwanja na kujenga kuna yeyote (hata balozi nyumba kumi..) aliyewaambia hili ni eneo la bandari?,...kama hakuna sasa inakuwaje wanabomolewa bila kulipwa kikamilifu?

tatizo kubwa zaidi ni kwamba ujenzi holela bado unaendelea kama kawa, next 5 years tutasikia wengine tena wamebomolewa ili kupitisha mabomba ya maji!
 
Watanzania tuna kasumba mbaya ya kudharau sheria muhimu za arthi...utakuta hizo nyumba zilijengwa ilihali wakijua kabisa kuwa hilo ni eneo la bandari.

Sasa siku inafika wanaambiwa ondoka wanakimbilia mahakamani...hii ni tabia chafu imeenea sana Tanzania. Maeneo karibu yote ya wazi mijini yamejengwa mengi ya hayo maeneo yalipimwa enzi za ukoloni mtu wanayekuja kujenga miaka 80 au 90 halafu wanajifanya hawakujua hilo sio tatizo la serikali.
 
Tatizo hao watu wa mipango miji, hiyo miji hivi waliipanga llini? baada ya watu kujenga kiholela au? Je hao watu walipokuwa wakiuziana viwanja na kujenga kuna yeyote (hata balozi nyumba kumi..) aliyewaambia hili ni eneo la bandari?,...kama hakuna sasa inakuwaje wanabomolewa bila kulipwa kikamilifu?

tatizo kubwa zaidi ni kwamba ujenzi holela bado unaendelea kama kawa, next 5 years tutasikia wengine tena wamebomolewa ili kupitisha mabomba ya maji!

Watanzania wengi wanakuwa na taarifa kamili kuwa hili ni eneo la bandari au barabara au eneo la wazi lakini wao ndio utakuta wako mstari wa mbele kuhonga maafisa wa arthi ili ramani za jiji zibadilishwe au wapewe vibali kujenga kwenye hayo maeneo. Matokeo yake wengi wanatapeliwa na siku ikifika ndio vilio kama hivi vinasikika.
 
...acheni Bandari Ipanuliwe Jamani......kwanza Ni Hasara Nyumba Ya Mbavu Za Mbwa Au Hata Ya Kifahari Kuzuia Upanuzi Wa Bandari.....uchumi Wetu Unaumia Kutokana Na Bandari Kuelemewa.....

..ningekuwa Na Uwezo ...ningevunja Squaters Zote Mjini Ie..mazenze,uwanja Wa Fisi,buguruni.....na Squeters Zote Along Highways .....kwa Sababu Hayo Maeneo Itakuwa Faida Zaidi Kuweka Viwanda Au Container Terminals Kuliko Makazi......ningevunja Alafu Ningefanya Ppp[private Public Partnership]....ambapo Watakaonunua Maeneo Husika Watajadiliana Moja Kwa Moja Na Wamiliki Wa Awali Na Kulipana.......

Hayo Maeneo Yaliyojegwa Zembe Pia Wawekezaji Wanaweza Kuwalipa Wamiliki Wa Awali..na Pia Wakapewa Apartment Mara Ujenzi Unapokamilika....unajua Kote Huko Ukijenga Magorofa....itasaidia Watu Wengi Wanaokaa Mbali Na Kuchelewa Kazini Na Kushusha Tija....
 
Kama kesi ilikuwa mahakamani, hiyo inamaana hatima ya jambo ilikuwa bado.

Kama hatima ya jambo ilikuwa bado, watu wasingeweza kuhama.

Tatizo linakuja, mahakama iliyaona madai yao hayana msingi lini? Na kwa nini wasipewe muda zaidi kutoka siku mahakama ilipoyatupilia mbali madai yao mpaka ubomoaji utakapoanza?
 
Hivi kweli vitendo kama hivi ni muhimu? Kwanini wasiwape muda wa kuhamisha vitu vyao?

Labda kama watu wamekaidi amri ya mahakama, vinginevyo kwa nchi maskini kama za kwetu, hatutakiwi kabisa kuharibu mali za wananchi kwa njia kama hizi.

..mswahili habembelezeki na hana ustaarabu huo unaoutegemea.

..ingekuwa hivyo tungefika mbali sana.
 
..mswahili habembelezeki na hana ustaarabu huo unaoutegemea.

..ingekuwa hivyo tungefika mbali sana.

..ni kweli hawabebeki..kama wale waliosaidiwa na rais akawaapa milionmi 20 kila mmoja pale tabata dampi..sasa wanagoma kufuta kesi waliyoahidi baada ya kulipwa ..SAASA WANATAKA WAPEWE TENA MILIONI 30 KILA MMOJA
 
..wakati mwingine wanapotajwa baadhi ya watu kuwa ni mafisadi, mi huguna!

..it seems, watanzania wengi ni mafisadi, kwa nafasi zao mbalimbali.
 
Tinga tinga lipo kazini ,Mpaka saizi bomoa bomoa imepamba moto.
View attachment 1974
Nadhani Watanzania we are learning the hard way. Inawezekana ndiyo njia pekee.....Si waombei haya, lakini panapokosekana mshikamano katika mambo makubwa ndiyo yanayotokea. Tunahitaji kujiuliza kama hakuna njia za kistaarabu zaidi? Kama vyombo vyote husika vilitimiza majukumu yao? Kama hakuna mipangilio katika mambo yote ndiyo inavyotokea. Wenzetu mlioko nje ni vema mkatupa pia uzoefu kwa wenzetu haya mambo yanafanyikaje mbona hatusikii vya hivi? Ni ngozi nyeusi ina matatizo zaidi au nini? Lakini pia kwanini kuna Estate developers kwa wenzetu? kwanini kuna credit facilities zikiwemo za nyumba kwa wenzetu? Hivi ukilipwa 12 huna ardhi utajenga wapi? labda tu apply hadithi ya Abunuwas....Nadhani Wanaharakati Tunahitaji uchambuzi wa kina. Haiwezekani kila kona ya nchi yatokee haya na daima wananchi wawe wakosaji tu..... Tunajitaji kuchambua na kutibu once for all. Wasio husika hasa wanawake na watoto, na wapangaji wasio hata na taarifa ya kinachoendelea wanaumia sana.
 
Back
Top Bottom