Bomoabomoa ya kibabe yatikisa Jiji

Bila ubabe nchi haiendi hii...........

Si kweli, ni makosa yaliofanywa na viongozi mwanzoni kuingiza siasa kwenye kila jambo ndio tunavuna sasa. Kama sheria zingefuatwa toka tunapata uhuru sidhani kama tungefikia hatua hizi.
 
Heshima mblele wakuu... sasa hii mambo ya bomoa bomoa mbona ianzidi kurindima humu jijini na mambo ya mirathi ndio on top of that!!

Nimeikuta hii kwenye Mwananchi la leo:

Bomoa bomoa ya kikatili Magomeni

Na Salim Said

FAMILIA sita zimekosa sehemu ya kuishi baada ya watu wanaodai kununua nyumba ya urithi ya watoto zaidi ya 10 wa marehemu, Yussuf Mbonde iliyopo Magomeni Mwembechai, kubomoa nyumba hiyo kwa kutumia greda huku wakilindwa na vijana wa kukodi maarufu kama mabaunsa pamoja na usimamizi wa polisi waliokuwa na silaha.

Bomoabomoa hiyo ilitokea jana majira ya saa 9:00 alasiri baada ya uvamizi huo kutokea na kusambaratisha nyumba na vitu vyote vilivyokuwemo ndani.

Kwa mujibu wa wanafamilia, waliohusika na uvunjaji huo ambao wamedai kuinunua nyumba hiyo kutoka kwa Ayasi Mbonde ambaye ni mjomba wa wanafamilia hao, ni Sabahi Chondoma na Abdallah Chondoma.

"Nyumba ni ya kwetu na hatujauza, Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ilisema haina uwezo wa kusikiliza kesi hii na kutuambia twende mahakama ya ardhi na kesho (leo) ndio ilikuwa tunaenda mahakamani," alisema Ayoub Yussuf.

Alisema rasharasha za bomoabomoa hiyo zilianza juzi wakati watu hao walipoenda na kuvunja milango ya maduka na ya uani huku wakitoa maneno ya vitisho kwamba lazima wahame la sivyo watauawa.

"Sabahi anatuambia tutahama lazima kwa sababu yeye ana fedha na polisi ni watu wake hivyo hawawezi kumfanya lolote," alisema mwanafamilia huyo kwa machungu.

Yussuf alifafanua kwamba baada ya vitisho hivyo walienda kwa mwenyekiti wa mtaa na Kituo cha Polisi Magomeni kutoa taarifa, lakini hawakupewa ushirikiano.

"Polisi ndio waliosimamia tena walikuwa na silaha, halafu hakuwa na hata namba katika sare zao," alisema Rajabu Yussuf.

"Wametuvamia kwa marungu na mawe mimi mwenyewe mkono huu wamenijeruhi; wamenipiga mawe ya kifua na mdogo wangu wamempiga mawe usoni; watoto wetu wengine walikuwamo ndani hatuwaoni," alisema.

Miongoni mwa mali zilizoharibiwa ndani ya nyumba hiyo ni vitu vyote vilivyokuwemo ikiwa ni pamoja na fedha taslimu ambazo watu hao waliobomolewa walidai kuwa ni Sh20 milioni.

Juhudi za kumpata mwenyekiti wa serikali ya mtaa wala watu wanaodai kununua nyumba hiyo pamoja na mjomba wao, hazikufanikiwa, huku polisi waliokuwepo eneo la tukio wakikataa kuzungumza na mwandishi kwa madai kwamba si wazungumzaji wa jeshi hilo .

Wanafamilia hao walisema hawana mahali pa kwenda baada ya nyumba yao kubomolewa na watabakia hapohapo kwa kuwa wao ni masikini hawana fedha ya kuhonga kwenye vyombo vya sheria.

Wanaodai kuwa ni warithi halali wa nyumba hiyo ni Zuwena, Riziki, Ayoub, Sharifa, Abdalla, Juma, Bakari, Fatuma na Rajabu ambao wote ni watoto wa marehemu mzee Yussuf Mbonde.

Kwa ujumla watu waliokuwa wanaishi humo pamoja na watoto ni watu 15.

http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=7091
 
Back
Top Bottom