Bomoabomoa ya kibabe yatikisa Jiji

Subiri na wewe ubomolewe nyumba yako uone uchungu wake hizo fidia wewe unajuaje kama zinalingana na hali halisi au thamani ya majengo hayo ? Ya Kibamba unayajua? Usianze kumtukana mkunga wakati uzazi ungalipo wengine ni wapangaji wa hizo nyumba zilizo bomolewa je serikali inaweza kufidia hizo hasara walizopata? Najua hayo ni masuala ya Landlord Vs Tenant lakini mbona hawakupewa muda wa kujiandaa? Tafadhali hiki ni kisa cha kusikitisha na sio kufurahia. Hao watu wa ardhi walikuwa wapi wakati jamaa wanajenga? Leo wanataka kupanua Bandari kwa kigezo cha wananchi. Nasikia wanataka kubomoa hata Kanisa la St Joseph pale Posta ya Zamani sasa wewe unayesema maendeleo umetumia kigezo kipi? Elimu , Sayansi na teknolojia au maendeleo ya kifisadi kwa kutumia mikataba haramu huku wananchi wakiumia? Sikukandii ila naomba ufikirie mara mbili kabla ya kusema.

Sio swala la mim kufikiria mara mbili, wewe unaetaka kujenga sehemu ambayo hujaidhinishiwa kwa matumizi hayo ndio wa kufikiria mara mbili kabla ya kutenda. Ziko nyumba zenye thamani ya mamilioni ya shilingi lakini tatizo zimejengwa bila mpangilio. Kama unaweza kujenga nyumba ya milioni thelathini ulishindwa nini kuwaita wapimaji (kwa sh 500,000) kutoka ardhi wakupimie na kisha upewe hati na kama hapawezekani ushauriwe kutafuta pengine? Zipo baabdi ya nyumba tulishindwa kupitisha jeneza kwenda kumzika jamaa kwajinsi nyumba zilivyofungamana, halafu unailaumu serikari hujalipwa fidia ya kutosha. This is the price u'll pay for your negligence bwana.
 
tatizo hawa watu walilipwa fidia na kupokea. imefika wakati wa kuhama wanadai fidia ilikuwa ndogo and they want re-evaluation!! ni ngumu kidogo kuwatetea japo wana kesi mahakama kuu ya ardhi
 
the matter is before judge Nchimbi Land case No. 74/08 i have seen the details na mbaya zaidi judge mwenyewe yuko kwenye session arusha hakuna msaada wowote kwa hawa watu kwa sasa
 
Haya ndo maafa ya huko ZAMCARGO
Vunja.JPG
Hebu fikiria umeenda kazini asubuhi unarudi jioni unakutana na kiama hiki.
Vunja-5.JPG
 
Naipongeza Serekali Lazimaiwe Katikamsimamokama Huu Hakuna Kuchezea Sekalika Amriikitoka Ndioimetoka Hakuna Kufanya Mzahaa Bomowatu
 
kama taratibu zilifuatwa kwa kweli hakina haja ya kuoneoana aibu kwani ili tuendelee tunahitaji watu kuwa waelewa na siyo ubishi bila kuwa na msingi wa kubishana

haya ni matokeo ya kudanganyana vijiweni na kupata tafsiri ya mambo kwa yule anayejua kuongea sana pale kijiweni ukipanda ubishi wa kujinga lazima uvune ujinga wako na ukipanda busara na utashi wenye mawanda mapana ya kuelewa huwezi kukaa na kubishana badala ya kutekeleza wajibu wako kwanza ndipo ukabishane
 
Na wale walio jenga magereji na nyumba katika maeneo wazi na ya shule kama kule Sinza Afrika Sana wao vipi?

Walio jenga juu ya mabomba ya maji Je?

Waliojenga Mahekalu na Mahotel ufukweni kinyume cha sheria je?

Waliojenga mabondeni kama Bonde la Msimbazi?

Waliojenga na kuziba mifereji ya maji hadi mafuriko kutokea, kama huko Mwananyamala kinondoni je?

Tuna nyumba Maelfu pale Dar za kubomoa.

Twaweza fungua midomo kusema sana juu ya yanayoendelea huko ZAMCARGO, lakini ikifika zamu ya kubomoa kila kona ya jiji hadi Ufukweni, nahisi kusema kutaendelea lakini kwa hoja kinyume.
 
Hata kama ujengaji wa nyumba ulijengwa kwenye kiwanja ambacho ni rightful yours, hawa hawa wanaelewa kwamba hivi viwanja walivyojengea nyumba sio vyao/chako 100%. Tunajua kwamba serikali itapokuja kutaka kutumia eneo hilo kwa manufaa ya Umma, wanachukua anytime, sasa tatizo nini na waliombwa waondoke????
Mahakamani, kwenda kwao mahakamani pia haina maana wakishinda kesi wataendelea kukaa hapo; whether they win or lose kuondoka ni-inevitable! Sasa mlitaka mlipwe kwanza hizo nyongeza(kama mkishinda kesi) ndio mlete ma-uhaul kubeba mali zenu? Ulalamishi tu mmeonewa mmeonewa kila siku. Mmeonewa sasa nini hapa? WaBongo saa nyingine bwana…..!

Hakuna cha nchi za nje wala ndani kufanyaje vitu wakikumbwa na situation kama hii. Si kila kitu tuige nje bwana.

Du, naona kweli unataka Rule of Law iwepo bongo. Mwanangu wenzako tulio huku tunakwenda kibongobongo.
 
Bongo kuna Temporary Building Permit, ambayo ina kipengere kinachosema kuwa
"Iwapo eneo hili litahitajika na serikali unatakiwa kuondoka pasipo kulipwa fidia yoyote"
Wengine wanabahati ya kulipwa fidia.....na bado wanabeza sheria
 
Na wale walio jenga magereji na nyumba katika maeneo wazi na ya shule kama kule Sinza Afrika Sana wao vipi?

Walio jenga juu ya mabomba ya maji Je?

Waliojenga Mahekalu na Mahotel ufukweni kinyume cha sheria je?

Waliojenga mabondeni kama Bonde la Msimbazi?

Waliojenga na kuziba mifereji ya maji hadi mafuriko kutokea, kama huko Mwananyamala kinondoni je?

Tuna nyumba Maelfu pale Dar za kubomoa.

Twaweza fungua midomo kusema sana juu ya yanayoendelea huko ZAMCARGO, lakini ikifika zamu ya kubomoa kila kona ya jiji hadi Ufukweni, nahisi kusema kutaendelea lakini kwa hoja kinyume.

hii imetulia mwanangu...asante
 
Hakika hii ndiyo Tanzania, hebu inakuwaje mtu ndani ya nchi yake anyanyaswe? utacheke hadi mbavu zikuchomoke ukiwasikiliza wale wanaobomolewa nyumba, yaani ni vituko, wanasema, walipita wathamini na hawakuelewana hochote, mara wanaletewa cheq, hautakiwa kubisha, sahihi ndiyo silaha yako, na kama haujaridhika basi ungetakiwa kwenda mahakamani, na huko makamani si mnajua tena
 
Nadhani Watanzania we are learning the hard way. Inawezekana ndiyo njia pekee.....Si waombei haya, lakini panapokosekana mshikamano katika mambo makubwa ndiyo yanayotokea. Tunahitaji kujiuliza kama hakuna njia za kistaarabu zaidi? Kama vyombo vyote husika vilitimiza majukumu yao? Kama hakuna mipangilio katika mambo yote ndiyo inavyotokea. Wenzetu mlioko nje ni vema mkatupa pia uzoefu kwa wenzetu haya mambo yanafanyikaje mbona hatusikii vya hivi? Ni ngozi nyeusi ina matatizo zaidi au nini? Lakini pia kwanini kuna Estate developers kwa wenzetu? kwanini kuna credit facilities zikiwemo za nyumba kwa wenzetu? Hivi ukilipwa 12 huna ardhi utajenga wapi? labda tu apply hadithi ya Abunuwas....Nadhani Wanaharakati Tunahitaji uchambuzi wa kina. Haiwezekani kila kona ya nchi yatokee haya na daima wananchi wawe wakosaji tu..... Tunajitaji kuchambua na kutibu once for all. Wasio husika hasa wanawake na watoto, na wapangaji wasio hata na taarifa ya kinachoendelea wanaumia sana.

Dr. W. Slaa,

Ni lipi la kushangaza mpaka uulize swali hili..

Process ya mswada,,, utanisahihisha nitakapokosea...

Mswada huandaliwa na serikali, makongamano ya kuuelewa, stakeholders meetings na wabunge wakialikwa, semina kwa wabunge, mswada kusomwa kwa mara ya kwanza, mara ya pili... na mara ya tatu mnapitilia mstari hadi mstari na kuupitisha....

Baada ya muda mfupi Rais anasign... mswada unakuwa sheria... Poa sina tatizo...

Haya si chini ya miezi sita mswada umeanza kufanya kazi, wabunge wanaulalamikia, semina nyingine inaandaliwa kuwaelimisha waheshimiwa wabunge...

Swali kama mswada ulipita sehemu michakato yote hiyo ya Bunge si utaamini kabisa kwamba Mbunge ndiye atakuwa ameielewa sheria kuliko raia mwingine yeyote.. sasa simina za baada ya sheria kutungwa ni za nini?

Kurudi kwenye maada kama wabunge watunga sheria haya yanatokea... unashangaa nini... mtu aliyejenga kwenye bonde la mto kuwa mbishi kiasi hicho.
 
Miaka ya karibuni nilinunua kiwanja ambacho hakikupimwa, katika kufuatilia masuala ya upimaji na leseni ya makazi, nikajikuta nipo ofisi ya kata, katika kucheki ramani nikagundua kwamba ardhi ya upande wa kushoto wa kiwanja changu inahesabiwa kama bondeni, na mtendaji akanihakikishia kwamba hapo ni bondeni na aliyejenga hapo hakutakiwa kujenga …

Siku moja nilipokuwa ujenzini nikaongea na huyo jirani aliyejenga bondeni… kwanza akashangaa maana kwa mtazamo na uelewa wake haoni kama lile ni bonde kiasi cha mtu kutokujenga nyumba… Halafu anasema alipokuwa akinunua kiwanja mjumbe alikuwa mmoja wa mashahidi, na ofisi ya serikali za mitaa ipo mita 20 tu kutoka kiwanjani kwake, kwa nini hawakumwambia pale haparuhusiwi kujenga?

Raia wababe/wenye makosa ni wachache, wengi hawajui hizi sheria za mipango miji na makazi zikoje. Mwananchi wa kawaida ambaye amelala hoi miaka, kudunduliza vipesa vya kununua kiwanja hawezi kununua kiwanja au kujenga mahali ambapo anajua wazi atakuja bomolewa,

Hao wa bandari wameshabomolewa…hatuna la kusema zaidi, lakini mambo yakiendelea hivi baadae watalia wengi
 
Wakazi Kurasini wagoma kuhama

na Deogratius Temba


Walisema mwaka 2006, wakati tathmini ilipofanyika mfuko mmoja wa saruji ulikuwa unauzwa sh 5,000, lakini sasa hivi ni kati ya sh 10,000 na 12,000, hivyo wangepaswa kuongezewa fedha, ili zikidhi gharama za wakati huu na mabadiliko ya gharama za vifaa vya ujenzi.
Pia wakazi hao walilalamikia kauli ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati, kuwa wakazi hao walilipwa sh milioni 20 kila mmoja kama fidia.
Walisema kauli hiyo ya Chiligati si ya kweli, kwani kuna watu waliolipwa mpaka sh milioni 1.5 kwa gharama zote………….

Source: Tanzania Daima

Waliobomolewa nyumba Kurasini wadai waziri amesema uongo
Na Furaha Kijingo


WAKAZI waKurasini Zam Cargo, Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam wamesikitishwa na kauli iliyotolewa bungeni na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati, kwamba kila mmoja amelipwa fidia zaidi ya Sh100m ili kupisha ujenzi wa bandari katika eneo hilo.
Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti wakazi hao walisema kauli ya waziri ni ya uongo kwani hakuna mtu aliyelipwa kiasi cha fedha hizo kati yao na kudai kuwa walizolipwa hazilingani na gharama za ujenzi na hata hadhi ya nyumba zao.
Mkazi wa eneo hilo, Shen Azad Shen(63) alisema, waziri amedanganywa kabisa na kuongeza: "Amekubali kupokea uongo huo, fedha walizosema tumelipwa si kweli, mi nimelipwa Sh16 milioni na nyumba yangu ina zaidi ya thamani ya Sh50 milioni. Kwanini Waziri anadanganywa na anakubali, halafu anakurupuka na kuongea kwa uhakika bungeni?”
Shen alisema hata madai ya kuwa kesi yao inayohusu mgogoro huo wameshindwa si ya kweli kwani bado itasikilizwa tena Oktoba16, mwaka huu katika Mahakama Kuu ya Ardhi.

Naye Abdallah Pogola Abdallah(54) alisema alilipwa ni Sh10 milioni na hata alipojaribu kufuatilia wizarani alipewa mchanganuo mzima wa jinsi atakavyolipwa inaonyesha kwamba alitakiwa kulipwa Sh24 milioni. Naye Mary Kiula alisema kuwa bomoabomoa hiyo haijawatendea haki ikilinganishwa na thamani ya nyumba zao nakudai kwamba kitendo cha askari kwenda na mbwa kuwaondoa kinaashiria kwambawaliobomolewa walikuwa wanadai haki.
''Mimi na wanangu sasa tunakwenda kukaa kwa mdogo wangu, fedha niliyolipwa haitoshi, nilipowauliza walijibu,' si ulipenda mwenyewe kujenga nyumba ya gharama,'' alilalamika Kiula.



Source : Mwananchi

-Inaonekana mawaziri wetu hawachambui vizuri taarifa wanazopelekewa, ambayo kwa kiasi fulani inaichafua serikali na pole pole inajenga watu kuichukia serikali.

-Kuna tuhuma nyingi sana hapo ardhi kuwa kwenye matukio kama haya watendaji wa wizara ya ardhi wanatumia kujitajirisha ....mfano hapo juu evaluation in 24M unlipwa 10M ....nyingine zinakwenda wapi?

-Evaluation zinafanywa leo unalipwa baada ya miaka miwili mpaka mitano ....nadhani hapo kuna jambo la kuwakosea haki wananchi.
 
Kufukuzwa nyumba ya kuishi na kuwa homeless. Kwanza kabisa ni jukumu la serikali kupitia halmashauri za miji kuona kwamba tatizo hili halipo. Kama huna mahali pa kuishi na wewe ni raia wa UK (Yaani sio mgeni wa kutoka nchi nyingine ambayo siyo ya EU ingawa kuna vipengele hapo) ni lazima:

(a) Waweze kukutafutia nyumba ya kuishi.

(b) Wakupatie pesa za kuweza kuishi kama binadamu wengine –kula,
kuvaa na entertainment kama sikosei £35 – 40 kwa wiki, kwa walio chini ya miaka 18 wanapewa nusu ya hizo na unapewa kila wiki.

Unapatiwa masharti ya kuweza kusoma kama hilo ni tatizo na wanaku-link up na sehemu unazoweza kufanya kazi. Wataendelea na jukumu hilo hadi pale utakapoweza kusimama wewe mwenyewe i.e. unaweza kulipa rent bila sokomoko na kama pesa unayolipwa ni kidogo watakuchangia (to-up) hadi pale utakapoweza kama inawezekana. Ukiweza kulipa kodi kila mwezi kwa muda wa miaka mitatu au mitano watakuuzia hiyo nyumba kwa bei ya 60% of the current market price.

Je, inakuwaje unafukuzwa? Kushindwa kulipa kodi ni sababu moja kubwa. Hawawezi kukupa mahali pa kuishi kama huna hati kutoka mahakamani (court order) kuonyesha kwamba wewe ni homeless. Kama halmashauri hawana nyumba watakuweka kwenye bed and breakfast hadi pale watakapoweza kupata mahali pa kukuweka wewe pamoja na familia yako. (ikumbukwe hapa huwezi kupata huduma hizo kama kwenye passport yako wamekugongea NO recourse to public funds). Kwa wageni ni lazima wawe na Indefinite leave to remain ndio wanaweza kupata huduma kama hizo.

Je, wanawezaje kugharimia gharama hizo? Ni rahisi sana – Kodi inayokusanywa na serikali pamoja na halmashauri za miji ndio zinafanya shughuli zote hizo. Vile vile ni jukumu la State kuhakikisha raia wake wanaishi maisha katika level ya kibinadamu. Afrika ni nchi moja tu (Botswana) ambayo imeanza kufanya hilo kwa wazee na wastaafu walio zaidi ya miaka 60 au 65.
TZ kwa nini tunashindwa?

Kodi inayokusanywa inaliwa na MAFISADI wakishirikiana na walafi kutoka ulaya kwa kuwapa tax holiday n.k. Viongozi kuficha pesa za walipa kodi kwenye visiwa vya Gurnsey, Jersey , Switzerland n.k. ili mradi kukwepa jukumu lake. Serikali imeshindwa kutekeleza majukumu yake, kama mnakumbuka ni jukumu la serikali kuona kila mwenye uwezo wa kufanya kazi inafanya kazi na kuona Keki ya taifa inawanufaisha WTZ wote, keki hii inawanufaisha Barrick na Canadians kwenye madini kwa mfano, pesa za EPA zinavyoliwa na magabachori, mikataba mibovu n.k. Ikumbukwe kwamba miaka michache iliyopita yulikuwa na sheria ya serikali kuwahudumia waliomaliza chuo kikuu ambao serikali ilishindwa kuwapa kazi – Je, walikuwepo au ndio kuna walafi wachache walikuwa wanaitafuna hiyo pesa!

Swala la kuvunja makazi bila kuwa na alternative ni uonezi ni sawa na Robert Mugabe alivyofanya kule Zimbabwe na kama mnakumbuka Mama Tibaijuka wa UN alikwenda kule kufuatilia hilo sakata. Je, serikali ya Tanzania ilifanya kila njia kuhakikisha wanaovunjiwa wanaondoa mali zao kwa muda muafaka? Walifuata sheria na kuwaarifu siku ya zoezi hilo? Je, walilipwa malipo halali?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom