Ukiweka other factors constant, na uzalendo aside, kwa mawazo yangu haileti economic sense kujenga bomba la mafuta kupitia Tanga as opposed kupitia Kenya. Ni kama wanyarwanda walivyotaka kupitishia mizigo yao Mombasa badala ya Dar es Salaam. Sijui kama bomba litapitia chini ya Lake Victoria au litazunguka, ila kwa kila hali itakuwa la gharama zaidi kuliko kupitia Kenya. Issue ya fidia ni one time cost na haiwezi kuwa kigezo cha kufanya uamuzi. Gharama za uendeshaji in the long run ndo kigezo muhimu.
Nafikiri sababu kubwa ya waganda kutaka kupitishia bomba kwetu ni usalama tu. Wakenya hawaaminiki kwani katika ule mgogoro wa kile kisiwa wakenya
walingo'a reli ya kwenda Uganda. Hicho waganda hawasahau leo mpaka kesho. Sasa fikiri ni bomba la mafuta linapita, si wangelichoma moto? Wakenya wakifanikiwa kuwapa assurance waganda kuhusu usalama, we might as well kiss this project goodbye.