Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,026
- 20,511
Ninafurahi kuona alichokizungumza Rais Museveni wa Uganda ndio yamekuwa maoni yangu tangu mwanzo juu ya kilichotokea Oktoba 29. 2025. Bahati mbaya kizazi cha Tanzania kwa sasa kimevurugwa na utulivu wa akili umetoweka kabisa, 99.9% ya vijana wanazungumza, wanajadili na kuamua kwa hisia na mihemko kuliko kutumia Akili. Wengi wana taarifa potofu au hawana taarifa kabisa. Kama taifa tunalo jukumu la kuwarudisha vijana na watanzania wote katika msingi wa ukweli, haki na umoja.
Naomba niwarejeshe nyuma, Ukiondoa mradi wa urutubishaji wa madini ya Uranium (Nyuklia) tuliosaini na Urusi wenye thamani ya Dola Bilioni 1.2 ambao umeiingiza katika Vita kali Urusi na Marekani na Ulaya, na kuzalisha chokocho zote zinazoendelea nchini kupitia udhaifu na ufedhuri wa ccm kushindwa kutawala nchi kwa kufuata katiba na sheria za nchi,
Pia Tanzania tuna vita ya muda mrefu zaidi dhidi ya Majirani zetu Kenya ambao walikosa dili la Mafuta ya Uganda ambalo walitaka lipite kwao katika babdari ya Mombasa na badala yake Tanzania tukalichukua dili hilo hadi Bandari ya Tanga. Hivi ni vita vya kiuchumi elewa hivyo ewe kijana na unayeshabikia harakati uchwara bila kutazama nyuma ya pazia.
Kwa Dili hili, Tanzania itapata dola 12 kwa ujazo wa pipa moja la mafuta kutoka serikali ya Uganda, itakapoanza kusafirisha mafuta hayo kwa bomba hadi Bandari ya Tanga. Dola 12 kwa ujazo wa pipa moja ni sawa na 20% ya mauzo ya mafuta kwa pipa katika soko la dunia.
Bomba hilo linatarajiwa kusafirisha ujazo wa mapipa 140,000 kwa siku. Hii inamaana kuwa kwa siku mapipa 140,000 x dola 12 sawa na Tanzania itapata dola 1,680,000 kwa siku. Kwa mwezi chukua $ 1,680,000 x 30 = $ 50,400,000. Kwa mwaka $ 50,400,000 x 12 = $ 604,800,000.
Dola 604,800,000 ni sawa na Shilingi Trilioni 1.5 za kitanzania kwa mwaka. Kwahiyo Tanzania itaingiza Trilioni 1.5 kila mwaka kutokana na bomba la mafuta. Yani mapato yatokanayo na bomba la mafuta yatazidi mapato yatokanayo na sekta zote za uchumi nchini isipokuwa mapato ya sekta ya utalii. Trilioni 1.5 ni sawa na asilimia 5.1% ya budget yetu kwa mwaka.
Kazi nzuri ya Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) ndio ilizaa mradi huu na kuzuia usiende bandari ya Mombasa. Hongera sana TISS kwa kufanikisha mpango huu wenye faida kubwa kiuchumi. Lakini yote kumi, Pongezi za dhati ziende kwa Jasusi mkongwe aliyekuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni Tanzania Mnyaluko Hayati Augustino Mahiga. Kwenye kitabu cha "Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi" nilishauri namna Idara ya Usama wa Taifa (TISS) na idara ya Usalama na Utambuzi Jeshini (MI) zinavyoweza kutumika kwa maslahi ya kiuchumi kwa taifa badala ya kutumika katika miundo ya kizamani ya kijamaa (kisiasa na kuwatumikia wanasiasa).
Miezi ya nyuma zilifanyika juhudi kubwa za maadui kuukwamisha mradi kwa kwenda kwenye kampuni ya Total tuliyoingia nayo mikataba ya kujenga mradi huu na kuitaka Kampuni hiyo iache kufanya kazi hiyo kwakigezo cha uharibifu wa mazingira. Walifika mbali hadi kwenda kushitaki kwenye Shirika la Mazingira Duniani UNEP na UNESCO na kisha kwenda kwa Rais wa Ufaransa huku wakiandamana ili mradi ufe. Majirani wa Kenya Waliwatumia wanaharakati wa ndani chini ya Maria Sarungi kueneza propanda na kila uzushi kujaribu kuzuia mradi huu. vikundi vya mitandaoni vikaandika makala nyingi sana twita na instagram kupotosha juu ya mradi huo. Lakini waafeli.
Watu haohao hatujawahi kuwasikia wakiandamana kupinga ujenzi wa mradi mkubwa wa mabomba marefu zaidi kutoka Urusi hadi barani Ulaya ya Nord Stream 1 & 2. Wala hawajaandamana kupinga ujenzi wa bomba linginge refu zaidi linalojengwa sasahi kutoka Urusi hadi Japan. Lakini kwa Tanzania tunaambiwa tunaharibu mazingira (kumbaaaafu zao!) mradi sasa umefika 84%.
Kama tuliweza kupambana kwenye ujenzi wa mradi wa bwawa la Umeme la Nyerere kule Rufiji ambao hawahawa Wanaharakati walifanya kila njia kukwamisha, hatutashindwa kwa mradi huu. Tujisahihishe tulipojikwaa, tusimame wima tena, Tupambane kuulinda mradi huu usituponyoke kwa vita vya maadui zetu Afrika na Ulaya. Matunda ya mageuzi yanaanza kuonekana, Tusiogope, wala tusiingizwe uoga akilini na mioyoni mwetu.
Na Yericko Nyerere