Bollen Ngetti apatikana huko Segerea

Bollen Ngetti apatikana huko Segerea

HOJA TATU CHANZO CHA KUKAMATWA/KUTEKWA BOLLEN NGETTI.

Bollen Ngetti, Mwanaharakati na Mwandishi wa habari za kiuchunguzi, aliyetekwa tarehe 23/12/2019 siku ya Jumatatu na watu wasiojulikana, kapatikana leo maeneo ya Tabata Segerea baada ya kuachiwa huru na watu hao wasiojulikana.

Bollen Ngetti, amekuwa akitekwa mara kwa mara kwa kipindi hiki cha miaka takribani 4, Mwanaharakati na Mwandishi huyu wa habari za kiuchunguzi ametekwa mara 3 na kutekwa kwake jana ikiwa ni mara ya 4.

KWANINI BOLLEN NGETTI ANATEKWA SANA?

Hizi ni hoja tatu (3) zilizotajwa na Bollen baada ya kutekwa siku ya Jana Tarehe 23 na kuhojiwa hoja hizi tatu ambazo Bollen Ngetti kataja kwamba zimekuwa zikijirudia sana anapotekwa na watu wasiojulikana.

1. Bollen Ngetti kila anapotekwa, amekuwa akiulizwa mahusiano yake ya kikazi na Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje wa Serikali ya awamu ya nne, Ndg. Bernard Kamillus Membe.

2. Bollen Ngetti, anasisitizwa pia kutaja watu anaofanya nao kazi, kazi ambayo watekaji hataki kuiweka wazi!

3. Bollen Ngetti, analazimishwa na watekaji kutaja sehemu ambayo huwa wanafanya vikao, vikao ambavyo Bollen hajui ni kuhusu nini.

Bollen Ngetti anakiri now hayuko sawa kisaikolojia, maana pamoja na kuamua kunyamaza lakini bado amekuwa akiandamwa sana.

Anamalizia kwa kusema "Namuachia Mungu, maana sasa sina amani tena kwenye nchi yangu, naamini ipo siku yatakwisha tu".
Duuh mpka huruma
 
Wamemteka Bollen na kubwa walilomhoji ni mahusiano yake na Bernard Membe anayetishwa kila siku na CCM kwa hisia zao kuwa atajitosa kupambana kuitaka tiketi ya kuteuliwa na chama kugombea Urais.

Hivi hapo kosa lipo wapi? Mbona mnamuogopa hivyo hadi kutumia vyombo vya dola kusumbua watu wengine?

Hii inaonyesha hamuungwi mkono ndani ya CCM kama mnavyotaka kuaminisha huku nje ndio maana mnahaha na kutaabika kunyamazisha kwa vitisho na ubabe kwani mnajua kuwa kukiwa na uchaguzi ni chali tu.

Acheni kutesa watu kwa hisia zenu.

Screenshot_20191224-185120.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Membe naye ndo wale waliolea Mfumo dhalimu , wakati tukiendelea kutubu

Nina maswali
1.Where is Ben
2.Kwanini laini yake ya Simu aliuziwa Mwingine
3.Kwanini hasa kwa nini
 
Membe naye ndo wale waliolea Mfumo dhalimu , wakati tukiendelea kutubu

Nina maswali
1.Where is Ben
2.Kwanini laini yake ya Simu aliuziwa Mwingine
3.Kwanini hasa kwa nini
Membe ni wale wale lakini bado najiuliza inakuwaje wanasema hawamuogopi lakini wanateka vijana wengine ili kuwauliza ya Membe wakati wamemuita kamati ya maadili.
Hivi huyo anayetaka kunyang'anywa na Membe nafasi ya kugombea hawezi jitetea mwenyewe kwa kuonyesha anafaa hadi vibaraka watumie ofisi zao na nguvu kubwa kumsimamisha Membe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Membe akikubali kwenda kuhojiwa tu Basi watamkolimba, bora atulie tu
 
Kisu kimeanza kukata mfupa (membe) atafikiwa tu ,jipe muda

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Atafikiwa ili iweje? Kwamba Hana haki ya kugombea nafasi yoyote ya kiuongozi ccm? Na Kama ndio, ni kwanini njia ya kidemokrasia isitumike kuwapata viongozi huko ccm kwa maana ya kupigiwa kura kwa wahitaji? Ngoja nisubiri kuuona udikteta unavyotamalaki ccm huku wakiwanyooshea vidole wengine!
 
Membe naye ndo wale waliolea Mfumo dhalimu , wakati tukiendelea kutubu

Nina maswali
1.Where is Ben
2.Kwanini laini yake ya Simu aliuziwa Mwingine
3.Kwanini hasa kwa nini
Kamuulize Membe mwenyewe!
 
Inasikitisha kwakweli.
Lakini Bollen Ngeti ajuwe akitaka kuingia kwenye siasa iwe kwa uandishi au harakati zozote basi ajiandae na akubaliane na mashambulizi ya kila namna kama vile yeye anavyo washambulia watu kwa namna anayoweza yeye yaani kutumia uandishi.
Vingineyo aandike vitu vingine kama waandishi wenzie wasiokumbana na misukosuko kama yake.

Asishambulie watu kwa uandishi na kutegemea hatashambuliwa kujibiwa mashambulizi, wenzie anao washambulia wao wana njia zingine tofauti na uandishi.
Asitafute huruma toka kwa wananchi, akianzisha vita basi apambane mwenyewe.
Kama ametaka kuwa shujaa ni vizuri sasa aendelee na vita alivyo anzisha na sio kuja kulialia. Akifanikiwa itakuwa faida yake binafsi na familia yake.
Huenda hata ameahidiwa kuwa waziri wa habari au afisa habari wa ofisi kubwa kabisa. Mtaka cha uvunguni lazima ....
Wakati mwingine hoja zenu zinakuwa kama za makafiri fulani hivi!!! Yaani mtu akiwa na hoja tofauti juu ya mwingine basi jawabu ni utekaji na si kwenda mahakamani kushtaki!!!? Yaani tupo kwenye "Law of the jungle" katika serikali ya awamu ya tano. Kwamba ukiwa na mawazo yaliyo tofauti na mtawala basi wewe umeingia vitani dhidi ya serikali!!? Kweli tuko Misri, lini tutaiona Kaanani, Mungu anajua!!!
 
Membe, endelea kuwavuruga hao wakuja mpaka wapoteane! Unatambua fika kuna mtu "mzito" yuko nyuma yako hivyo hawana cha kukufanya, zaidi tu wataishia kukutishia nyau.
 
Back
Top Bottom