Bollen Ngetti apatikana huko Segerea

Bollen Ngetti apatikana huko Segerea

HOJA TATU CHANZO CHA KUKAMATWA/KUTEKWA BOLLEN NGETTI.

Bollen Ngetti, Mwanaharakati na Mwandishi wa habari za kiuchunguzi, aliyetekwa tarehe 23/12/2019 siku ya Jumatatu na watu wasiojulikana, kapatikana leo maeneo ya Tabata Segerea baada ya kuachiwa huru na watu hao wasiojulikana.

Bollen Ngetti, amekuwa akitekwa mara kwa mara kwa kipindi hiki cha miaka takribani 4, Mwanaharakati na Mwandishi huyu wa habari za kiuchunguzi ametekwa mara 3 na kutekwa kwake jana ikiwa ni mara ya 4.

KWANINI BOLLEN NGETTI ANATEKWA SANA?

Hizi ni hoja tatu (3) zilizotajwa na Bollen baada ya kutekwa siku ya Jana Tarehe 23 na kuhojiwa hoja hizi tatu ambazo Bollen Ngetti kataja kwamba zimekuwa zikijirudia sana anapotekwa na watu wasiojulikana.

1. Bollen Ngetti kila anapotekwa, amekuwa akiulizwa mahusiano yake ya kikazi na Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje wa Serikali ya awamu ya nne, Ndg. Bernard Kamillus Membe.

2. Bollen Ngetti, anasisitizwa pia kutaja watu anaofanya nao kazi, kazi ambayo watekaji hataki kuiweka wazi!

3. Bollen Ngetti, analazimishwa na watekaji kutaja sehemu ambayo huwa wanafanya vikao, vikao ambavyo Bollen hajui ni kuhusu nini.

Bollen Ngetti anakiri now hayuko sawa kisaikolojia, maana pamoja na kuamua kunyamaza lakini bado amekuwa akiandamwa sana.

Anamalizia kwa kusema "Namuachia Mungu, maana sasa sina amani tena kwenye nchi yangu, naamini ipo siku yatakwisha tu".
Alhamdullilah
 
Kokoto ni muoga kama matako ya kicheche

Akistuliwa kidogo tu,amehara!

Majitu yasiyo na akili hata yawe na madaraka kama “mungu” bado yatakua majinga tu!

Ujinga hauondolewi kwakua na madaraka!
Kumbe haya yote ni kwa sababu ya Membe???

jamaa ni mwoga sana.
 
Kumbe sababu kubwa ni Membe hivi Magufuli zimwo kweli?

Unamuogopa Membe ili iweje kwa mfano wakati una kila kitu?

Wewe ni rais, majeshi polisi TISS yote yako chama pia wewe ni mwenyekiti si umfukuze Membe uwanachama?
Ingawa wanasema tusikosoe kwa kejeli nawaza nawezaje kumkosa kwa staha mtu kama JPM??
 
Inasikitisha kwakweli.
Lakini Bollen Ngeti ajuwe akitaka kuingia kwenye siasa iwe kwa uandishi au harakati zozote basi ajiandae na akubaliane na mashambulizi ya kila namna kama vile yeye anavyo washambulia watu kwa namna anayoweza yeye yaani kutumia uandishi.
Vingineyo aandike vitu vingine kama waandishi wenzie wasiokumbana na misukosuko kama yake.

Asishambulie watu kwa uandishi na kutegemea hatashambuliwa kujibiwa mashambulizi, wenzie anao washambulia wao wana njia zingine tofauti na uandishi.
Asitafute huruma toka kwa wananchi, akianzisha vita basi apambane mwenyewe.
Kama ametaka kuwa shujaa ni vizuri sasa aendelee na vita alivyo anzisha na sio kuja kulialia. Akifanikiwa itakuwa faida yake binafsi na familia yake.
Huenda hata ameahidiwa kuwa waziri wa habari au afisa habari wa ofisi kubwa kabisa. Mtaka cha uvunguni lazima ....
Tatizo linakuja pale nchi inapoacha mambo yote na kuanza kumobiluze resources kumshambulia Ngeti Mmoa tena asiye na siraha. Hivi Kweli Ngeti ni wa kushambuliwa na serikali nzima?
 
Tatizo linakuja pale nchi inapoacha mambo yote na kuanza kumobiluze resources kumshambulia Ngeti Mmoa tena asiye na siraha. Hivi Kweli Ngeti ni wa kushambuliwa na serikali nzima?
Unasema Ngeti mmoja asiye na silaha???!!
Kwani silaha ni nini?
Maneno ni silaha kubwa mno, kalamu ni silaha kubwa inayo weza kukusanya mamilioni ya askari wa kiwango cha kujitoa muhanga kabisa.
Achana na the power of spoken or written words.
Maneno ya Adolf Hitler yalisababisha vita kuu ya pili ya dunia na kuuwa mamilioni ya watu kisha kubadilisha kabisa mfumo wa maisha ya binadamu dunia nzima.
Maneno yalitosha kuuwa wayahudi zaidi ya milioni 6.
Maneno yalisababisha mauwaji ya halaiki Rwanda na Burundi.
Maneno yame muondoa madarakani Albashir wa Sudan, hakitumika bunduki wala bomu kumuondoa.
Maneno ya uongo toka kwa viongozi wao yalisababisha waingereza na wamarekani wakubali askari wao wakavamie Iraq na kuivuruga nchi hadi kesho.

Waandishi wana nafasi kubwa sana kutumia silaha ya maneno ktk maandishi yao au matangazo yao ya sauti.
 
Mkuu yule si mwandishi wa habari za kiuchunguzi.
Yule ni mchambuzi wa mambo ya kisiasa.

Anyway lets get back to the point. Tufanye yeye ni muandishi wa habari za kiuchunguzi. Hivyo anajuwa anachokifanya ni kama kutembea kwenye eneo ambalo watu wanapigana vita huku risasi zikirushwa ovyo. He may find himself caught in cross fire.
Kama hiyo ni taaluma yake aliyo somea anapaswa kujua ni kazi ya hatari sana sababu unachezea ulaji/maslahi ya watu.
Katika kulielewa hilo watu waliosomea taaluma hiyo ya habari za kiuchunguzi kuna protocol (sijui niite protokali au itifaki) flani zimewekwa ili kujilinda usidhuriwe kirahisi kama inavyotokea kwake.

Umeona jinsi mwandishi fulani wa 'Ze-ikonomi' alivyo chukuliwa kwa shida nyumbani kwake kiasi kwamba ilibidi walio mchukuwa waseme wamechukua na hakudhuriwa?
Uliwaona wale waandishi wa kimataifa watetezi wa waandishi wa habari sijui toka SA na nchi jirani walivyo chukuliwa kwa shida na kurudishwa kwa namna ile?

Sababu kubwa hao walikuwa wanajua protocol na walizifuata.
Sio kama huyu Bollen Ngeti mara kadhaa anatekwa(au anasingizia kutekwa) kirahisi sana na kurudishwa kirahisi mno, huyu anatumiwa na wajanja ambao nao ni makanjanja wanamuuza kwa kutompa ulinzi.

What I was doing in that comment is just stating the obvious, kwamba kazi anayofanya anajuwa ni ya hatari na nini kitamtokea hivyo hasipo chukuwa hatua au tahadhari yakimkuta yanayo mkuta hatakiwi kuja kulia lia kwa wananchi. Ipo siku anaweza kudhuriwa pakubwa na hata wananchi wakija kumlilia haitabadili kitu atakuwa kashamezwa na chatu hawezi au watu hawawezi kubadili kitu.

Alafu hapa lazima tuweke ukweli mmoja wazi, kuna mstari mdogo sana kati ya kuandika kwa malengo ya kulikomboa taifa na kuandika sababu ya kufanya propaganda za kumsaidia mtu flani ashike dola nawewe upate shibe yako na familia yako.
Waandishi njaa na vijarida au vigazeti uchwara vipo vingi sana, hasa baada ya kuzaliwa wanamtandao. Na vyama vingi vya vya siasa kupata pesa toka kwa mabeberu ya kuanzisha vijarida vya propaganda.

Siasa ni vita, ukijiingiza ktk siasa kwa namna yeyote ile ujue unajiingiza ktk vita.

Kuna mwana nadharia wa kivita wa kijerumani aitwae Carl von Clausewitz alipendekeza tafsiri ya vita iwe ni "Vita ni muendelezo wa siasa kwa njia nyingine"
Kwa namna hiyo kimantiki utaona kumbe siasa ni vita ktk njia nyingine au ktk sura nyingine.

Kama tukitafsiri siasa ni vita basi inabidi ukubaliane na nadharia nyingine ambayo ni ukweli tupu kwamba na hapa namnukuu tena Carlo von Clausewitz
"watu wenye moyo mwema wanafikiri bila shaka kuna njia ya busara ya kumpokonya sila na kumshinda adui yako bila kumwaga damu nyingi, na huweza kudhania kwamba haya ndio hasa malengo halisi ya vita, Dhana hii hata ipendeze vipi masikioni mwa watu lakini sio dhana sahihi na uongo unaopaswa kuwekwa bayana. Vita ni biashara hatari sana kwamba makosa yatokanayo na fadhili(roho njema kwenye vita yoyote) ndio mabaya zaidi"

Maana yake nini hapa? Usitegemee fadhila toka kwa adui yako, pigana kwa mbinu au njia zozote umshinde adui wako, ushinde vita. Inashangaza kuona watu wengi hapa wanataka upande mmoja wa wanaopigana vita vya kupigania dola/madaraka uwe unawapa fadhila washindani(adui) wake. Atumie mbinu au njia safi huku yeye akiwekewa hadi sumu na kuombewa afe.
Au awape adui zake fadhila huku hao adui wanatafuta wafadhili (mabeberu) waje wammalize anae takiwa kutoa fadhila kama alivyomalizwa Ghadaf au Saddam Hussein.

Vita haijui mipaka (War knows no boundaries) hivyo huwezi kumpangia adui yako mipaka au mbinu za kushinda vita dhidi yako, hakuna huruma ktk vita. Ukiingia vitani hakuna huruma wala busara zaidi ya kuhakikisha unashinda vita. Iwe kwa kutumia bunduki, maneno ya mdomoni au kalamu kwenye maandishi ya vitabuni, mitandaoni au magazetini.

Mfadhili wa Bollen Ngeti kama angepata nafasi ya kumuondoa adui wake ofisi kuu hata kwa kumuondoa duniani kwa sumu au risasi angeitumia nafasi hiyo haraka sana, vivyo hivyo huyo mtu/watu wa ofisi kuu akipata/wakipata nafasi ya kumshinda Bollen Ngeti na/au mfadhili wake basi ataitumia/wataitumia hiyo nafasi by any means necessary.
Hata kama sikubaliani na maudhui ya andiko lako 100℅ lakini kuna logic. Wakati mwingine tujifunze kukubali kutokubaliana.
 
Ka
Unasema Ngeti mmoja asiye na silaha???!!
Kwani silaha ni nini?
Maneno ni silaha kubwa mno, kalamu ni silaha kubwa inayo weza kukusanya mamilioni ya askari wa kiwango cha kujitoa muhanga kabisa.
Achana na the power of spoken or written words.
Maneno ya Adolf Hitler yalisababisha vita kuu ya pili ya dunia na kuuwa mamilioni ya watu kisha kubadilisha kabisa mfumo wa maisha ya binadamu dunia nzima.
Maneno yalitosha kuuwa wayahudi zaidi ya milioni 6.
Maneno yalisababisha mauwaji ya halaiki Rwanda na Burundi.
Maneno yame muondoa madarakani Albashir wa Sudan, hakitumika bunduki wala bomu kumuondoa.
Maneno ya uongo toka kwa viongozi wao yalisababisha waingereza na wamarekani wakubali askari wao wakavamie Iraq na kuivuruga nchi hadi kesho.

Waandishi wana nafasi kubwa sana kutumia silaha ya maneno ktk maandishi yao au matangazo yao ya sauti.
Kama nilivyosema awali hata kama mtu hakubaliani na maudhui ya andiko lako lakini kuna hoja,huwezi kupuuza.Tujifunze kukubali kutokubaliana!
 
Hata kama sikubaliani na maudhui ya andiko lako 100℅ lakini kuna logic. Wakati mwingine tujifunze kukubali kutokubaliana.
Hakika hii ndio demokrasia umehubiri kwa vitendo. Tukubaliane kutokubaliana.
Mimi mwenyewe sipendi kabisa haya mambo ya kutekana na kutesana lakini wanao tekwa wachukue tahadhari kujilinda na sio kutegemea watanzania wanafiki na hash tag za #freeFlani wakiombwa waandame hawatoki ndani hata hatua moja.
 
Hayo ya kumuachia Mungu yanamchefusha Karl Marx huko aliko. Pambana na hali yako!
 
Inasikitisha kwakweli.
Lakini Bollen Ngeti ajuwe akitaka kuingia kwenye siasa iwe kwa uandishi au harakati zozote basi ajiandae na akubaliane na mashambulizi ya kila namna kama vile yeye anavyo washambulia watu kwa namna anayoweza yeye yaani kutumia uandishi.
Vingineyo aandike vitu vingine kama waandishi wenzie wasiokumbana na misukosuko kama yake.

Asishambulie watu kwa uandishi na kutegemea hatashambuliwa kujibiwa mashambulizi, wenzie anao washambulia wao wana njia zingine tofauti na uandishi.
Asitafute huruma toka kwa wananchi, akianzisha vita basi apambane mwenyewe.
Kama ametaka kuwa shujaa ni vizuri sasa aendelee na vita alivyo anzisha na sio kuja kulialia. Akifanikiwa itakuwa faida yake binafsi na familia yake.
Huenda hata ameahidiwa kuwa waziri wa habari au afisa habari wa ofisi kubwa kabisa. Mtaka cha uvunguni lazima ....
I appreciate mkuu, mwanaharakat unakuw umejitolea kwa kila kitu, kufa, kuchinjwa, kuliwa......😂😂, Sasa yeye alianza hzo harakat na anajua impact yake, syo Tz tuu n dunian kote, America tunayoiona et wana democracy but fuatilia what happened kwa kina Martin Luther Jr na wengine kibaooo, akae kwa kutulia amalize alichokianzisha😂😂😂
 
Back
Top Bottom