HOJA TATU CHANZO CHA KUKAMATWA/KUTEKWA BOLLEN NGETTI.
Bollen Ngetti, Mwanaharakati na Mwandishi wa habari za kiuchunguzi, aliyetekwa tarehe 23/12/2019 siku ya Jumatatu na watu wasiojulikana, kapatikana leo maeneo ya Tabata Segerea baada ya kuachiwa huru na watu hao wasiojulikana.
Bollen Ngetti, amekuwa akitekwa mara kwa mara kwa kipindi hiki cha miaka takribani 4, Mwanaharakati na Mwandishi huyu wa habari za kiuchunguzi ametekwa mara 3 na kutekwa kwake jana ikiwa ni mara ya 4.
KWANINI BOLLEN NGETTI ANATEKWA SANA?
Hizi ni hoja tatu (3) zilizotajwa na Bollen baada ya kutekwa siku ya Jana Tarehe 23 na kuhojiwa hoja hizi tatu ambazo Bollen Ngetti kataja kwamba zimekuwa zikijirudia sana anapotekwa na watu wasiojulikana.
1. Bollen Ngetti kila anapotekwa, amekuwa akiulizwa mahusiano yake ya kikazi na Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje wa Serikali ya awamu ya nne, Ndg. Bernard Kamillus Membe.
2. Bollen Ngetti, anasisitizwa pia kutaja watu anaofanya nao kazi, kazi ambayo watekaji hataki kuiweka wazi!
3. Bollen Ngetti, analazimishwa na watekaji kutaja sehemu ambayo huwa wanafanya vikao, vikao ambavyo Bollen hajui ni kuhusu nini.
Bollen Ngetti anakiri now hayuko sawa kisaikolojia, maana pamoja na kuamua kunyamaza lakini bado amekuwa akiandamwa sana.
Anamalizia kwa kusema "Namuachia Mungu, maana sasa sina amani tena kwenye nchi yangu, naamini ipo siku yatakwisha tu".