Bollen Ngetti apatikana huko Segerea

Bollen Ngetti apatikana huko Segerea

Inasikitisha kwakweli.
Lakini Bollen Ngeti ajuwe akitaka kuingia kwenye siasa iwe kwa uandishi au harakati zozote basi ajiandae na akubaliane na mashambulizi ya kila namna kama vile yeye anavyo washambulia watu kwa namna anayoweza yeye yaani kutumia uandishi.
Vingineyo aandike vitu vingine kama waandishi wenzie wasiokumbana na misukosuko kama yake.

Asishambulie watu kwa uandishi na kutegemea hatashambuliwa kujibiwa mashambulizi, wenzie anao washambulia wao wana njia zingine tofauti na uandishi.
Asitafute huruma toka kwa wananchi, akianzisha vita basi apambane mwenyewe.
Kama ametaka kuwa shujaa ni vizuri sasa aendelee na vita alivyo anzisha na sio kuja kulialia. Akifanikiwa itakuwa faida yake binafsi na familia yake.
Huenda hata ameahidiwa kuwa waziri wa habari au afisa habari wa ofisi kubwa kabisa. Mtaka cha uvunguni lazima ....
Hivi ulivyoamua kuandika hii habari ama comment umefikiria ama umejurupuka?
 
Kumbe sababu kubwa ni Membe hivi Magufuli zimwo kweli?

Unamuogopa membe ili iweje kwa mfano wakati una kila kitu?

Wewe ni rais, majeshi polisi TISS yote yako chama pia wewe ni mwenyekiti si umfukuze Membe uwanachama?

Magufuli anaingiaje Hapa.
 
Hivi ulivyoamua kuandika hii habari ama comment umefikiria ama umejurupuka?
Nimefikiria lakini nimefikiria tofauti na wewe mkuu wangu.
Si ndio nimetumia uhuru wangu wa mawazo, kuandika au kuongea kama mnavyotaka?
 
Nimefikiria lakini nimefikiria tofauti na wewe mkuu wangu.
Si ndio nimetumia uhuru wangu wa mawazo, kuandika au kuongea kama mnavyotaka?
Nimekuuliza hili swali sababu kwenye comment yako umeitaja kazi yake na mwisho unasema ati anataka huruma ya wananchi kwa kushambulia watu. Unless unajua nini kazi ya mwandishi wa habari za uchunguzi huwezi kuandika ulichokiandika. Kwa taaluma nyingine sijui ungeuliza kwanini mpasuaji hakubaki kuwa GP tu agawe vidonge na kuchoma watu sindano badala ya ku specialise. Comment yangu hakumaanisha kukushusha hadhi bali kukuasa kuthamini taaluma za wstu. Martin Luther King II kulikua na watu kama ninyi walikua wanamdhihaki lakini leo hii wote mnaunua umujimu wake
 
Nimekuuliza hili swali sababu kwenye comment yako umeitaja kazi yake na mwisho unasema ati anataka huruma ya wananchi kwa kushambulia watu. Unless unajua nini kazi ya mwandishi wa habari za uchunguzi huwezi kuandika ulichokiandika. Kwa taaluma nyingine sijui ungeuliza kwanini mpasuaji hakubaki kuwa GP tu agawe vidonge na kuchoma watu sindano badala ya ku specialise. Comment yangu hakumaanisha kukushusha hadhi bali kukuasa kuthamini taaluma za wstu. Martin Luther King II kulikua na watu kama ninyi walikua wanamdhihaki lakini leo hii wote mnaunua umujimu wake
Mkuu yule si mwandishi wa habari za kiuchunguzi.
Yule ni mchambuzi wa mambo ya kisiasa.

Anyway lets get back to the point. Tufanye yeye ni muandishi wa habari za kiuchunguzi. Hivyo anajuwa anachokifanya ni kama kutembea kwenye eneo ambalo watu wanapigana vita huku risasi zikirushwa ovyo. He may find himself caught in cross fire.
Kama hiyo ni taaluma yake aliyo somea anapaswa kujua ni kazi ya hatari sana sababu unachezea ulaji/maslahi ya watu.
Katika kulielewa hilo watu waliosomea taaluma hiyo ya habari za kiuchunguzi kuna protocol (sijui niite protokali au itifaki) flani zimewekwa ili kujilinda usidhuriwe kirahisi kama inavyotokea kwake.

Umeona jinsi mwandishi fulani wa 'Ze-ikonomi' alivyo chukuliwa kwa shida nyumbani kwake kiasi kwamba ilibidi walio mchukuwa waseme wamechukua na hakudhuriwa?
Uliwaona wale waandishi wa kimataifa watetezi wa waandishi wa habari sijui toka SA na nchi jirani walivyo chukuliwa kwa shida na kurudishwa kwa namna ile?

Sababu kubwa hao walikuwa wanajua protocol na walizifuata.
Sio kama huyu Bollen Ngeti mara kadhaa anatekwa(au anasingizia kutekwa) kirahisi sana na kurudishwa kirahisi mno, huyu anatumiwa na wajanja ambao nao ni makanjanja wanamuuza kwa kutompa ulinzi.

What I was doing in that comment is just stating the obvious, kwamba kazi anayofanya anajuwa ni ya hatari na nini kitamtokea hivyo hasipo chukuwa hatua au tahadhari yakimkuta yanayo mkuta hatakiwi kuja kulia lia kwa wananchi. Ipo siku anaweza kudhuriwa pakubwa na hata wananchi wakija kumlilia haitabadili kitu atakuwa kashamezwa na chatu hawezi au watu hawawezi kubadili kitu.

Alafu hapa lazima tuweke ukweli mmoja wazi, kuna mstari mdogo sana kati ya kuandika kwa malengo ya kulikomboa taifa na kuandika sababu ya kufanya propaganda za kumsaidia mtu flani ashike dola nawewe upate shibe yako na familia yako.
Waandishi njaa na vijarida au vigazeti uchwara vipo vingi sana, hasa baada ya kuzaliwa wanamtandao. Na vyama vingi vya vya siasa kupata pesa toka kwa mabeberu ya kuanzisha vijarida vya propaganda.

Siasa ni vita, ukijiingiza ktk siasa kwa namna yeyote ile ujue unajiingiza ktk vita.

Kuna mwana nadharia wa kivita wa kijerumani aitwae Carl von Clausewitz alipendekeza tafsiri ya vita iwe ni "Vita ni muendelezo wa siasa kwa njia nyingine"
Kwa namna hiyo kimantiki utaona kumbe siasa ni vita ktk njia nyingine au ktk sura nyingine.

Kama tukitafsiri siasa ni vita basi inabidi ukubaliane na nadharia nyingine ambayo ni ukweli tupu kwamba na hapa namnukuu tena Carlo von Clausewitz
"watu wenye moyo mwema wanafikiri bila shaka kuna njia ya busara ya kumpokonya sila na kumshinda adui yako bila kumwaga damu nyingi, na huweza kudhania kwamba haya ndio hasa malengo halisi ya vita, Dhana hii hata ipendeze vipi masikioni mwa watu lakini sio dhana sahihi na uongo unaopaswa kuwekwa bayana. Vita ni biashara hatari sana kwamba makosa yatokanayo na fadhili(roho njema kwenye vita yoyote) ndio mabaya zaidi"


Maana yake nini hapa? Usitegemee fadhila toka kwa adui yako, pigana kwa mbinu au njia zozote umshinde adui wako, ushinde vita. Inashangaza kuona watu wengi hapa wanataka upande mmoja wa wanaopigana vita vya kupigania dola/madaraka uwe unawapa fadhila washindani(adui) wake. Atumie mbinu au njia safi huku yeye akiwekewa hadi sumu na kuombewa afe.
Au awape adui zake fadhila huku hao adui wanatafuta wafadhili (mabeberu) waje wammalize anae takiwa kutoa fadhila kama alivyomalizwa Ghadaf au Saddam Hussein.

Vita haijui mipaka (War knows no boundaries) hivyo huwezi kumpangia adui yako mipaka au mbinu za kushinda vita dhidi yako, hakuna huruma ktk vita. Ukiingia vitani hakuna huruma wala busara zaidi ya kuhakikisha unashinda vita. Iwe kwa kutumia bunduki, maneno ya mdomoni au kalamu kwenye maandishi ya vitabuni, mitandaoni au magazetini.

Mfadhili wa Bollen Ngeti kama angepata nafasi ya kumuondoa adui wake ofisi kuu hata kwa kumuondoa duniani kwa sumu au risasi angeitumia nafasi hiyo haraka sana, vivyo hivyo huyo mtu/watu wa ofisi kuu akipata/wakipata nafasi ya kumshinda Bollen Ngeti na/au mfadhili wake basi ataitumia/wataitumia hiyo nafasi by any means necessary.
 
Hi
HOJA TATU CHANZO CHA KUKAMATWA/KUTEKWA BOLLEN NGETTI.

Bollen Ngetti, Mwanaharakati na Mwandishi wa habari za kiuchunguzi, aliyetekwa tarehe 23/12/2019 siku ya Jumatatu na watu wasiojulikana, kapatikana leo maeneo ya Tabata Segerea baada ya kuachiwa huru na watu hao wasiojulikana.

Bollen Ngetti, amekuwa akitekwa mara kwa mara kwa kipindi hiki cha miaka takribani 4, Mwanaharakati na Mwandishi huyu wa habari za kiuchunguzi ametekwa mara 3 na kutekwa kwake jana ikiwa ni mara ya 4.

KWANINI BOLLEN NGETTI ANATEKWA SANA?

Hizi ni hoja tatu (3) zilizotajwa na Bollen baada ya kutekwa siku ya Jana Tarehe 23 na kuhojiwa hoja hizi tatu ambazo Bollen Ngetti kataja kwamba zimekuwa zikijirudia sana anapotekwa na watu wasiojulikana.

1. Bollen Ngetti kila anapotekwa, amekuwa akiulizwa mahusiano yake ya kikazi na Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje wa Serikali ya awamu ya nne, Ndg. Bernard Kamillus Membe.

2. Bollen Ngetti, anasisitizwa pia kutaja watu anaofanya nao kazi, kazi ambayo watekaji hataki kuiweka wazi!

3. Bollen Ngetti, analazimishwa na watekaji kutaja sehemu ambayo huwa wanafanya vikao, vikao ambavyo Bollen hajui ni kuhusu nini.

Bollen Ngetti anakiri now hayuko sawa kisaikolojia, maana pamoja na kuamua kunyamaza lakini bado amekuwa akiandamwa sana.

Anamalizia kwa kusema "Namuachia Mungu, maana sasa sina amani tena kwenye nchi yangu, naamini ipo siku yatakwisha tu".
Hizi ni drama za kijinga kabisa kuwahi kutokea,kwamba eti anatekwa then anaachiliwa huru (anakuwa dumped somewhere)
Eti anaulizwa maswali kumhusu Benard Membe,Eti anaulizwa Membe huwa anawasiliana na nani,kweli kabisa na nyie mnaamini huu upuuzi wa huyu jamaa?Eti huwa mnakutana wapi mnaongea nini?
Hivi kweli,Membe kama anaweza kuwa hacked na watu wanaingilia mawasiliano yake wanashindwa kujua anawasiliana na kina nani na wanaongea nini na wanakutana wapi? Kwamba Bollen anatekwaga na watu wa idara?halafu wanamwachia kifalafala hivyo?
Trust me kama huyu jamaa anatamani kutekwa na watu wa idara basi asubili tu na siku hiyo ndo atajua uzushi na kutafuta sifa kwa jina la kitengo yalikuwa makosa makubwa katika maisha yake.
 
Membe, endelea kuwavuruga hao wakuja mpaka wapoteane! Unatambua fika kuna mtu "mzito" yuko nyuma yako hivyo hawana cha kukufanya, zaidi tu wataishia kukutishia nyau.
Kuku akishanyonyolewa mabawa yake hana ujanja
 
Na ndiyo maana Mungu huwa hachukui hatua yoyote kwakuwa huwa anaona ni wazembe kabisa. Mambo wanayoweza kuyasema na kuyafanya wao wenyewe wanamwachiaje Mungu? Mungu ana kazi nyingi hawezi kupokea kazi ndogo ndogo ambazo binadamu anaweza kuzifanya ndiyo maana akatupa akili na maarifa sasa kama hatuzitumii ni ujinga wetu siyo tena kuanza kumwachia yeye kazi huo ni utovu wa nidhamu
Tatizo la hawa wanaotekwa ni hiyo kauli yao ya kumwachia Mungu...
Siku zote Mungu yupo bize sana..
Sasa utamuachiaje mambo yanayosababishwa na binadamu (m)wenzako...??
Hivi hii ni theolojia ya wapi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamhuri imfungulie mashtaka kama Nondo
Kama katekwa mara 4 na bado anaachwa akiwa hai, basi hii inaleta maswali kadhaa;

1. Kuwa, hivi iweje huyu Mwandishi anatekwa mara 4 na bado anakuwa hajifunzi tu namna ya kujilinda mwenyewe kwa maana ya self defense?

2. Na iweje hawa watekaji wamteke mara 4 na wakiwa na madai yaleyale yasiyo na majibu??

å Yaani wamteka mara ya kwanza kwa madai yaleyale, hawakupata jibu....wakamuachia....!!

å Mara ya pili, madai yaleyale, hawakupata jibu wakamwachia....!!

å Mara ya tatu, madai yaleyale, hawakupata majibu kwa mtu yuleyule, wakamuachia....!!

å Na sasa ni mara ya NNE, madai yaleyale, wakamuachia bila kumdhuru ikiwemo kuuwawa ama kupotezwa kabisa kama kina Ben Sanane ama Kagomba....!!

JAMANI tujiulize hivi ina - make sense kweli juu hiki kinachoitwa utekaji kwa staili hii??

Je, siyo mchezo fulani tu wenye nia na malengo fulani?

Hii maana yake tutegemee huyu jamaa kutekwa kwa mara ya 5 huku watekaji wakiwa na madai yaleyale ambayo huyu mtekwaji hawezi kuwapatia majibu yake....

Na kwanini serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama hususani jeshi la polisi wameshindwa kukomesha tabia hii ambayo kwa viwango vyote inaipa nchi yetu ya Tanzania taswira mbaya ktk anga za kimataifa?

Ama vyombo vyenyewe hivi ndivyo vinahusika na ujinga huu wa kuteka watu hovyo hovyo??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tutakutumia kama shahidi upande mashtaka tutakapo mshtaki kwa kutoa taarifa za uwongo inaonekana unajua habari zake sana
Mambo mengne bhana ni kujichosha tu.
Mtu anaondoka nyumban kwake anazima simu zake anaenda kwa mchepuko wake wajinga wanaanza kutangaza ametekwa.

Mashuhuda wakat anatekwa ni akina nani?
Yaani jamaa kaenda kwa mchepuko wake kalala siku moja anaweka defence kwa mke wake kwamba katekwa na mijitu inaamini ametekwa..
Kizazi hiki kina shida kweli

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom