Boflo enzi zake.....

Boflo enzi zake.....

Sikonge

Platinum Member
Joined
Jan 19, 2008
Posts
11,635
Reaction score
6,238
Boflo,

Hapa ulikuwa barabara ipi? Bofloooooooo.........

bonk-boflo.jpg
 
Last edited by a moderator:
Sikonge hiyo ni UDA?...plate No naona kama ya Kenya? Na hapo pamekaa kama station..

Bongo imechange sana majengo/population/kila kitu
 
Nadhani hapo ni kenya. Tanzania basi kama hili haliruhusiwi kutoa huduma.
 
Mkuu unanikumbusha mbali,hiyo ilikuwa barabara ya SIKONGE,nilikuwa naelekea TUTUO!
 
hii mikate tulikua tunaigonga na maji baridi halafu unalamba sukari na majani kisha unakaa juani (chai inaivia tumboni)
 
alianzia huku kabla ya kwenda kwenye lami

basi.jpg
 

Attachments

  • saleee.jpg
    saleee.jpg
    52.5 KB · Views: 61
Hahahaa, Kumbe wewe kweli ni Tukutuku. Mitaa ya kwetu hiyo. Tutuo pamechangamka sana sana kwa sasa na hasa Kabanga, sijui kwa nini? Huku kwa Waarabu yaani ilipokuwa Stand ya Mabasi zamani pamepooza sana. Itabidi na mie nitafute kiwanja hapo Tutuo.

Tutuo.JPGKabanga.JPG
Mkuu unanikumbusha mbali,hiyo ilikuwa barabara ya SIKONGE,nilikuwa naelekea TUTUO!
 
Hahahaa, Kumbe wewe kweli ni Tukutuku. Mitaa ya kwetu hiyo. Tutuo pamechangamka sana sana kwa sasa na hasa Kabanga, sijui kwa nini? Huku kwa Waarabu yaani ilipokuwa Stand ya Mabasi zamani pamepooza sana. Itabidi na mie nitafute kiwanja hapo Tutuo.

View attachment 71880View attachment 71881
Ni jambo zuri sana kuendeleza miji yetu na tena umenikumbusha mbali sana.Mambo ya ipole,inyonga,Mtakuja na mto ugalla kwenye samaki nayamiss sana kwa kweli!Nasikia siku izi inyonga imeamishiwa wilaya ya Mlale mkoa wa katavi!
 
Inawezekana ingawa kusema ukweli mie kwa kwenda Ipole, mwisho wangu ni Chabutwa na huku upande mwingine niliishia Kiloleli na zaidi ya hapo, siyo mwenyeji sana wa Tabora kwa sababu ya uvivu wa kutembea. Kama sina ndugu au cha muhimu cha kunipeleka, basi siendi sehemu kutembea.

Ila sehemu zinabadilika sana. Tutuo na Kiloleli kuna Guest House na Kiloleli kuna fisadi mmona anaitwa Boni kaweka hadi umeme wa Solar. Ukiingia jioni Umeme unawaka, lohh 🙂

Kuvua samaki, lohh wakati wa masika na hasa Kambale na Ngenge.... Mwisho kuogelea. Kilimo cha mpunga, mgongo unauma si kawaida. Ila wakati wa mavuno ndiyo raha hasa karanga za kuchemsha mbichi au njugu za kuchemsha, unakula hadi tumbo linauma maana hujui kusema STOP. Nina imani usafiri ukiwepo mzuri, Tabora itachangamka. Ngoja nikimbie maana tutaharibu topic ya Kandimu (ingawa tumeshaharibu, hahahahaa).
Ni jambo zuri sana kuendeleza miji yetu na tena umenikumbusha mbali sana.Mambo ya ipole,inyonga,Mtakuja na mto ugalla kwenye samaki nayamiss sana kwa kweli!Nasikia siku izi inyonga imeamishiwa wilaya ya Mlale mkoa wa katavi!
 
Inawezekana ingawa kusema ukweli mie kwa kwenda Ipole, mwisho wangu ni Chabutwa na huku upande mwingine niliishia Kiloleli na zaidi ya hapo, siyo mwenyeji sana wa Tabora kwa sababu ya uvivu wa kutembea. Kama sina ndugu au cha muhimu cha kunipeleka, basi siendi sehemu kutembea.

Ila sehemu zinabadilika sana. Tutuo na Kiloleli kuna Guest House na Kiloleli kuna fisadi mmona anaitwa Boni kaweka hadi umeme wa Solar. Ukiingia jioni Umeme unawaka, lohh 🙂
Ni jambo la kushukuru kama miji imebadilika kwa kiasi hicho.Mimi sijafika siku nyingi sana,mara ya mwisho ulivyofika walikuwa wanaongeleaje kuhusu mambo ya uchawi maana miaka ya nyuma ilikuwa inatisha?
 
Back
Top Bottom