Bodi ya TANESCO yaamua kumtimua kazi Mhando!

Hata Dr Idirisa naye afuatiliwe Mhando alifuata yale aliyokuwa anafanya Dr Idirisa kwa kutuletea mgawo wa umeme wa bandia
 
Kabainika aliingia mikataba kwa maslahi yake mwenyewe bila kujali kanuni za kazi yake na kusababishia taifa hasara kubwa. Je, kutokana na kauli yenu ya kukubali kuwa alikuwa na makosa, huyu mtu mnachukulia hatua gani? Kwanza ni mwizi, kaibia taifa na kuliletea hasara kibao kwa hai ya kawaoda huyu inabidi ataifishwe mali zake na achukuliwe hatua kali ili iwe kigezo kwa wengine watakaofuata. Binafsi, napenda yeye pamoja na rais ama waziri yeyote atakayebainika kuwa ni mwezi na kutumia madaraka vibaya, lazima anyongwe ili iwe fundish kwa wengine.
 
Hee....Kwani hii bodi bado ipo hadi leo hii.....Nilidhani ishavunjwa baada ya madudu yote iliyofanya! Imbombo ngafu. Hii kweli bongo
 
angetakiwa aanze rais wa nchi, yeye ndiye kawafikisha wenzie wote hapo walipo kwa UDHAIFU wake! rubbish!

na afikishwe mahakamani siyo kumfukuza tu kama ushahidi kwa kufukuzwa upo na wa kumpeleka mahakamani lazima upo usifichwe... Tumeteseka sana ametuweka sana gizani na wengine walioshirikiana nae nao wawajibishwe haiwezekani alikuwa peke yake.
 
Naomba mwongozo hapa! Hii kitu imewekwa kama photo a jepg, Haina muhuri au kuna utaratibu gani hapa?
 
Kama alifanya makosa na yakajulikana kumwachisha kazi pekee nidio suluhisho au

Kama kila fisadi ataishia kutimuliwa kazi tu basi hakuna hukumu nyengine nahisi mafisadi watazidi kuongezeka nchini
na hapo kila mmoja anatumia msemo wa "Chukua Chako Mapema" ukitimuliwa umeshaula !!!!
 
na afikishwe mahakamani siyo kumfukuza tu kama ushahidi kwa kufukuzwa upo na wa kumpeleka mahakamani lazima upo usifichwe... Tumeteseka sana ametuweka sana gizani na wengine walioshirikiana nae nao wawajibishwe haiwezekani alikuwa peke yake.

Mhando ni kielelezo cha mambo yanavyofanyika serikalini na katika mashirika ya umma. Kama "alitutesa" kwa harakati zake basi jua hayo ni maumivu ya muda mrefu sana ujao; hayaishi na kupanguka kwa huyo mtu mmoja. Mhando kateleza tu na kuangukia kwenye taa kali ya umma (public spotlight). Na itakuwa ni kujidanganya kushangaa alikopata ujasiri wa kuhujumu shirika na nchi kiasi hicho. Sekta ya nishati na ya madini Tanzania zimekuwa mtaji mkubwa sana wa ulaji wa viongozi wakubwa katika taifa. Wanaofanya kazi huko inabidi wa "play ball" au wapishe wenye kujua. Hebu pima jeuri ya vibopa wenye makampuni ya petroli mbele ya serikali ndio ujue wenye nchi ni akina nani.
 
waweza kufafanua?

Hakuna haja ya mimi kufafanua hapa Jamvini. Soma taarifa za migongano ya kibiashara katika TANESCO kuanzia ununuzi wa mafuta, gas, na uagizaji wa vifaa vya umeme. Mgongano huo wa maslahi ya wakubwa ndo umemponza Injinia mwenzangu Mhando. Soma taarifa ya kamati ya Bunge n.k utaona na kujua ninachokisema!
 
Ameachishwa kazi lakini
----hiyo mikataba inaendelea kaama kawaida.
-----anapewa kii nua mgongo kamamstaafuwa kawaida
------------mwisho utasikia mh. Mstaafu
 
Mhando ni kielelezo cha mambo yanavyofanyika serikalini na katika mashirika ya umma. Kama "alitutesa" kwa harakati zake basi jua hayo ni maumivu ya muda mrefu sana ujao; hayaishi na kupanguka kwa huyo mtu mmoja. Mhando kateleza tu na kuangukia kwenye taa kali ya umma (public spotlight). Na itakuwa ni kujidanganya kushangaa alikopata ujasiri wa kuhujumu shirika na nchi kiasi hicho. Sekta ya nishati na ya madini Tanzania zimekuwa mtaji mkubwa sana wa ulaji wa viongozi wakubwa katika taifa. Wanaofanya kazi huko inabidi wa "play ball" au wapishe wenye kujua. Hebu pima jeuri ya vibopa wenye makampuni ya petroli mbele ya serikali ndio ujue wenye nchi ni akina nani.

kweli mkuu kwa mazingira yaliyopo sasa inabidi tubadilishe mfumo mzima kuanzia juu mpaka chini hivi viraka vya kuwaondoa wakina mhando na wengineo haviwezi kumaliza matatizo. huu muda uliopo tufanye upembuzi yakinifu ili 2015 tufanye uamuzi sahihi ili tujinasue kwenye hili tope.
 
Back
Top Bottom