Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 879
- 4,116
Tatizo kubwa la umeme Tanzania linaanza na msimamo wa wanasiasa. Magufuli alisema hakuna kukatika kwa umeme na akaweza kwa sababu aliweka nadhiri yakutokula matapishi yake. Akakata mirija yote ya wauza majenereta na mafuta waliokuwa wananufaika na mgawo wa umeme.
Sasa hivi kila mtu anafungua kituo cha mafuta kwa sababu anaamini kabisa usipoyanunua kwa ajili ya chombo cha usafiri utanunua kwa ajili ya mifumo ya umeme nyumbani. Viwanda vingi vinatumia sana mafuta kuwasha majenerator na baadhi mitambo inaweza ikachakaa kabla ya muda
BODI ya TANESCO hata tungeshusha viumbe kutoka nchi gani bado haitaweza kuvuka Kiunzi hiki kwa sababu haina nguvu yoyote kisheria kupinga wishes za mwanasiasa. Wakipinga wanatoka na wasipopinga watatoka. Lakini pia sometimes bodi hizi nyeti tuzitenge na watumishi wa dola kwa sababu inapotoka press bodi imevunjwa inaleta tafsiri ya kutumbuliwa kwa mwenyekiti wa bodi au kufeli kwake......huyu mtu ni mtumishi ambaye kwa cheo alichokuwa nacho kwenye dola kinatia doa viongozi waandamizi wa dola.
Nadhani ni wakati sasa wa kuchukua tahadhari kabla ya kuteua na baada ya kuteua ili ikiwezekana hawa wazee wetu waliojenga heshima yao muda mrefu wasitiliwe shaka kuhusu uwezo wao wa kuleta matokeo chanya.
Political will ikiwa strong hata kama hakuna bodi mambo yatakwenda kwa sababu kila ukiamka utawaza umeme...kila ukisali kama mtumishi wa TANESCO utasali ukame usitokee kwasababu ndio umepoteza kazi ...kila ukisikia transfoma imeibiwa utaunda mikakati ipatikane na kuweka sheria kali.......kila ukisikia Luku inasumbua utawalipa vijana wakae standby kushughulika na mfumo.
Sasa hivi TANESCO unashindwa kujua tatizo ni maji au nini? Maana mvua zimenyesha ila mgao upo palepale na hakuna kauli yakueleweka kuhusu chanzo cha tatizo. Tuwalinde wazee wetu hawa wamefanya mengi kwa nchi yetu