Bodi ya TANESCO yaamua kumtimua kazi Mhando!

kumuachisha kazi means, Wananchi maskini wa Tanzania wanaenda kumlipa mwizi mamilioni ya shilingi kwa wizi bora aliowafanyia dah!!...hakika haya yanatokea Tanzania pekee.
 
Wapi Zitto's take? Alikuwa akimkingia kifua huyu.

Halafu baada ya kumtimua kitafuata nini? Maana kama ndo mwisho wa mchezo sioni disincentive kwa mwizi mwingine anayetaka kuiba.

Anaangalia anaona hela zipo, ukiiba unatimuliwa tu? Mwisho wa mchezo? Sheeesh.

Tena ndo anafanya kweli haibi kitoto, akitimuliwa anapumzika vizuri hana haja ya kuhangaika.

Wapi TAKUKURU, mchakato wa mahakamani et?
 
Kwa Tanzania yetu hii ata kama angeuza mitambo yote,atapelekwa mahakamani na kesi ikiwahi sana kuisha labda miaka 6 na mbaya zaidi anakuja kushinda na kulipwa fidia tena,jilie tu bwana mhando as life has turn to be the game of opportunity.
 
TAARIFA+KWA+UMMA+001.jpg
 
Huyu Eng alikuwa kero kubwa sana kiasi kwamba migao yote ilikuwa sababu yake na umeme wa dharura ulikuwa sababu yake pia. Ingekuwa china angenyongwa, Kwa vile ni bongo bora afikishwe mahakamani ili apunguze fedha zake za ufisadi hata kwa kuhonga au kuwalipa mawakili.
 
Kwa hiyo waziri na katibu wake wameshinda, nasikia board ilikuwa inamkingia kifua wameishia vipi sasa, na tena kwa maana hiyo na board nayo si inaingia kwenye jahazi hilo kwa sababu na wao si ndio walibariki hayo madudu ????
 
Kumwachisha kazi hakuna tofauti na kumstaafisha maana atalipwa haki zake zote. Uamuzi wa haki bodi ingemfukuza na kuamuru afunguliwe mashtaka

Haya mawazo yako hayawezi kufanya kazi kwa Tanzania ya sasa japo ni mazuri.
Labda kama JK amebadili mtizamo wake baada ya kutoka Oman, inawezekana Mhando akapelekwa kwa Jaji Lugakingira
 
Huyu Eng alikuwa kero kubwa sana kiasi kwamba migao yote ilikuwa sababu yake na umeme wa dharura ulikuwa sababu yake pia. Ingekuwa china angenyongwa, Kwa vile ni bongo bora afikishwe mahakamani ili apunguze fedha zake za ufisadi hata kwa kuhonga au kuwalipa mawakili.

Mkulu anaweza kuwaambia wananchi kesi za watu kama hawa zinahitaji umakini sana hivyo kabla ya kuwapeleka mahakamani uchunguzi wa kina unahitajika kama alivyofanya kwa watuhumiwa wa EPA
 
Hili si pigo kwa Mh. Zitto wala Mh. Gosbert Blandes zaidi ni pigo kwa sisi wananchi ambao ndio tunawachagua wenzetu kama hao waheshimiwa tukawapa matumaini na nguvu waendelee kuwa vigeugeu kusimamia maslahi ya wachache mafisadi kama alivyokuwa Mhando badala ya wananchi.

Hii ni warning kwa mtu yeyote anayepewa dhanana katika huduma za umma kuwa mwisho wa siku hakuna atakaye baki hata kwa utetezi wa yule mlaghai shupavu toka enzi za Adamu - Lusifer - Ibilisi; hata kama mfumo ungemtetea WANANCHI ambao ndio maboss wakuu wa viongozi wote wangemtoa tu siku moja. Ndivyo itakuwa kwa Nyoni, ndivyo itakuwa kwa Gosbert (nawahakikisheni kuwa hatarudi tena Bungeni baada ya 2015 maana hata kwa kuchakachua, malaika waibuka na kuonyesha kura halali zitakazo pigwa) na hata kwa Zitto ataangukia pua kama hataamua kuchukua maamuzi magumu na kujirekebisha kujali maslahi ya umma kama alivyokuwa mwanzoni.

Nakubaliana na Mwanakijiji kuwa sasa na Mwenyekiti wa Bodi Mzee wetu Mjeshi afuate akapumzike maana alishindwa kabisa kazi aliyopewa.

Kweli inaendelea kushinda wakati si-kweli inabaki mahala pake pa kuona aibu.
 
ZZK anamtetea mwizi muhando mpaka povu linamtoka ndio anaota kuja Kuwa rais wangu? Labda akawe raisi wa bongo fleva cdm wakimpitisha kura yangu na familia yangu nampa Dovutwa.....
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom