The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 15,396
- 12,979
Mr. Zero hizi taarifa umezisikia wapi?Binafsi siko nchini lakini nilianza kukatwa mkopo huo mwaka 2007 kwenye mshahara wangu ambapo nalipa TZS 25,000 kila mwezi na denni ni TZS 5,000,000. Ukiangalia deni ni kubwa kuliko pesa waliyo nikopesha, nilikwenda kuwauliza bodi wakadai watashughulikia lakini bado nakatwa kiwango hicho hadi leo.
Mbaya zaidi baadhi ya classmates wangu tuliokuwa darasa moja hawadaiwi na wote tulipewa mkopo huo, wengine wanandaiwa TZS 2,000,000. Kwa hiyo bodi hawana data za wakopaji walicho fanya ni kukadiria madeni.
Sasa mkuu labda tusubiri walioko TZ kwa sasa watupe details.
hebu njoeni mlipe madeni bana, watanzania wengine nao wanahitaji kusoma, ebo.moderator, naomba hii ikae kwa muda ili tupate some infomation kutoka kwa walio nchini.
nasikia bodui ya mikopo leo imetoa majina ya wanaodaiwa na wametowa siku 30 otherwise wanakufikisha kotini.
kuna wengine kama sisi ambao tulimaliza zaidi ya miaka 13 iliyopita nasikia kuwa majina yetu yapo.
mwenye info naomba atuletee hapa, sitaki nijekuwa arrested airport nikirudi likizo.
hebu njoeni mlipe madeni bana, watanzania wengine nao wanahitaji kusoma, ebo.
Mje mlipe.
Uzalendo ni kulipa hilo deni.
Sio kukazania ufisadi,ufisadi
wakati na huo ni ufisadi.
Mawazo yako hayo. Wakati tunaanza hiyo mikopo haikuwepo ilikuja katikati, na wala sikuwahi kupata barua kunipa mkopo wala barua ya kunitaarifu ni kiasi gani nadaiwa. sasa ulitaka nilipeje. Hiyo bodi ya mikopo haikuwepo!!!
Hebu tuache hadithi na wengine wasome. Nadhani ni vyema kila mtu ajipeleke ili alipe. Turudishe hizo pesa jamani na wengine wasome otherwise ni ubinafsiKwa wale mlimaliza miaka 12 iliyopita na serkali ilikaa kimya huo mkataba ia time barred .hapa wakienda mahakamani ni objection mapemaa
Mawazo yako hayo. Wakati tunaanza hiyo mikopo haikuwepo ilikuja katikati, na wala sikuwahi kupata barua kunipa mkopo wala barua ya kunitaarifu ni kiasi gani nadaiwa. sasa ulitaka nilipeje. Hiyo bodi ya mikopo haikuwepo!!!
Waswahili bwana ni watu wa ajabu.
Wasipopewa mkopo shida tupu. Walipewa mkopo leo wanajifanya kuuliza sijui barua sijui statement, hivi kweli hujui ulikopa shilingi ngapi na unatakiwa kulipa shilingi ngapi?
Hii inaonyesha hamkuwa na nia ya kulipa ndio sababu mmesahau madeni yenu ni shilingi ngapi!
Lipeni au wawapeleke mahakamani. Hivi bond zenu ilikuwa ni nini vile? zile nyumba za baba zenu? na mashamba yao?
Mama yangu weeeeeeeeeee mmekwisha. Kalipeni haraka wengine wasome.

Kaka kumbe unaushahidi wa kujitetea!Kwanza hiyo mikopo wakati inaanza tulilazimishwa kuomba kwa kujaza form. Kwa kumbukumbu yangu sikuwahi kupata barua ya kusema nimepata mkopo na ni kiasi gani. Sasa kama bodi imeishiwa pesa na wanataka kuokoteza kila mahali then watumie utaratibu mzuri badala ya kuzuka na kutoa majina ya watu magazetini. Hawajui kuwa wanaweza kuchafua majina ya watu kwa utaratibu huu???