Mwaikibaki
JF-Expert Member
- Mar 19, 2015
- 2,975
- 3,624
Wadau,
Ni jambo la kutia moyo pale ambapo wakopaji wanarejesha mikopo kwa wakati ili kuwezesha wengine wapate msaada kama wao.
Hapa nyumbani nina kijana wangu ambaye miaka ya nyuma sana alipata mkopo wa daraja C ambao kwa miaka hiyo ilikua daraja la mwisho.Baada ya kuhitimu chuo alipata kibarua na mara moja akaanza kikatwa deni kwa mujibu wa sheria..alilipa kwa muda wa miaka 2 akamaliza deni lake.
Hata bodi ya mikopo walipochapisha majina ya wadaiwa yeye HAKUWEMO.!
Ghafla jana tu bodi ya mikopo imeleta taarifa kupitia kwa mwajiri mpya wakionyesha kua kijana alilipa kiasi cha laki nne tu!na ana deni kubwa.
Nimejaribu kuwapigia hawa jamaa ili watoe maelezo ila hawapokei simu zao hapa napanga kuwawndea ofisini ili watoe ushahidi wote.
Ninachojiulizia ni kuwa hii Bodi ya mikopo haina taarifa za kutosha za miaka ya nyuma au ni aina gani ya utendaji wanaaofanya wa double standards???
Hii inatia aibu na kukarahisha!