Bodi ya Mikopo: Mmeanza kujichanganya kwenye kumbukumbu za urejeshaji mikopo??

Mwaikibaki

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,975
3,623
Wadau,
Ni jambo la kutia moyo pale ambapo wakopaji wanarejesha mikopo kwa wakati ili kuwezesha wengine wapate msaada kama wao.

Hapa nyumbani nina kijana wangu ambaye miaka ya nyuma sana alipata mkopo wa daraja C ambao kwa miaka hiyo ilikua daraja la mwisho.Baada ya kuhitimu chuo alipata kibarua na mara moja akaanza kikatwa deni kwa mujibu wa sheria..alilipa kwa muda wa miaka 2 akamaliza deni lake.

Hata bodi ya mikopo walipochapisha majina ya wadaiwa yeye HAKUWEMO.!

Ghafla jana tu bodi ya mikopo imeleta taarifa kupitia kwa mwajiri mpya wakionyesha kua kijana alilipa kiasi cha laki nne tu!na ana deni kubwa.

Nimejaribu kuwapigia hawa jamaa ili watoe maelezo ila hawapokei simu zao hapa napanga kuwawndea ofisini ili watoe ushahidi wote.

Ninachojiulizia ni kuwa hii Bodi ya mikopo haina taarifa za kutosha za miaka ya nyuma au ni aina gani ya utendaji wanaaofanya wa double standards???

Hii inatia aibu na kukarahisha!
 
hapo mkuu umekwama lazima ulipe! Nakumbuka kuja jamaa zangu walimaliza kulipa deni ila walisahau kitu kimoja tu ambacho kuchukua clearence letter iliwalazimu walipe!
Note ukimaliza kulipa den hakikisha umepata barua ya kumaliza deni lako lastly kama una cash ni bora uwape ujipange vzr!
 
Nenda na evidence (receipt) za repayment zako ,omba nakala from employer, then wakafanye reconciliation, huwa inatokea kama michango ya nssf, huwa wanalipwa sema wazee au vijana wavivu Ku post katika akaunti za wakopaji, mostly uende uwaconvince, na kwa uzoefu wana clear
 
Kwa miaka hio daraja c ilikua ni asilimia 60 au 40 sasa kwa jinsi marejesho yalivyo ya bodi ya mikopo no nadra sana kuweza kurudisha mkopo wote ndani ya miaka miwili maana approximately mikopo hurange kati ya milioni 6-12 kutokana na kozi either ya miaka 3 au 4 chuoni hivyo kwa ile 8% per month ni ngumi kuweza kurudisha mkopo wote...
 
Back
Top Bottom