BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Kuna kitu kimoja ambacho kimekuwa kikilalamikiwa chinichini mara nyingi kwenye ulimwengu wa soka.
Ishu ya baadhi ya timu kucheza saa nane mchana wakati wa jua kali imekuwa ni kama kilio cha baadhi ya timu ambazo zinaonekana hazina nguvu kubwa.
Simba na Yanga wao ni wakubwa, TFF na Bodi ya Ligi wamekuwa na hofu ya kupanga michezo ya timu hizo saa nane.
Inawezekana wanafanya hivyo kwa lengo la kibiashara ili inapotokea wamecheza muda huo viwanja visiwe na mashabiki wachache, hiyo ni hoja ya msingi lakini vipi kuhusu maumivu wanayopata wale wanaocheza mchana.
Kuna viwanja ambavyo vina nyasi bandia, napotokea timu zinacheza mchana saa nane na kuna jua kali maumivu yake huwa si ya kitoto.
Kuna mchezaji mmoja aliwahi kuniambia unaweza kuumia na ukashindwa kulala chini kusubiri machela.
Bodi ya Ligi iacheze hizi mambo
Hata kama wanaangalia biashara lakini kuwachezesha saa nane kwenye viwanja vyenye nyasi bandia huku Simba na Yanga wao wakiwa ‘watoto’ wa kipekee siyo sawa.
Kama ni ratiba za TV basi hata hao wakubwa wahusike, isiwe ni timu ‘ndogo’ tu ndizo ziungue kwenye nyasi.
Ushauri wangu, Azam TV na Bodi ya Ligi waangalie kuhusu ratiba zao, kama kuna viwanja zaidi ya viwili ambavyo watu wanaweza kucheza usiku, hakuna ulazima wa kuchezesha timu saa nane mchana waungue na jua kali.