Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Tido Mhando, ameongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, akitangaza kuanzishwa kwa mfumo mpya wa kidigitali wa kupata Ithibati na Kitambulisho cha Uandishi wa Habari (Press Card).
Kupitia mfumo wa TAl-Habari, waandishi sasa wataweza kujisajili mtandaoni kwa urahisi zaidi .
Mambo muhimu anayopaswa kuwa nayo mwombaji ni pamoja na:
Baada ya kujisajili, mwombaji atapokea msimbo wa
SMS na barua pepe ili kuendelea na hatua za kujaza taarifa, kufanya malipo, na kuwasilisha ombi lake.
Kitambulisho hiki kinatumika sehemu yoyote ya shughuli za kihabari - ndani na nje ya taasisi.
Ni kwa mujibu wa Kanuni ya 17(a) ya Sheria ya Huduma za Habari, inayowalenga Wahariri, Watangazaji, Waandishi wa kujitegemea, Wapiga picha, Waandaaji wa vinindi, Wanafunzi wa uandishi, na hata Wa. V shi wa Habari wa kigeni.

- Picha ndogo (passport size)
- Vyeti vya elimu
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
- Barua ya utambulisho kutoka taasisi au kama ni freelancer
- Ada ya Ithibati ya TZS 50,000