JAB: Hakuna muda wa nyongeza usajili waandishi

JAB: Hakuna muda wa nyongeza usajili waandishi

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,074
Reaction score
7,068
Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), imesema haitatoa muda wa nyongeza kwa waandishi wa habari kujisajili,na kwamba kufanya kazi za kihabari bila usajili ni kosa kisheria.

Kaul hii imebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Patrick Kipangula, ambapo amesema kuwa baada ya muda uliowekwa kumalizika, waandishi watakaoshindwa kujisajili hawataruhusiwa kufanya kazi zao.

“Tunatoa wito kwa waandishi wote kuhakikisha wanakamilisha usajili mapema. Kufanya kazi za habari bila ithibati ni kosa kisheria na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaokiuka,” alisema Kaimu Mkurugenzi.

Soma Pia: Bodi ya Ithibati yawataka waandishi wa habari kujisajili ili watambuliwe rasmi


JAB imeeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha taaluma ya uandishi wa habari inazingatia maadili na viwango vya kitaaluma vilivyowekwa kisheria

 
"....when they came for me...."
Sema tu itafurahisha zaidi pale tukija kugundua kuwa hata huyo anayetoa maelekezo ya kushughulikiwa wengine naye anapokea maelezo kutoka juu yake, then tukigundua 'chanzo kikuu' itabidi tuzimie kwa muda!
 
Back
Top Bottom