Inaoneka Tanznaia tunachagua chama na hatuchagui kiongozi. Viongozi wote ni mafisadi lakini inabidi tuangalie fisadi zaidi ni nani.. Chamuhimu kuwepo viti vingi vya upinzani bungeni angalau 55%/45% hapo ndio patakua patamu, lakini upande mmoja ukizidi sana basi hapo tujue hata kama tutamchagua nani ufisadi utaendelea kama kwaida,
Funguneni macho na mtizame hapa Afrika je kuna nchi gani isiokua na mafisadi hadi leo??
Na vita na vurugu havileti maendeleo, ingawa nishawahi kusikia badhi ya watu wakishabikia vita au kumwaga damu, Vita ikitokea basi mjue hata kama tutafanyeje hatutakuja kupata maendeleo. Kila mtu atake kufa kwenye vita ujue italeta kisasi zaidi na zaidi na zaidi na chuki. Watanzania tulinde kwa hali na mali usalama wetu na amani yetu, ndio heshima pekee tuliokua nayo kwa sasa
Mtu anayepiga pushapu jukwaani amejiandaa kwenda kuvunja na kuiba pesa za hazina yetu.
Lowasa mnasema ni mgonjwa na kweli afya yake sio imara sana japo kama baba au kiongozi wa taifa tunamtaka aendelelee mbele ili atimize ndoto yake ya kututoa hapa tulipo.
Naamini kua kwa umri wake na jinsi wanavyomwita mgonjwa hawezi kuiba.
Hakuna mgonjwa anayeweza kuwa jambazi .
Majambazi ni haya masisiem yanayonyanyua vyuma na kupiga pushapu na kupitia madirishani kwa msemo wa kijambazi wa hapa kazi tu ya kuvunja na kupora.
Haya ni maneno mara nyingi ya majambazi na wezi wawapo kazini.
Mgonjwa kamwe hawezi kuwa mwizi.
Ugomvi wa kifamilia usifanywe kuwa ni ugomvi wa kitaifa.
Kuna kakundi kadogo ndani ya CCM ambako hakamtaki Lowasa na kamefanikiwa kuuhadaa ulimwengu kuwa Lowasa ni adui yao wakati sote tunajua kuwa Lowasa ni kipenzi cha watanzania.
Na wote wako tayari kwa lolote endapo kura zao zitauzwa au kuchakachuliwa na mtu yoyote .
Magufuli hapendwa na watu toka moyoni anapendwa kwa woga na mapesa yanayotolewa na sisiem na serikali yake.
Tuliwaona watangaza nia wa ubunge ndani ya CCM walivyokua wanakamatani kwa rushwa na rafu na hata kupigana marungu.CCM hata ukimuuliza shetani atakuambia ndio wanaotoa rushwa ya uchaguzi kila kona ya nchi. Wanawahadaa watu wa vijijini kwa rushwa za TASAF bila kujua kua baada ya uchaguzi wataingia mitini.
Bila rushwa na rafu CCM kamwe hiwezi kushinda na mwaka huu ni man to man. Hakuna kulala na ukiiba kura ni bora ungekua kibaka kwani utakipata cha mtema kuni.