Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 38,249
- 24,839
Ndugu zangu Watanzania,
Katika historia ya Taifa letu na tangia kuanza kwa mfumo wa Vyama vingi hapa Nchini. Rais wetu Mpendwa na Mama yetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan anakuwa Mgombea wa kwanza Mwenye Mvuto na shawishi Mkubwa sana kwa wapiga kura.
Ni Mgombea ambaye amefanikiwa kuiteka mioyo ya mamilioni kwa mamilioni ya wapiga kura. Ni mgombea ambaye anakubalika , kupendwa na kuaminika sana kwa wapiga kura. Sera na ajenda zake zimekuwa zikihusu maisha na ndoto za watu na namna ya kuwainua watu kiuchumi na kuwawezesha kutimiza ndoto zao bila kikwazo cha aina yoyote ile.
Ni Mgombea ambaye amebeba ajenda zenye kuleta matumaini na nuru kwa Maisha ya watu. Ndio sababu ya kupokelewa kwa kishindo na watanzania maelfu kwa maelfu. Ndio sababu watu wanamiminika na kufurika kwenye mikutano yake,ndio sababu ya watu kujiandaa kumpigia kura za ndio kwa wingi mkubwa. Ndio sababu ya watu kuwa na imani naye na kumwamini sana.
Kwa sababu Wameona na kutambua ya kuwa Mama ni mtu wa kazi na matendo na siyo maneno Maneno yasiyo tekelezeka. Wameona kazi kubwa iliyofanyika ndani ya muda mfupi wa uongozi. Ndio sababu watanzania kwa mamilioni wanataka kumpa miaka mingine mitano ili aendeleze kazi nzuri aliyokwisha kuianza.
Makundi yote yameridhia na kusema kwa kauli moja kuwa Mama ndio chaguo lao. Wakulima wanasema ni Mama tu maana wameona matunda ya ndani ya muda mfupi. Ikumbukwe ya kuwa kwa kipindi kifupi tu cha uongozi wake Mama yetu Mpendwa ametoa ruzuku ya Billion 726. Hali iliyopelekea kushuka kwa pembejeo hususani mbolea.
Ndani ya muda mfupi ameongeza bajeti ya kilimo kutoka Billion 250 hadi Trilioni moja point 2. Amesogeza huduma za kijamii karibu kabisa na wananchi. Na sasa wanafunzi wanapata Elimu karibu kabisa pasipo kutembea umbali mrefu. Sasa zahanati na vituo vya afya vinapatikana jirani kabisa na mwananchi na vinatoa hudumu bora kabisa.
Ukienda kwa vijana unakuta katoa ajira maelfu kwa maelfu. Mfano ndani ya muda mfupi ameweza kuajiri walimu zaidi ya Elfu 89. Na ndani ya siku 100 za uongozi wake atatoa zingine takriban 7000 pamoja na za afya takribani 5000.anaendelea kumwaga ajira mitaani kwa kadri hali ya uchumi inavyoruhusu.
Hakuna aliyeachwa nyuma au kusahaulika katika uongozi wa Rais Samia. Kila mmoja kafikiwa na mkono wa Mama. Ndio maana watanzania wanaendelea kumuunga mkono Rais wetu na kujitokeza kwa wingi sana kwenye mikutano yake ya kampeni.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.