PostGE2025 Bodaboda na Machinga Dar: Desemba 9 hatufungui biashara

PostGE2025 Bodaboda na Machinga Dar: Desemba 9 hatufungui biashara

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,438
Reaction score
14,672
Shirikisho la Vyama vya Madereva Bodaboda na Bajaji na Uongozi wa Machinga mkoa wa Dar es Salaam, wameahidi kutofanya kazi siku ya Disemba 9, 2025, kwa madai kuhofia kuingizwa kwenye mkumbo wa watu wanaofanya vurugu, kufuatia tetesi za kuwepo kwa maandamano yanayohamasishwa mitandaoni.

Viongozi wa Shirikisho hilo na wa Machinga mkoa wa Dar es Salaam, Said Kagomba na Namoto Yusuph wakitoa salamu zao katika Kongamano la kupongeza Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la 13 jijini Dodoma, wameweka wazi msimamo wao kuelekea siku ya Disemba 9, 2025.

Kauli hiyo imeungwa mkono na Mkuu wa wilaya ya Ilala na mwenyekiti wa kamati ya usalama ya wilaya hiyo Edward Mpogolo, aliyeahidi kulifikisha katika vikao husika, huku Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Ilala Kamishna wa Polisi Yustino Mgonja, akieleza mikakati ya jeshi hilo katika kuwalinda raia na mali zao.


 
UVCCM wa mchongo
a17bcad5-213d-4a9b-a478-ac980573a020.jpeg
 
UVCCM ndiyo wanafanya maigizo ya kuwa wao ndiyo bodaboda na machinga
 
Bora wafanye hivi aisee maana mwanzoni watu wengi walikufa ilihali hawakuhusika na maandamano
 
Wakulima tunaogopa hata kulima mashamba yetu yule mtangazaji wenu uchwara wa CNN akiona shamba limepaliliwa anasema ni ushahidi wa kaburi la halaiki
Tatizo hata mambo ya teknolojia hujui, ukiwa magonjwa na akili zinapotea.
 
Wakulima tunaogopa hata kulima mashamba yetu yule mtangazaji wenu uchwara wa CNN akiona shamba limepaliliwa anasema ni ushahidi wa kaburi la halaiki
Sheikh Bakonzi una vituko,
Hutaki vichwa vya waandamanaji tena?
 
Kwani tarehe 9 kuna machafuko yanakuja ? siku ya uhuru raia hawana uhuru wa kutoka na kujitafutia chochote🐼
 
Back
Top Bottom